January Makamba: Rushwa imetembea uchaguzi wa EALA!

Kama viongozi wa takukuru nao wanakula wacha wale tu,kiama chao 2015...bhaji nasikia leo kachoka sana mpaka sasa ajaamka kwa rushwa aliotoa ya aina ya mmmh....
 
Wabunge wahojiwe na PCCB kama kweli hii taasisi inatenda haki na inasimamia vita dhidi ya rushwa. Maan wabunge wenyewe wamekiri tena wameweka bayana kuwa wamehongwa. Hii ni aibu kwa taifa zima iwapo tunapata taarifa kisha tunanyamaza.
 
Kwa maneno hayo TAKUKURU ifutwe bajeti wanayopewa itumike kusafisha miji yetu.

Umesema ukweli wote; kama polisi walishindwa eti dawa ikawa kuunda kikosi cha polisi wasiona sare na kubadili jina AIBU, hawawezi ifutwe tu. Sakata la RADA JE, hawa kweli tunawahitaji au tatizo ni vipaumbele vyetu?
 
sasa kama wamekiri takukuru hawatakuwa na kazi kubwa wawakamate na wawatie ndani haraka.
au takukuru haihusiki na rushwa za siasa?
nalishawahi tembelea bunge mtumishi wa bunge akasema wabunge wakiwa ndani ya bunge polisi hawaruhusiwi kumkamata wala kumuhoji mbunge amsubiri akitoka nje ya geti la bunge maana bunge ni mahala tukufu na ndio mahala pekee wabunge wapo salama.
kwa kauli hii takukuru wawasubiri nje wawakamate wote waliokiri na wasio kiri watatajwa na waliokiri taratibu uone kazi kama hujakuta nusu ya wabunge kizimbani.
lakini masikini takukuru haina menoooooooooooooooooooooooooooooooo.ovyooooooooooooooo
kwanza haka kataasisi wakavunje fedha walizokuwa wanalipwa wakawalipe wakulima wa korosho huko mtwara.
 
Mimi naona baadhi ya vijana wa CCM wana akili timamu japokuwa wanakuwepo pia wenye kusifu hata mtu aliyeuchi kuwa kavaa vizuri na hali ukweli wanaujua
 
Mbunge anasema hivyo hadharani halafu kimyaa, kama katoa salamu tu vile. yaani kutoa rushwa hapa tz ni kama kunywa bia moja..
 
Kuna wengine wanasema chochote ili wawe maarufu zaidi.

Kama ana uchungu angewataja,just another opportunist.
 
hiyo inatupa pcha kwamba hatahuko kwenye kamati anapokea. basi aje hapa jamvini atueleze hayo

Huyu asituzingue kwani yeye mwenyewe pale alipo anapokea na anatoa kama baba yake Yuisuf; kwani zile shs bilioni moja [ U.S $ I millon] alizoletewa na shemejie ili apate ubunge Lushoto alimgawia nani? Na sio kweli kuwa wabunge wote walihonga ni hao wa ccm tu!! Dr. Kessy hakuhonga hata senti moja!!!!
 
nasubiri jibu teh teh teheeee...:)
ahh na kingereza chake cha marekan TANDALE jana wakat anaomba kura dah...bdada anajua sana kuutumia UCHUMI WAKE wala haukaliiiii mwaya akhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ye anapaa tu kwa raha zake:car:
Lakini kibarua kilimpata, wote hao!
 
Ukweli halisi: Rushwa imetembea sana kwenye uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Wabunge wa vyama VYOTE tunahusika. Aibu kwa taifa zima!

Maneno yake hayo on twitter

Kama wao wanatoa kuhonga wapiga kura wao watashindwaje kuhongwa?
 
Kuna Baadhi ya Wabunge wamedai kuwepo kwa rushwa kwenye uchaguzi wa EALA!! Hivi TAKUKURU hawawezi kuchunguza kwa kuwahoji wabunge waliosema hadharani kama mashahidi??
 
Mimi hata sishangai wabunge kuhongwa kwakuwa nao ni mazao ya rushwa. Kilichonistua ni kura kuharibika mjengoni, nikakumbuka kuwa kuna viti maalum, nikatulia.
 
Umesema ukweli wote; kama polisi walishindwa eti dawa ikawa kuunda kikosi cha polisi wasiona sare na kubadili jina AIBU, hawawezi ifutwe tu. Sakata la RADA JE, hawa kweli tunawahitaji au tatizo ni vipaumbele vyetu?
Hapana, msiwalaumu hawa watu. Rushwa kubwa zinagusa watu wakubwa pia. Ndio maana utasikia wanachunguza rada, kagoda, meremeta, kiwira, na nyingine nyingi kubwa. Halafu ngoma ikifika kwa DPP (a point of exit iliyowekwa makusudi) hatoi kibali. Kwa mujibu wa Katiba Hakuna chombo chenye ruhusa ya kuhoji maamuzi ya DPP. Tuna matatizo mengi nchi hii.
 
Kwanini kwenye Twitter, na isiwe TBC 1, huyu jamaa na yeye anapenda umaarufu rejareja, akiandika kwenye twitter babu zangu wa kule Ikungulyambeshi wanaijua hiyo twitter??
Usimpangie mtu.... Mbona ww hupeleji magazetini
 
Rushwa rushwa rushwa hivi PCCB wanafanya kazi gani? Au hawaruhusiwi kuingia bungeni?nisaidieni jamani.
 
Ukweli halisi: Rushwa imetembea sana kwenye uchaguzi wa Wabunge wa EALA. Wabunge wa vyama VYOTE tunahusika. Aibu kwa taifa zima!

Maneno yake hayo on
twitter

Sasa Kama Mbunge January kakiri mbona takukuru hawajatekeleza majukumu Yao?Au kazi Yao ni kutafuna kodi zetu sisi wananchi kwa kuendesha taasisi hii ya TAKUKURU isiyowajibika au mnatupumbaza sisi wananchi uwepo Wa taasisi hii iwe kigezo cha sie wananchi kuona Serikali inawajibika?Jamani nyekundu ibaki kuwa nyekundu,hebu TAKUKURU fanyeni kazi yenu
 
Back
Top Bottom