January Makamba: CCM imeshashinda majimbo 176 mpaka sasa

January Makamba: CCM imeshashinda majimbo 176 mpaka sasa

KIUKWELI Haya majimbo tumepoteza imeniuma sana

Wabunge wapya fanyeni kazi
 
Mimi sielewi ina maana tume mpaka sasa bado tu hawajamkamata makamba kwa kufanya kazi ya tume ya kutangaza matokeo ya uchaguzi ya ubunge.....aisee asipokamatwa basi nchi hiii kitanuka

Majimbo ambayo bado UKAWA inapeta
1. Whatsapp
CDM 87%
CCM 9%
2. Nyomi
CDM 92%
CCM 00%
3 FASIBUKU
CDM 98%
CCM 1%
 
January Makamba anajua madhara ya kutangulia mbele ya tume? Kikitokea cha kutokea atasema

Makamba ni ushuzi wa kuotea mbali...huyu mjinga cku ya kupiga kura tu alitangaza tarehe ya kumtangaza Magufuli kama mshindi afu leo anamshangaa Maalim Seif!!
 
Majimbo ambayo bado UKAWA inapeta
1. Whatsapp
CDM 87%
CCM 9%
2. Nyomi
CDM 92%
CCM 00%
3 FASIBUKU
CDM 98%
CCM 1%

Hii ni kali. Makamba alidai majimbo 167 kati ya 264 CCM imeshinda, hadi sasa CCM ina majimbo 114 yaliyothitishwa na NEC, bado majimbo 53 tu, yanayosalia yamechukuliwa na UKAWA na WENGINEO.
 
It wouldn't have mattered if Slaa had been their candidate.

CCM would have won anyway.

The opposition will never win a single general election under the current setup.

He lost in 2010 and he would have lost this one as well.

Well said Mkuu Ngabu. Slaa shouldn't have made any changes. Tubadili mfumo tuwe na tume huru. Period.
 
Siamini kama kuna waliotarajia kuwa EL anaweza kufurukuta mbele ya Magufuli.
 
Makamba ni ushuzi wa kuotea mbali...huyu mjinga cku ya kupiga kura tu alitangaza tarehe ya kumtangaza Magufuli kama mshindi afu leo anamshangaa Maalim Seif!!

Huyo ni Mwizi tuu, tokea anasoma mpaka sasa. Oneni hii kitu.
 

Attachments

  • 1445954409908.jpg
    1445954409908.jpg
    54.6 KB · Views: 74
Masikini Mzee Edo alilalamika kuwa tume inapendelea, sasa sijui haoni kuwa TV nazo zinatangaza hayohayo.

Press conf ijayo ataomba tume wakitangaza matokeo wasitangaze ya Magufuli ili aonekane anawashinda kina Chief Lutayosa, Dovutwa.......
 
Kumbe Kuratitbu Matokeo Kwa KUKUSANYA Na Kuyajumlisha!! Kwa CCM Sio Tatizo, Ila Kwa UKAWA Ndio Tatizo!!!!?? Maana Bila Ya Kufanya Hivyo, Hizo Takwimu Utazipataje!!!!!??? Haya Bhana Makamba, Ninyi Mmeshika Mpini Wa Kisu!!!!!
 
Akiongea na waandishi wa habari muda huu January Makamba amesema kwa mujibu wa taarifa rasmi za mabandiko ya Tume ya uchaguzi katika vituo vya matokeo, ni kuwa CCM mpaka sasa imeshinda majimbo 176 kati ya majimbo 264 na imekomboa majimbo 12 kutoka upinzani.

Aidha amesema Maalim seif Hamad kutangaza matokeo ya ushindi wa ZNZ ni mzaha

=============================


Kwa kauli hii ni wazi kua na Uchaguzi wa Tanzania Bara nao unafaa kufutwa.
Hapa pia sababu hizi hapa chini pia zinafanya uchaguzi huu ufutwe nao

MATOKEO YA NEC YANA KASORO NYINGI.!

Jana nilisema nitatoa screnario tano kudhibitisha kuwa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume si ya kweli na yanafaa kupuuzwa na kila mtu mwenye akili timamu. Licha ya Tume ya uchaguzi kutokua huru lakini imeamua kushirikiana na CCM kupuuza maoni ya watanzania na kuhujumu matokeo ya uchaguzi.

Scenario zifuatazo zinathibitisha hivyo;

1. Jimbo la Tunduma karatasi iliyobandikwa ktk ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi ikiwa na muhuri wa Tume inaonesha Lowassa amepata kura 32,219. Lakini matokeo yaliyotangazwa na Tume yanaonesha Lowassa amepata kura 6,000 tu. This means NEC hawatangazi matokeo wanayopokea kutoka kwny majimbo bali wanatangaza matokeo yao kama wanavyoelekezwa na CCM.

2. Jimbo la Bumbuli matokeo ya Ubunge yanaonesha kuwa waliopiga kura ni watu 20,512 ambapo January Makamba amepata kura 17,805. Lakini cha ajabu kwenye matokeo ya Urais jimbo hilohilo la Bumbuli waliopiga kura ni watu 44,011 ambapo Magufuli anadaiwa kupata kura 35,801.

Sasa jiulize imekuaje waliopiga kura za mbunge wawe watu 20,512 halafu kura za Rais wawe 44,011. Yani kuna watu 24,000 walienda vituoni kupiga kura za Rais tu lakini hawakupiga za Mbunge. Haya ni maajabu ya dunia. Haihitaji degree kujua kwamba Tume imeongeza wapiga kura hewa 24,000 na kura zote hizo wakampa Magufuli.

Niliwahi kusema "CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu". Kiazi kama January ndo anapewa kazi ya kuiba kura za Lowassa unategemea nini? Haiwezekani watu 24,000 waende kituoni kumpigia kura Rais tu halafu wasipige za Mbunge. Utaratibu ulikua watu kupiga kura 3. Sasa iweje waliopiga kura za Urais Bumbuli wawe wengi kuliko waliopiga za Mbunge? Yani mtu alienda kituoni akapewa karatasi ya Rais tu, alipopiga akaondoka bila kupiga ya Mbunge?.

3. Majimbo mengi asilimia za kura zimeonekana kuzidi 100 jambo ambalo linadhihirisha wizi wa waziwazi. Jimbo la Monduli Arusha Lowassa anatajwa kupata kura 49,675 na Magufuli kura 11,335 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (18%).

Jimbo la Arusha Mjini Lowassa anatajwa kupata kura 150,107 na Mgombea wa Chauma amepata kura 551 lakini wote wametajwa kuwa na asilimia zinazolingana (69%). Yani Lowassa amelingana na Hashim Rungwe jimbo la Arusha mjini.

Jimbo la Ndanda ukijumlisha asilimia za wagombea zinakuja 108%. Jimbo la Arusha mjini zinakuja asilimia 182% na majimbo mengine hivyo hivyo. This means waliopewa kazi ya kuiba kura walikosa umakini. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

4. Baadhi ya majimbo idadi ya kura zilizopigwa imezidi idadi ya wapiga kura. Kwa mfano ukijumlisha matokeo ya Jimbo la Makunduchi Zanzibar kwa wagombea wote utapata kura 10,382. Lakini idadi ya kura halali ni 10,352. Yani kura zilikua nyingi kuliko idadi ya wapiga kura. Sasa sijui kama kuna watu walipiga kura mara mbili au vp. CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

Hali hiyo pia imejitokeza katika jimbo la Kilindi, jimbo la Bumbuli na majimbo mengine. Hii inapaswa kuingia kwenye kitabu cha records za dunia (Guiness) maana ni maajabu kupata kura nyingi kuzidi idadi ya wapiga kura.

Mwaka 1927 aliyekua Rais wa Liberia Charless King aliingia kwny kitabu cha Guiness baada ya Tume ya uchaguzi nchini humo kumtangaza kuwa ameshinda kwa kura 234,000 wakati idadi ya wapiga kura nchini kwake ilikua 15,000 tu. NEC nao wamefuata nyayo za Charless King. Wanapenda namba lakini hawajui hesabu.

5. Kwa mujibu wa NEC jimbo la Bumbuli na Bukoba mjini ndio majimbo yenye watu smart kuliko majimbo yote Tanzania maana ndio majimbo pekee ambalo hakuna hata kura moja iliyoharibika.

Kwa mfano Bumbuli Idadi ya wapiga kura ni watu 44,011 na idadi ya kura halali ni 44,011. Haya ni maajabu mengine ya dunia. Yani ktk watu 40,000 hakuna hata mmoja aliyekosea. These people are very smart.

Ni ajabu jimbo la Makunduchi Zbar lenye wapiga kura 10,000 walioharibu kura ni watu zaidi ya 100 lakini jimbo la Bumbuli lenye wapiga kura zaidi ya 40,000 hakuna hata mmoja aliyeharibu kura. Kama unaelewa Probability utajua huu ni uongo wa kiwango cha PhD. Watu 44,000 are more likely kuharibu kura nyingi kuliko watu 10,000. KaJanuary hakajui hii formular coz kanapenda namba tu lakini hakajui hesabu. Itz shame.

NINI CHANZO CHA YOTE HAYA?

Sababu inayopelekea fraud hii ya kijinga ktk kutangazwa matokeo inasababishwa na Tume kuacha kutangaza matokeo halisi na kuamua kutangaza matokeo wanayopewa na CCM.

Kuna kikosi kazi cha vijana wa CCM wanaofanya tallying na kuwatumia Tume ya Uchaguzi. Kwa hiyo matokeo yanayotoka majimboni hayaendi moja kwa moja Tume, yanapita kwanza kwa vijana wa CCM wanayachezea ndipo yanaenda Tume. Katika kufanya kazi hiyo wanakosa umakini na kukosea hata vitu vidogo kama niliorodhesha hapo.

Licha ya kubadilisha matokeo ya Urais, mbinu nyingine wanaofanya ni kupunguza kura za Lowassa kwa kuongeza kwenye idadi ya kura zilizoharibika. Katika majimbo mengi Lowassa aliyoongoza hata idadi ya kura zilizoharibika ni nyingi.

Hebu jiulize imekuaje jimbo la Arusha mjini watu zaidi ya 5000 waharibu kura? Watu 5000 ni sawa na wakazi wote wa jimbo la Wawi Zanzibar. So ni sawa na kusema jimbo lote la Wawi wameharibu kura. Impossible.!

Mbinu nyingine ni kupunguza kura za Lowassa na kuwaongezea wagombea wa vyama vidogo. Kwa mfano jimbo la Moshi mjini mgombea wa ADC alipata kuta 11 jimbo zima. Na fomu ya matokeo iliyobandikwa ofisi ya Mkurugenzi inaonesha hivyo. Lakini kwenye matokeo yaliyotangazwa na Tume inaonekana amepata kura 186. Ongezeko la kura 175. Ujinga huu wameufanya ktk majimbo mengi.

WAY FOWARD.

Sisi tumefanya tallying ya majimbo yote ya nchi nzima na tunayo matokeo halisi kama yalivyosainiwa na mawakala wa vyama vyote. Matokeo hayo yanaonesha maoni halisi ya watanzania.

Viongozi wa chama wanakutana leo na muda si mrefu watatoa tamko. Rais wa Tanzania anachaguliwa na Watanzana, ni vizuri kuheshimu maamuzi yao.!
 
Last edited by a moderator:
Makamba hajatangaza matokeo ya jimbo lolote.ni kama UKAWA ilivyosema Kwa TAARIFA zao wameshinda.lakini hawajatangaza matokeo yeyote
 
Makamba hajatangaza matokeo ya jimbo lolote.ni kama UKAWA ilivyosema Kwa TAARIFA zao wameshinda.lakini hawajatangaza matokeo yeyote
Aliyekuwa ana post matokeo kabla ya NEC ni nani? Hizo post ziko huku ni nani anaratibu? Kwanini hawakukamatwa? Sheria ni msumeno lazima ukate kote kote otherwise nchi inageuka uwanja wa fujo.
 
Yaani huyu Makamba bado hajakamatwa tu kwa kutoa matokeo kabla ya NEC. ama hii ni ile NEC ya CCM
 
Makamba hajatangaza matokeo ya jimbo lolote.ni kama UKAWA ilivyosema Kwa TAARIFA zao wameshinda.lakini hawajatangaza matokeo yeyote

Kwa hiyo unakubali kwamba kukamatwa kwa vijana wa UKawa ni uonevu ?

Na je Makamba naye anapaswa kukamatwa kwa kuwa anafanya vile vile walivyofanya vijana wa Ukawa?
 
Back
Top Bottom