January ni lango; panda mbegu yako sasa!

January ni lango; panda mbegu yako sasa!

hongera mshana kwa ufafanuzi wa masuala haya kwa jamii ,uwepo wa jamii forum tunapata elimu ambayo ingetulazimu kupeleka kuku na mkojo wake ili kupata habari hizi murua .tushukuru pamoja ,kuhusu mtoto wa kwanza ndg Mshanajr
naomba ufafanuzi hapo pia ni lango limekaaje na nini kinatakiwa kufanyika kwa mtoto huyo wa kwanza wa family ,na je endapo si mtoto wa ndoa na ni wa kwanza na ukaoa mke mwingine ukajaaliwa kupata watoto huyu naye ni wa kwanza ?au wa pili .
 
nadhani makala imewasilisha kwamba january ndio msingi wa kujipanga kufikia december...uimara wa december na kuhumaliza mwaka ktk kufikia malengo...unabebwa na january ambayo umejiandaa kwa namna gani..??...nimekusoma mkuu....
 
hongera mshana kwa ufafanuzi wa masuala haya kwa jamii ,uwepo wa jamii forum tunapata elimu ambayo ingetulazimu kupeleka kuku na mkojo wake ili kupata habari hizi murua .tushukuru pamoja ,kuhusu mtoto wa kwanza ndg Mshanajr
naomba ufafanuzi hapo pia ni lango limekaaje na nini kinatakiwa kufanyika kwa mtoto huyo wa kwanza wa family ,na je endapo si mtoto wa ndoa na ni wa kwanza na ukaoa mke mwingine ukajaaliwa kupata watoto huyu naye ni wa kwanza ?au wa pili .
Asante sana kuhusu la mzaliwa wa kwanza kama lango naomba tuwe na subra aje Heaven Sent na Divine...
 
View attachment 459432
Kwa hesabu zetu huu ni mwanzo wa mwaka Kwa mujibu wa kalenda tunayoitumia, zipo kalenda nyingi lakini hii ndio iliyomakinika na kuwa na nguvu hivyo yote yatakayofanyika na kutokea Kwa mwaka huu yataathiriwa sana na kalenda hii.

January ni mwezi wa kwanza kabisa katika mwaka wenye miezi 12, ni kama ilivyo tarehe moja kwenye mwezi wenye siku 28 ama Jumatatu kwenye juma lenye siku saba.

January ni lango kama ilivyo kwa mtoto wa kwanza na ni shamba jipya linalopaswa kupandwa mbegu bora kwa ajili ya kupata mazao bora
December yako ambayo ndio mwisho wa mwaka itategemea umeanzaje January yako.

Kidunia utaweka mipango na matarajio sahihi ukiweka nadhiri na kunuia kufanya mambo kadha ambayo yatatiwa nguvu kiimani na sadaka yako...jipange kukataa mabaya yote nia kupata yale unayotamani kupata kwa njia sahihi na mipango thabiti.

Kumbuka lango huingiza chochote kama halina kizuizi wakati unaweka nadhiri zako kupitia dua maombi na sadaka kuna upande wa giza nao unapanga yake.

Wakati Mungu akikupangia hili na lile (kwa wale waamini)shetani naye anapanga yake...kila penye chanya hapakosi hasi.

Hapa inategemea unasimamia wapi nguvu yako iko upande gani , unaweza kuwa ni mshika dini mzuri lakini matendo yako yakawa hasi yasiyo na misingi yoyote ya kile unachokiamini..unaweza ukawa ni unajua unachokitaka lakini ukawa huna mwongozo sahihi wa kukipata.

Jitafakari na utengeneze lango lako sasa chukua muda wa kutosha kutafakari ulikotoka makosa uliyofanya ulipo na uendako.

January yako ifanye kuwa lango sahihi kwa kuzuia nguvu hasi zote zinazokuandama zikatae kwa kunia kwa kinywa chako mwenyewe ili utengeneze mbegu ya roho itakayokupa matokeo mema.
View attachment 459433.....!

Nakuombea...!

NB: Mada hii ni kwa msaada mkubwa wa dada Devine
Amina
 
DKT hupo? Shukrani sana Mkuu kwa kutukumbusha kufanya wajibu wetu hasa kumtolea Mungu Sadaka na kunuia Unataka Akufanyie Nini Katika Mwaka Huu.

Nikweli kabisa kwamba Yatupasa tuwe watu wa Malengo.

Wengi hawafanikiwi kwa sababu ya kutokuwa na Malengo pamoja na kutumia Muda vibaya.

Mimi ni Mfanyabiashara. Ili nifanikiwe yanipasa niwe Mtu wa Malengo pamoja na kutumia Muda vizuri.

Kumshirikisha Mungu Katika Mipango yako, na Kupanda Mbegu yaani Kumtoa Sadaka Yenye Lengo la Kusimama kama Mbegu yako juu ya Malengo Uliyonayo kwa Mwaka Mzima.

Watu wengi wa Mungu wanafanya vibaya katika eneo la Uchumi kutokana na Kutokujua Siri ya Kumtolea Mungu Sadaka Nyingi.

Wenzetu wa Upande wa Pili wanamtolea mungu wao sadaka nyingi sana na kupata mafanikio kwa haraka tukokana na kumweshimu mungu wao.

Ila Wacha Mungu wengi Utumia sana dua na Maombi na kusahau swala la kuambatanisha Dua zao na Maombi yao na Sadaka zakuridhisha.

Utakuta mtu Anamwomba Mungu Mwaka huu Amfanikishe Kujenga Nyumba ya Ml 100. Alafu anaweka kwenye Bahasha shilingi mia tano!

Embu tubadilike jamani Tuanzekuchukua hatua mwaka huu 2017 lazima tutie bidii kwenye kumtafuta Mungu kwa ukamilifu na kumtolea sadaka nzuri na zakuridhisha.

Mbona kwenye maharusi,misiba,masherehe tunatoa pesa nyingi lakini tukija kwa Mungu tunatoa 500?

Hivi kweli Mungu Atambarika mtu ambae anamdharau?

Tuwe na Malengo na tuutumie muda vizuri, Muda ni Pesa, pesa ni Muda.

Nakushukuru Dkt Mshana Jr.
 
*HAYA TENA KWA MARA NYINGINE TENA BAHATI HAIJI MARA MBILI* *JE, WAJUA BANDO NA SIMU YAKO NI MTAJI TOSHA?*Kama huna ajira na unataka kuongeza kipato chako *Furusa hiyo fungua link hii http://jamiiforums.com/?refcode=102945
ujipatie pesa haraka sana kuliko kupoteza bando bila faida yoyote jaribu sasa uwaambie na members wengine watumie furusa hii*
 
*HAYA TENA KWA MARA NYINGINE TENA BAHATI HAIJI MARA MBILI* *JE, WAJUA BANDO NA SIMU YAKO NI MTAJI TOSHA?*Kama huna ajira na unataka kuongeza kipato chako *Furusa hiyo fungua link hii http://**********/?refcode=102945
ujipatie pesa haraka sana kuliko kupoteza bando bila faida yoyote jaribu sasa uwaambie na members wengine watumie furusa hii*
peleka jukwaa la biashara.
 
Asante sana kwa kukumbushana ngoja tuzidi kupambana kwa uwezo wa Mungu
 
Back
Top Bottom