Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,836
- 730,300
Kwa hesabu zetu huu ni mwanzo wa mwaka Kwa mujibu wa kalenda tunayoitumia, zipo kalenda nyingi lakini hii ndio iliyomakinika na kuwa na nguvu hivyo yote yatakayofanyika na kutokea Kwa mwaka huu yataathiriwa sana na kalenda hii.
January ni mwezi wa kwanza kabisa katika mwaka wenye miezi 12, ni kama ilivyo tarehe moja kwenye mwezi wenye siku 28 ama Jumatatu kwenye juma lenye siku saba.
January ni lango kama ilivyo kwa mtoto wa kwanza na ni shamba jipya linalopaswa kupandwa mbegu bora kwa ajili ya kupata mazao bora
December yako ambayo ndio mwisho wa mwaka itategemea umeanzaje January yako.
Kidunia utaweka mipango na matarajio sahihi ukiweka nadhiri na kunuia kufanya mambo kadha ambayo yatatiwa nguvu kiimani na sadaka yako. Jipange kukataa mabaya yote nia kupata yale unayotamani kupata kwa njia sahihi na mipango thabiti.
Kumbuka lango huingiza chochote kama halina kizuizi wakati unaweka nadhiri zako kupitia dua maombi na sadaka kuna upande wa giza nao unapanga yake.
Wakati Mungu akikupangia hili na lile (kwa wale waamini)shetani naye anapanga yake. Kila penye chanya hapakosi hasi.
Hapa inategemea unasimamia wapi nguvu yako iko upande gani , unaweza kuwa ni mshika dini mzuri lakini matendo yako yakawa hasi yasiyo na misingi yoyote ya kile unachokiamini unaweza ukawa ni unajua unachokitaka lakini ukawa huna mwongozo sahihi wa kukipata.
Jitafakari na utengeneze lango lako sasa chukua muda wa kutosha kutafakari ulikotoka makosa uliyofanya ulipo na uendako.
January yako ifanye kuwa lango sahihi kwa kuzuia nguvu hasi zote zinazokuandama zikatae kwa kunia kwa kinywa chako mwenyewe ili utengeneze mbegu ya roho itakayokupa matokeo mema.
Nakuombea...!
NB: Mada hii ni kwa msaada mkubwa wa dada Divine...