GE2025 Japheti Hasunga aahidi kutafuta timu ya ligi kuu Songwe

GE2025 Japheti Hasunga aahidi kutafuta timu ya ligi kuu Songwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,131
AHADI imetolewa kwamba wagombea ubunge na udiwani wa CCM wakichaguliwa kwenye uchaguzi mkuu watahakikisha Mkoa wa Songwe unapata timu inayoweza kushindana kwenye ligi kuu.

Mgombea wa ubunge katika Jimbo la Vwawa kupitia CCM, Japheti Hasunga ametoa ahadi hiyo jana alipoomba kura kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo.

Amesema malengo yake pamoja na mgombea wa ubunge Jimbo la Mbozi Onesmo Mnkondya ni kuhakikisha mkoa unakuwa na timu imara inayoundwa na vijana wa mkoa huu ili wapate ajira.

Wakati huohuo Timu ya Azam Fc jana imeharibu pilau la timu ya Mbeya City kwa kuitandika mabao 2-0 katika mchezo wa sherehe za Mbeya City kutambulisha wachezaji.
Mabao hayo yamefungwa katika vipindi vyote viwili ambapo moja limefungwa kipindi cha kwanza na la pili limefungwa kipindi cha pili.
1757232824865.png
 
Back
Top Bottom