Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi

Pascal Mayalla Haya Mataifa hayawezi kuunga mkono juhudi za Mh. Rais, hasa pale ambapo tunaanza kufanikiwa katika kuwabana wanyonyaji wa maliasili zetu. Watakuja na kila aina ya propaganda, na watatumia vyombo na taasisi zao kutuchafua. Mambo ya aina hii yamekua yakitokea sio tu kwa Tanzania, tumeona propaganda za namna hii zikienezwa kwa nchi nyingine zilizokataa unyonyaji wa mataifa ya maghalibi na zilizoamua kusimamia usawa katika kusimamia maliasili za nchi.

Sisi watanzania hatupaswi kurudishwa nyuma na propaganda dhaifu kama hizi, inafaa tusimame kwa pamoja, tumuunge mkono Mh. Rais wetu, na tuendelee mbele. Tanzania ki uhalisia tulihitaji kiongozi wa kaliba ya Mh. Magufuli, sasa tumempata tumtumie katika kipindi hiki cha miaka 10 na tutafikia pazuri.
Okay unaweza ukawa na hoja nzito kwamba mataifa ya magharibi hayatutakii mema ila je unaweza kunisaidia lipi walilosema hapo ni uongo?? Ina maana uchumi haujashuka kma walivyoweka takwimu hapo au ina maana kweli demokrasia haijanyongwa kama wanavyodai?? Ni vizuri ungesema kwamba serikali ifuatilie ikomeshe vitendo vinavyoonyesha viashiria vya udikteta na uminywaji demokrasia bila kusahau waweke vipaumbele vya kumuokoa maskini wa nchi hii ila kusema tu WAZUNGU hawatutakii mema kisa wameongea mambo yenye uhalisia hapa kwetu sioni kama unatendea haki uchambuzi huu

Alafu kituko media hizi hizi za wazungu ziliwahi kumshindanisha magufuli kma kiongozi bora wa afrika mbona mlikubali ile article.... Kuna article ya economist ilimuita rais mzalendo na alisifiwa sana mbona hamkuwahi lipinga hili magazine iweje leo wakikosoa ndio mnasema wapuuzwe ila wakisifiwa huwa mnakuja na article zao humu kwenye jukwaa??
 
Yaani makinikia mlivyowazingua kwa mbwembwe ya media sasa na wao wanaanza kuwachafua taratiibu
Kama ni kete ndo kwanza wanazichanga

Unapigwa na media then unapigwa kidiplomasia afu wawekezaji wanakata kamba afu unawekewa vikwazo ukibishi zaidi unaletewa vita vya wenyewe kwa wenyewe wanachukua mali bure huku wakiwa supply siraha na ulinzi afu ukieleweka unawapa gharama za kukujengea nchi upya afu unawapa mikataba unayokukandamiza zaidi then wameshunda vita

Tulitakiwa tutumie busara sana kwa vita ile
 
pascall wewe ni mwandishi kanjanja tu, acha unafki na kujipendekeza, hujui kinachoendelea nchini ? unaona uchumi unakuwa kwa kasi ?

ngoja nikushauri kitu......
-haya mambo ya kisiasa unayoandika pengine kwa kuogopa kutekwa/kupotezwa kama wenzio kina Azory bora uachane na siasa, uandike mambo mengine kwa usalama wako na familia yako.
-kuliko kujipendekeza kwa kumsifia raisi sijui wanamuonea ni bora uache kuandika hizo habari....
-credibility yako inashuka kwa kiwango cha SGR

mwisho naona unautafuta Uteuzi kwa gharama yeyote yule, wacha hao wanaoona uozo na ubovu wa serikali hii watusaidie kupaza sauti, yes nasaoti tuwekewe economic sanctions.
 
Tupo vizuri mkuu. Rest assured!
Fanya kazi.
Enzi za kupiga madili na ujanjaujanja ndo zimeshaisha hivo.
Labda hadi mtakapotuletea tena Rais mwenye sura na tabasamu nzuri.
Tupo vzuri kivp wakati watanzania 70% wanasurvive kwa chini ya buku 2 kwa siku. Pesa imepungua kwenye mzunguko ndio maana watu wanalalamika sasa kwani mkiwekeza kwenye sekta ya kilimo ambayo inamgusa mtanzania moja kwa moja mtapungukiwa nini??? Unafkiri SGR inamnufaisha nini mkulima wa mpanda au mtwara?? Ila mngewekeza kwenye kuwasaidia wafanye kilimo cha kisasa ili wasitegemee mvua na mkawawezesha mazao yao wauze mpaka nje ya nchi unafkiri kelele za vyuma kukaza zingekuwepo

Hii ni nchi yetu sote mkikosolewa mnachukua hatua sio mnapuuza kma wwe unavyofanya...

Kuhusu madili zimeishaje mbona E passport wamepiga hela..... Nida walipiga hela.... Vipi taarifa ya CAG kila mwaka ufisadi wa mabillion.... Au madili gani unayosemea wewe
 
Mimi naona hajawakosea kitu ila tatizo la hawa wazungu walizoea kunyenyekewa,kulambwalambwa na hii hali tokea uhuru ipo kama unakumbuka Kikwete na watangulizi wake kila walipomaliza kuapishwa haikuchukua muda walienda kwa wazungu,hii iliwafanya wao waone uhitaji na umuhimu wao Tz hata kama walijua ss ndio tunawafanya wawe juu,huhuyu JPM kaanza vibaya hataki kwenda kuwasabahi,hataki kuwakaribisha,biashara zao anazitilia vimavi tena hataki hata mazungumzo nao kwani anahic akizugumza nao watamzidi hoja naye kushindwa hataki kwani ni JIWE,na kama ujuavyo dawa ya jiwe ni kulipasua tu hata kwa mitalimbo mizito,JPM ameanza ghafla sana ukizingatia watangulizi wake wameshawazoeza hawa wazungu vibaya,ilipaswa aende nao taratibu tena kwa akili saaaana si ubabe na kukurupuka hivi,kitakachofuata atavunjika au kupasuka maana kama ni mfupa umeshakomaa,hawa jamaa wakiamua kukuondoa madarakani huchukui muda hata ukiwa na haki,mfano ni LIBYA,IRAQ nk, ni nchi nyingi,hataki kujifunza mbinu za kula na kipofu,haya maandamano na vitisho unavosikia kila kukicha si dalili nzuri kuna kitu kinatafutwa,asitegemee jeshi maana jeshi lenyewe linatumia silaha ambazo zimetengenezwa na wao wazungu,mbaya zaidi kajenga chuki na wapinzani hawa ndio wabaya zaidi kwani hakuna vita mbaya kama vita vya ndani,kajenga chuki na wananchi wake hii ndio balaa zaidi ,hivyo ni suala la muda tu hawa jamaa wanatafuta mbinu ya uhakika ya kummaliza,Ni lazima ajitazame saana wakishindwa sehemu zote watasubiri ktk uchaguzi ujao akumbuke hata zile karatasi za kura zinatoka kwao,mnaweza mkapiga kura kwake ikageuka ikaenda kwa mgombea upinzani then ye akaonekana ameshindwa na ye kukubali kushindwa hataki,asishangae hata katk serikali yake kuna watu wameshwawekwa ni vibaraka wa wazungu tena ni watu wake wa karibu sana ,wanamchota tu,ngoja tusubiri ni suala la muda,wao wana usemi usishindane na serikali ila wazungu nao wana usemi usishindane na aliyekuzidi,baba ni baba hata kama akitembea na kichaa au house girl wako atatbaki kuwa baba na yule housegirl au chizi pia atakuwa mama yako,busara ni mhm saaaana kuliko ubabemwao wapate na sisi tupate sehemu yetu.
 
Ila mwandishi anafurahisha kwaiyo Magufuli na Nyerere ni madikteta!sasa tunaomba atuaeleze wao waingereza walipokuwa wanatutawala walifanya yapi ili tulinganishe na haya ya hawa madikteta wawili.
 
Wanaweweseka hao. Walizoea kujisombea madini na resources zetu huku wakitusifia kua uchumi wetu unapanda?

Nchi imepata Rais mwenye akili na anayewajua janja yao, sasa wameanza propaganda za kishenzi.

Kama uchumi unadorora si watuache kama wanaweza?

Ukisema wanaweweseka so sahihi lazima kujiuliza kwa mini kelele.zimekuwa nyingi nje wanalalamika ndani wanasema vyuma vimekaza lazima kujitahidi kuondoa hali hiyo kiongozi mzuri in yule anayesikiliza anaowaongoza.

Lakini ikitokea kila anayeonya na kukosoa anapewa kila jina baya iko siku utatoka uchi na watu watakuacha uonekane kituko.
 
Pascal Mayalla Haya Mataifa hayawezi kuunga mkono juhudi za Mh. Rais, hasa pale ambapo tunaanza kufanikiwa katika kuwabana wanyonyaji wa maliasili zetu. Watakuja na kila aina ya propaganda, na watatumia vyombo na taasisi zao kutuchafua. Mambo ya aina hii yamekua yakitokea sio tu kwa Tanzania, tumeona propaganda za namna hii zikienezwa kwa nchi nyingine zilizokataa unyonyaji wa mataifa ya maghalibi na zilizoamua kusimamia usawa katika kusimamia maliasili za nchi.

Sisi watanzania hatupaswi kurudishwa nyuma na propaganda dhaifu kama hizi, inafaa tusimame kwa pamoja, tumuunge mkono Mh. Rais wetu, na tuendelee mbele. Tanzania ki uhalisia tulihitaji kiongozi wa kaliba ya Mh. Magufuli, sasa tumempata tumtumie katika kipindi hiki cha miaka 10 na tutafikia pazuri.

Hivi katika mafisadi wa Tanzania je kuna fisadi yoyote ambae ni mzungu?

Au katika watu ambao walikuwa wanatumia madaraka vibaya na kusaini mikataba je kuna mzungu yoyote alisaini mikataba kwa ajili ya Tanzania?

Hii Dhana ya kusema wazungu wanatuonea wivu coz serikali kwa sasa inabana matumizi na inazuia rushwa wao kama wazungu wanaadhurika vipi?
 
Tupo vzuri kivp wakati watanzania 70% wanasurvive kwa chini ya buku 2 kwa siku. Pesa imepungua kwenye mzunguko ndio maana watu wanalalamika sasa kwani mkiwekeza kwenye sekta ya kilimo ambayo inamgusa mtanzania moja kwa moja mtapungukiwa nini??? Unafkiri SGR inamnufaisha nini mkulima wa mpanda au mtwara?? Ila mngewekeza kwenye kuwasaidia wafanye kilimo cha kisasa ili wasitegemee mvua na mkawawezesha mazao yao wauze mpaka nje ya nchi unafkiri kelele za vyuma kukaza zingekuwepo

Hii ni nchi yetu sote mkikosolewa mnachukua hatua sio mnapuuza kma wwe unavyofanya...

Kuhusu madili zimeishaje mbona E passport wamepiga hela..... Nida walipiga hela.... Vipi taarifa ya CAG kila mwaka ufisadi wa mabillion.... Au madili gani unayosemea wewe

Una akili wewe.
Nakubaliana 100% kuhusu serikali kuwekeza kwenye kilimo ambacho hubeba wananchi wengi.
Hivi kabla ya JPM ni asilimia ngapi walikuwa wanasurvive juu ya buku 2?
Kuhusu SGR inamnufaisha nini mkulima wa Mpanda na Mtwara, unanikumbusha hoja ya Nape na Umuhimu wa Bombadier. -Tafuta wachumi watakufafanulia hili.
Nani kapiga hela kwenye E passport - ni muhimu tukapata facts halafu tuone kama hatua hazitachukuliwa. Report za CAG zipo kila mwaka. Tunapaswa tujadiliane UFISADI gani ulioreportiwa hauchukuliwi hatua? Mkuu si kwa JPM. Leta facts za UFISADI wa kipindi cha uongozi wake ili tushirikiane kumsuta JPM
 
Mimi nimejaribu kuiangalia hiyo graph kwa makini nimeona tangu mwaka 2000 mpaka mwaka jana tufanya vizuri tu hao walioandika hako kapropaganda niwatumie tu salamu wafanye kazi ya kuitangaza na kuipamba nchi yao watakuwa wanasaidia kuiweka nchi yao mahali pazuri kwakuwa vita ya uchumi bado inaendelea. Kwa watanzania wenzangu siku zote mtu anapoamua kuacha ya kwake na kuangalia ya wengine jua vipo anavyovitamani kuvipata kutoka kwa hao. Na kwa sasa hakuna vya dezodezo. Kutwa kucha wao hawalali wanahangaika na Afrika tu kwasababu vipo tunavyowazidi na laiti kama aridhi hii wangekuwa nayo wao jumlisha ubaguzi wa rangi msitegemee kwamba tungeonekana ni binadamu. Leo kuna baadhi ya watu bado wanawasikiliza hao kutoka mataifa mengine kwakuona kwamba eti ndo wakumsaidia. Mi nadhani kumesha pambazuka.
 
Ukisema katukanwa Magufuli, wakati huo huo anatajwa pia Mwalimu Nyerere na ujamaa mbovu, ulio unguza nyumba za maelfu na kuwa rundika makambini kutekeleza Ujamaa basi lengo la mwandishi wa makala hiyo litakuwa halijatimia kabisa! Kwa kifupi imetukanwa Tanzania toka huru mpaka hapa ilipo! Je, kumuita Magufuli, Mr. baada ya Dr. ni sahihi? Kama mwandishi anashindwa kuelezea vizuri wasifu wa mwakilishi wa nchi , iweje tuamini maneno yake na kuyashikia bango? Kwa maoni yangu hiyo 'Tanzania' aliyoiandika mwandishi ni ya 'Kusadikika' siyo halisi!
 
Ukisema wanaweweseka so sahihi lazima kujiuliza kwa mini kelele.zimekuwa nyingi nje wanalalamika ndani wanasema vyuma vimekaza lazima kujitahidi kuondoa hali hiyo kiongozi mzuri in yule anayesikiliza anaowaongoza.

Lakini ikitokea kila anayeonya na kukosoa anapewa kila jina baya iko siku utatoka uchi na watu watakuacha uonekane kituko.
Mkuu.
Unaporekebisha nchi ambayo ilikuwa na uhovyo mwingi kwa kiasi tulichokuwa tumefikia, ni lazima maumivu yatatokea. Ndio maana Rais anasema tuvumilie lakini ni lazima tupitie kipindi hiki kama kweli tupo serious tunataka kupona kama nchi.
 
How? wanaomba misaada kwetu? Wana nini wanachokikosa wakiachana na sisi? Jiulize wakisusia dhahabu kuna wa kuzinunua? Remember, Diamonds are forever!
Wakisusa itabaki na tutauza kipindi Dunia mambo yakibadilika ,lakini wanazihitaji ndio maana walikubaliana na mabadiliko yetu ya kisheria na kisera
 
Back
Top Bottom