January ni lango; panda mbegu yako sasa!

January ni lango; panda mbegu yako sasa!

Katika mwaka kuna kufunga mwaka na kufungua mwaka.

Mwanzo wa wa kitu ndipo ambapo tuna uwezo wa kuweka kitu kiwe ni kibaya au kizuri

Waswahili wanasema siku nzuri huonekana asubuhi

## mwezi wa kwanza ni kipindi cha kupanda kitu chema ambacho kitakua na wewe mwaka mzima.

Mwezi wa1 ni lango pia. Au mwez wa 1 unaweza pitisha vitu unavyo vitaka.

Na siku, mwaka huwa zina masikio
Kwanini nasema vinauwezo wa kukusikia..

Kama nchi( ardhi) inaweza kukusikia kwanini siku zisikie?

Hii wiki nilikuwa nasoma Neno, hii sehemu nilikuwa nasoma

Hesabu 20:8
Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake...


Mungu aliwaambia Musa na Harun wauambie mwamba utoe maji.

## kumbe hata mwamba unasikia

Tuje katika topic.
Mungu aliwaambia wana wa Israel wazaliwa wa 1 wa wanyama na watu ni wangu
: Mfano Tukija ktk Biblia
Mungu anasema kile cha1 ni cha kwake.
Wazaliwa wa1 ( wafunguao tumbo ni wake)
Ina maana mwez wa1 ni wake
Anapotaka kuwahi kitu cha 1 ili aweze kulinda na wale wazaliwa wanao fuata
Ukiwahi mwez wa1 ukimpa Mungu ina maana miez yote yeye atakuwa hapo


15 Kila kifunguacho tumbo, cha wenye mwili wote watakachomsongezea BWANA cha wanadamu na cha wanyama, ni chako; lakini mzaliwa wa kwanza wa binadamu, huna budi utamkomboa, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi utamkomboa.

16 Na hao watakaokombolewa katika wanyama hao, tangu aliyepata umri wa mwezi mmoja utamkomboa, kama utakavyohesabu kima chake, kwa fedha ya shekeli tano, kwa shekeli ya mahali patakatifu (nayo ni gera ishirini).

17 Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, iwe harufu ya kupendeza.
Hesabu 18


Hapo juu Mungu anataka cha1, ukipanda cha1 kwa Mungu vyote vinavyo fuata atavilinda sababu kuna nguvu ya kitu cha 1( mwezi)


: 22 Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
23 Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.
Kutoka 12

Tuje hapo chini

: Uambie mwezi wa 1 wewe ni lango na 2017 ni mzaliwa1 na mwaka mpya napaka damu ya pasaka( damu ya Yesu) katika miimo na vizingiti vya malango wala mambo mabaya hayatapita hapa

Utapitisha mema tu na sio mabaya
: Panda kwa imani.


: Unaweza tumia sadaka kuiambia sadaka napanda mbegu ya mwaka huu nataka hichi na hichi na hichi na sitak kuona hichi na hichi
Vyoote unavyo vitaka nena mwaka 2017 sikia neno la Bwana na ww mwez wa kwanza sikia neno la Bwana na ww mbingu na ardhi mnakuwa mashaid napanda mbegu hii kupitia sadaka yangu hii
Mfano nitafanikiwa huu mwaka
Sitoumwa
Sitozika vifo vinavyo tokana na wachaw uganga au shirikina labda kifo kinacho tokana na mapenzi ya Mungu
Au nitajenga, nitakuwa na kibal cha Bwana niingiapo na nitokapo

Na popote pale nyayo zangu zitakapo kanyaga nitamiliki( yoshua1:3,6)

Na hakuna mtu atakaye simama mbele yangu siku zote za maisha yangu)

Hapo ina maana hakuna atakaweza kuzuia njia zako au mafanikio yako nk

: Sitopoteza bal nitapata tu.
Mim na familia yangu ni watu wa afya tu
: Na taja vitu vyote vibaya uambie mwaka 2017 na ww mwez wa1 sikia
Sitaki hich na hichi.


: Mwez wa1 ni lango kama vile mtoto wa1 ni lango


: Na ktk lango kuna vita
: Shetan anapanda vyake na Mungu pia anapanda

: Sasa inategemea
: Unasimama upande upi

: Unapo tamka neno kuna roho inafuatilia ndani yake yaan roho kamil itahikikisha kile kitu kitokee

[: Ukiangalia kutoka 12: 20 na kuendelea


: Utaona kabisa Mungu baada ya kuvuka yale majaribu wana wa Israel walianza mwez wa 1 mwaka 1 ktk maisha yao
: Kama mwez wa1 ni lango linaweza pitisha chochote kile

: Nani alinde ule mlango?
Achilia damu ya pasaka ktk miimo na vizingiti vya malango ili mwovu asipitishe vya kwake

: Hata wachaw wanafanya hivyo hivyo wana miez maalum ya kuweka vya kwao
: Na wanatamka
: Na ww tamka usinenee ndani ya moyo

: Kuna nguvu ya kinywa ukisema yanatokea

Mbingu na nchi zikawe shahidi

Iambie

Mbingu na nchi mkawe mashahidi wa haya niliyo tamka na mkaweke kumbukumbu ndani yake

Kumb 30:19a
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo......

Mbingu na nchi zaweza kuwa mashahid wako zinasikia

## kumbukw toba kabla hujaanza maombi hayo

Shika sadaka utajua pa kupeleka madhabahu ipi

Kama yatima kama kanisani

Lakin hakikisha unaiweka ktk madhabahu sahihi

## watu mtauliza na sadaka tena?

Sadaka ina nguvu na inaongea

Upande wa nguv za giza huwa hawafanyi vitu vyao bila sadaka

Tutoe sadaka kwa Mungu aliye hai.

Mungu awabariki
Msisahau kuyasemesha malango y mwezi wa 1, nimerud kusoma tena, happy New Year Jamii forum member
 
January ni Asubuhi yako. Semesha asubuhi yako ikae upande wa Mungu, isimame kinyume na adui.
January uwe tasa upande wa adui, uzalishe cha Mungu.

January Pigana vita upande wake wangu, simama kinyume cha adui.

Nitabarikiwa mjini , mashambani

Nitamiliki malango ya maadui zangu

Mimi ni uzao wa Ibrahim, mtu wa milki ya Mungu, masikani yake Mungu. Taifa takatifu la Mungu.

Nitajenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake

Nitakuwa na afya na sio magonjwa,
2026 umebaikiwa kwaajili yangu.

Kila neno Ambalo si la Bwana halitafanikiwa wala halitakuwa,

Shauri la Bwana ndio litasimama.

Omba kwa Neno la Mungu, sabb ana angalia neno lake apate kulitimiza

Huo ni mfano tu una 29 days za kupanda
 
Back
Top Bottom