JaffarMohammed
JF-Expert Member
- Nov 13, 2016
- 762
- 283
Lakini kiuhalisia na kiukweli jumatatu ni siku ya tatu ya wiki. Na jumamosi ndio siku ya kwanza.Nisome uelewe kutokana na mazoea na utaratibu uliopewa nguvu kisheria ambao ndio unafanya kazi
Lakini kiuhalisia na kiukweli jumatatu ni siku ya tatu ya wiki. Na jumamosi ndio siku ya kwanza.Nisome uelewe kutokana na mazoea na utaratibu uliopewa nguvu kisheria ambao ndio unafanya kazi
Kumbe kuna Mungu wa kike!!Mwezi mei au mai unatokana na mungu wa kike wa kirumi aitwae maia. Maia alikuwa anatambulika kama mungu wa ukuzi ( growth) , maia alikuwa mama wa Hermes na pia ni binti wa atlas.
Kiebrania mwezi wa wa tano ni Av ambao unachukua baadhi ya tarehe katika kalenda ya kirumi mwezi wa saba na wanane.
TwangojaNitarudi baadaye , nikitulia nitaleta somo. Mungu akinipa kibali.
Mungu awalinde
sitaweza kuendelea tena maana kuna mtu ana mtizamo hovyo ashaanza nitukana. Principal yangu mwaka huu sitajibu upuuzi, atakaye niletea upuuzi namuweka kwenye ignore list .Naomba uendelee kuichambua hiyo miezi yote tuliorithi toka huko upaganini, utupe na athari zake (za kuitumia kalenda hiyo)
Sio Mungu wa kike! Ni mungu wa kike. Kuna tofauti kubwa sana mtu aandikapo "mungu" na "Mungu"Kumbe kuna Mungu wa kike!!
AfuaanSikuweka kwa nia hiyo bali kama kiwakilishi cha msingi imara kwenye mipango na matarajio yetu
Lengo la kalenda ni kutambua nyakati ili kuweza kupanga mipango, kuweka na kupima malengo. Huo ndio mwisho, nyingine zote mbwembwe.Kwanza kabisa ijulikane kwa uwazi kwamba majina ya miezi ya kigregoria imeanzishwa kwa mfumo wa kumbukumbu za miungu ya kirumi badala ya Mungu wa kweli.
Kama alivyosema mshana jr kwa imani ya kirumi mwenzi wa kwanza ni lango, hii inatoka na maana na asili ya neno january (Janus ) ambae alikuwa ni mungu wa lango.
Picha ya mungu Janus.
![]()
Kuamini na kendelea kutumia sikukuu na mapokeo ya kale yenye asili ya miungu, kwamimi naamini sio sahihi, lakini mambo mengi tumekuwa tukiyafuata kwaajili ya mfumo wa maisha bila kujua asili yake ni nini.
Kiebrania mwezi wa kwanza ulikuwa unaitwa mwezi wa Nisan amabao kwenye kalenda hii ya kirumi inachukua baadhi ya tarehe ndani ya mwezi wa tatu na wanne.
Mara nyingi tunapoingia mwaka mpya, wachungaji na viongozi wa dini ( haswa imani za kikristo) wamekuwa wakitoa kama unabii kuwa mwaka huu ni mwaka ya jambo fulani kwa mfano mwaka huu ni mwaka wa kupokea, au mwaka huu ni mwaka wa maongezeko, au mwaka huu ni mwaka wa shange, kicheko n.k. . Swali je Mungu anatengwa na vipimo vyetu vya miaka? je mwaka jana ni tofauti kwa Mungu. Ninavyo amini mimi kalenda ni mipango ya binadamu ili kuweza kujipima katika malengo.
Nitaendelea zaidi baada ya kuona michango ya watu.
Sio Mungu wa kike! Ni mungu wa kike. Kuna tofauti kubwa sana mtu aandikapo "mungu" na "Mungu"
Avachee!!View attachment 459432
Kwa hesabu zetu huu ni mwanzo wa mwaka Kwa mujibu wa kalenda tunayoitumia, zipo kalenda nyingi lakini hii ndio iliyomakinika na kuwa na nguvu hivyo yote yatakayofanyika na kutokea Kwa mwaka huu yataathiriwa sana na kalenda hii.
January ni mwezi wa kwanza kabisa katika mwaka wenye miezi 12, ni kama ilivyo tarehe moja kwenye mwezi wenye siku 28 ama Jumatatu kwenye juma lenye siku saba.
January ni lango kama ilivyo kwa mtoto wa kwanza na ni shamba jipya linalopaswa kupandwa mbegu bora kwa ajili ya kupata mazao bora
December yako ambayo ndio mwisho wa mwaka itategemea umeanzaje January yako.
Kidunia utaweka mipango na matarajio sahihi ukiweka nadhiri na kunuia kufanya mambo kadha ambayo yatatiwa nguvu kiimani na sadaka yako...jipange kukataa mabaya yote nia kupata yale unayotamani kupata kwa njia sahihi na mipango thabiti.
Kumbuka lango huingiza chochote kama halina kizuizi wakati unaweka nadhiri zako kupitia dua maombi na sadaka kuna upande wa giza nao unapanga yake.
Wakati Mungu akikupangia hili na lile (kwa wale waamini)shetani naye anapanga yake...kila penye chanya hapakosi hasi.
Hapa inategemea unasimamia wapi nguvu yako iko upande gani , unaweza kuwa ni mshika dini mzuri lakini matendo yako yakawa hasi yasiyo na misingi yoyote ya kile unachokiamini..unaweza ukawa ni unajua unachokitaka lakini ukawa huna mwongozo sahihi wa kukipata.
Jitafakari na utengeneze lango lako sasa chukua muda wa kutosha kutafakari ulikotoka makosa uliyofanya ulipo na uendako.
January yako ifanye kuwa lango sahihi kwa kuzuia nguvu hasi zote zinazokuandama zikatae kwa kunia kwa kinywa chako mwenyewe ili utengeneze mbegu ya roho itakayokupa matokeo mema.
View attachment 459433.....!
Nakuombea...!
NB: Mada hii ni kwa msaada mkubwa wa dada Devine