Kiturilo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 709
- 2,858
Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu waziri mpya wa nishati bwana January Makamba ateuliwe na rais Samia Suluhu kushika nafasi hiyo.
Waziri Makamba tangu ateuliwe amefanya ziara Kigoma tu tena mjini mjini baada ya kupewa maagizo na makamu wa rais afike huko kutatua kero ya kukatika katika umeme.
Baada ya hapo tunamuona waziri Makamba akiwa anajipositi akifanya vikao na wazungu kwenye hoteli kubwa kubwa mara tunasikia anafanya ziara Saudi Arabia kuonana na waziri wa nishati wa nchi hiyo!
Hoja yangu ya kwanza ni kwamba kwenye miradi ya REA vimebaki vijiji elfu 2 tu kuunganishiwa umeme, je kwa hali hii ya waziri kuonekana kwenye mahoteli ya kifahari tu vijiji hivi 2000 vitaisha kupelekewa umeme hadi kufikia mwaka 2025 kama ilani ya uchaguzi inavyotaka?
Hoja yangu ya pili ni kwamba maeneo yanayokatika katika umeme siyo Kigoma tu ulipoelekezwa na mh Makamu wa rais ukafanya ziara, tatizo hili ni kila mahali nchini umeme unakatika kwa sasa je ni lini utaanza kufanya ziara vijijini kuunganisha umeme na kuangalia matumizi ya kodi za watanzania kama zinatumika kwa usahihi?
Ina maana mtu wa kubaini ubadilifu aliyebaki ni waziri mkuu pekee bwana Kassim Majaliwa?