Uchaguzi 2020 Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

Wanabodi,

"Watakao Rudi Bungeni ni 'Wakijani' "

Haya sii maneno yangu, na sio maneno ya kuambiwa ni maneno yaliyotamkwa na ambayo nimeyasikia mwenyewe kwa masikio yangu mwenyewe!.

Japo maneno haya ni maneno machungu kumeza, kwasababu Tanzania ni ya Watanzania wote na siyo ya 'wakijani' tuu, na katika uchaguzi uliopita, wasio wa kijani waliungwa mkono na Watanzania zaidi ya milioni 6, na kuna wabunge 145 wasio wa kijani, na kwa upande wa Zanzibar na Pembe kwa mujibu wa matokeo halali ya NEC, wasio wa kijani ndio wengi kuliko kura zote za kijani!, hivyo wote hawa ni Watanzania wenye haki sawa licha ya kutofautiana rangi!. Kauli hii ndio ukweli wenyewe wa uchaguzi wa 2020!, Watanzania woote katika Umoja wao, wamewakubali sana 'wakijani' na hili watalithibitisha tarehe 28 October, 2020. Mwenye masikio na asikie!.

Sisemi yamesemwa na nani na yamesemwa wapi, bali nawaomba tuu mniamini!.

Hongereni sana 'Wakijani'

Tulipokuwa tukiwaeleza humu kuhusu Watanzania tujifunze kuukubali ukweli hata uwe ni mchungu vipi kama ukweli huu
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
Mlinibeza!.

Niliposema kuhusu hoja ya wabunge wasio wa kijani, wakitaka kurejea Bungeni 2020 ni lazima wajitambue
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?
Pia mlinibeza humu.

Sasa leo Bunge limevunjwa rasmi, tegemeeni "the mass exodus" kwa wabunge wasio 'wakijani' watakao jitambua, they will do the needful, by jumping ships, kwa ving'ang'anizi na wenye misimamo, ambao watashikilia msimamo kwa kusimama na wanachokiamini, hawa ni mashujaa!, watakufa kizungu na tai shingoni na kama ni meli au jahazi, hata likumbwe na tufani kubwa kiasi gani, wao hawata jump ship na ku abandon, hawa watang'ang'ania meli yao, kwa kujishika kwenye milingoti, huku wakijiangalia na watazama na meli yao au jahazi lao na kufa kishujaa na watatamkwa ni mashujaa waliokufa kishujaa kuifia meli yao!. Hoja ya kati ya "waliojitambua" hai, waka abandon meli yao na ku jump ships hivyo kubaki hai na kusurvive na 'mashujaa' wafu, waliokubali kufa huku wanajiona kwa kuifia meli yao, nani ni muhimu zaidi?. This is debatable!.

Kwaheri ya kuonana hadi Novemba
2020... "ndani ya nyumba" panapo majaaliwa!.

Paskali
 
Hakutakuwa na chama kimoja, wapinzani watakuwepo ila sio hao vibaraka wa wakoloni mambo leo, waende huko wakatumike vizuri zaidi lakini sio kwa kodi zetu.

Hao vibaraka wanakera sana
Yan tangu Jana internet iko slow Sana, Yan sisi wafanyabiashara wa kutumia online tumeteseka Sana Tena sana

Yan Hawa vibaraka wa mabeberu warudi tu huko walikotoka

Wamefanya Mpaka maji yetu ya kunywa yamekuwa ni tope kabisa
 

Attachments

  • 2020-10-25 09.17.05.png
    2020-10-25 09.17.05.png
    575.2 KB · Views: 1
Nilishasema awali, una njaa wewe na unalazimisha uteuzi kwa kujipendekeza. Kazana maana ndiyo shortcut uliyonichagulia kujitafutia tonge!!
 
Swali langu ni dogo tu
Why tumetumia gharama nyingi kuendesha uchaguzi wakati kila kitu tayari kipo planed?

Ndio maana wazungu huwa wanatufananisha na masokwe

Hayo maela yote si bora yangeenda kulipa pession kwa wazee wetu?
Mkuu hp4510 , huu ndio ulikuwa ushauri wangu wa kwanza kabisa, angalia tarehe ya bandiko hili
P
 
Wakijani watarudishwa bungeni na NEC baada ya hapo ziraili mtoa roho ataanza kuwaondoa mmoja baada ya mwingine maana yake ni hii haki huinua taifa na mwenye haki ataishi

Hao Wakijani muda wao wa kirudi bungeni ulikoma baada ya kifo cha Mkapa kifuatacho sasa ni RIP KWA KIJANI WOTE WATAKAO RUDISHWA BUNGENI NA NEC

NB
MUNGU SIO MEKO
 
Naona huku Hai CCM wameamua wasipoteze kura, kumbe waliamshana nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na hawamuachi mpiga kura nyuma hata wagonjwa wenye kadi halali za kupiga kura (*152*00# -9 ikifuatiwa na namba kitambulisho chako) CCM inawetengezea jinsi gani ya kuwafikisha vituoni. Kuna mfumo wa aina yake wa kukusanya kura hapa Hai.

Mbona wemejipanga hivi? kuna nini kinakuja kutokea?
 
Wala Soo mchungu huo! JPM nA CCM ndio mpango mzima! Tunawasaidia hao waziba midomo wasije siku moja wakajisahau na kujiwekea super glue! Wake huku wasugue benchi kwanza! Sipati picha Kila Lema, Sugu, Mbowe na henge lake watakavyoishi! Chezea JPM ww! Waaaacha maneno, Kwisha habari yao! JPM ndio mpango mzima, imeishia hiyo!
 
Kada mwenzangu hapa kidogo haileti maana kwani sio. Hili lifikirie vizuri kumbuka bila upinzani tutalala sana na mwisho hatutakuwa hatuna hoja kumbuka tangu 1977 tupo madarakani na kama tupo tuangalie na nyakati na upepo unavumaje kwetu ndani ya chama na nje ya chama.
 
Back
Top Bottom