Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
- #181
ha haaa, sasa kama umejivalisha birthday suit utatoka hivyo hivyo?Wee FP usinitoe machozi kwa kicheko, mwizi yupi utakayemsikia wa kukupa nafasi ya kukwapua hiyo wrap ili ujisitiri na kutoka mbio?
si lazima utajikwapulia kitu?.
nakumbuka wakati nasoma sekondari boarding kulikuwa na mlio wa kengele ya dharura, sijui bado ipo hii!
ikipigwa hiyo hata uwe wapi, lazima uwahi assembly ground.
wakati mwingine sasa ilikuwa inapigwa usiku wa manane, hapo sasa ndo tulikuwa tunajichekea kwa watu ambao wanalala na birthday suits......
sababu ni dharura na hujui ni nini mnaitiwa yaani ilikuwa ni kutoka mbio.....
umeme shule za serikali ilikuwa mwisho saa 4 baada ya prep wanazima jenereta zao, kwa hiyo usiku kucha full giza.
kwa wale ambao walikuwa hawalali na nguo walikuwa wanatoka na nguo anavaa huku anakimbia, anapofika chini anajikuta au alibeba sketi tupu au blauzi tupu, au sketi na suruali.......
tulikuwa tunacheka sana