January Makamba ajihami kupitia

Unaunga juhudi za wengine kufukuzwa huku hutaki Makamba kufuzwa, unfair treatment hii na maslahi binafsi nilitegemea kuwa sheria ichukue mkondo wake
 
Wa buddha huwa wanamsemo maarufu husemao:Three things cannot be long hidden.The sun,the moon and the truth.Anaweza kuwa amefanikiwa kulizima hili skendo kwa kumnyamazisha huyo mzungu kwa pesa,lakini hipo siku hili jinamizi litamjia tena.

Mimi binafsi huamini mtu anapokuwa amehudhika au kughadhibika na jambo fulani dhidi ya mtu fulani.Kile kimtokacho mdomoni kwa wakati huo ni ukweli mtupu.Mzungu ameyasema ya moyoni.Na imedhihirika kuna lengo lililomfanya huyu mzungu kuwa karibu na familia ya makamba.Kama makamba alivyokiri kuna madili makubwa na penyo aliloliona kupitia kwake kwa maana ndiyo michezo aliyoizoea kuicheza.

Kumbukeni MYTH IS MUCH MORE IMPORTANT AND TRUE THAN HISTORY.Wale waliosema wakina balile wanaandika stori za kusadikika kwenye gazeti la jamhuri,baadaye walikuja kuumbuka pale Magu aliposema walichoandika ni ukweli.Najua mnampenda January na mko radhi kumtetea kwa maslahi yenu.Hila tukumbuke Taifa ni kubwa kuliko mtu mmoja.
 
endeleeni kufukuzana na upepo tu.. Tunaishi kwa kuanzisha matukio ili kuwaondoa kule mliko ili mje huku kisha kule tuendelea
 
Huyu mleta mada inavoonesha atakuwa na uhusiano wa karibu na mh. Makamba. Maana alivotapika kwenye hii thread yake nikama amekunywa pombe uliooza.
 
Nafikiri Mh. Makamba angejitokeza ajitee mwenyewe kuliko hawa ambao naona kama wanazidi kuharibu zaidi
 
Mkuu, ungehudhuria mkutano wa yule Muitaliano leo pale Hyatt Hotel ili umbane kwa maswali, na kama ametunga uongo yote yatadhihirika kupitia majibu atakayokuwa anadefend. Sasa unamtetea jamaa bila kielelezo chochote zaidi ya stori za hapo Cruz-In, wakati Muitaliano anamuangamiza kwa vielelezo bila kupingwa, unadhani watu watamuamini nani kati yako na Muitaliano?
Mkuu kikao kimefanyika kwani
 
halafu tunaambiwa hawa vijana ni wasomi na wana akili sana , sasa kwanini wanashindwa kuanzisha mambo mengine zaidi ya kung'ang'ania ajira za babazao ? mfano wa karibu ni mimi erythrocyte , pamoja na kwamba sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania lakini nilitumia vizuri elimu yangu na sasa nimeajiri watz zaidi ya 300 , hawa wanaogopa nini , si wana akili sana ?
mioga, mijizi, mikwapuaji. Inaogopa ikijiajiri yenyewe haiwezi kujikwapulia.
 
Mkuu, ungehudhuria mkutano wa yule Muitaliano leo pale Hyatt Hotel ili umbane kwa maswali, na kama ametunga uongo yote yatadhihirika kupitia majibu atakayokuwa anadefend. Sasa unamtetea jamaa bila kielelezo chochote zaidi ya stori za hapo Cruz-In, wakati Muitaliano anamuangamiza kwa vielelezo bila kupingwa, unadhani watu watamuamini nani kati yako na Muitaliano?

Wakuu, tupeni feedback za huo mkutano kwa yule atakayezipata. Wengi tunataka kujua zaidi kuhusu "saga" hili.
 
Mkuu wasomi wetu ni majipu, wasoni wetu wapiga dili, wasomi wetu wezi, wasomi wetu waongo wanapenda kuishi unafiki, bora hata mie mkulima wa maharage Na mihogo kuliko hawa wanojiita wasomi

Wanaingia wakiwa safi. Punde kidogo tu, wanakuwa "corrupted" na mfumo wa serikali yao wenyewe.
 
halafu tunaambiwa hawa vijana ni wasomi na wana akili sana , sasa kwanini wanashindwa kuanzisha mambo mengine zaidi ya kung'ang'ania ajira za babazao ? mfano wa karibu ni mimi erythrocyte , pamoja na kwamba sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania lakini nilitumia vizuri elimu yangu na sasa nimeajiri watz zaidi ya 300 , hawa wanaogopa nini , si wana akili sana ?
Hongera mkuu, kumbe ni mkurugenzi. Watz 300 wanapata mahitaji kupitia Erythrocyte. Si jambo la kitoto.
 
Dah umezunguka weeeeeeee kumbe lengo kumtetea the makambaz ~~~~mtumishi/kiongozi wa umma haruhusiwi kupokea zawadi inayozidi elfu hamsini (50,000/=). Akifanya hivyo lazima aitaarifu mamlaka.........Tena kanuni imesungumzia zawadi ambayo chanzo chake unaifahamu sembuse midola from unknown source?
 
Utetezi kama huu ndo unatufanya hata wengine ambao bado tunampa benefit of doubt Makamba tuanze kuchoka.Bora kukaa kimya mjipange kwanza mtoe utetezi unaoeleweka vinginevyo hata kama anasingiziwa mnazidi kumchimbia "kaburi"

Ingawa wanasema aliyeleta kashfa hii ni kichaa tusimwamini, lakini nilivyosoma issue yote, nimegundua she is actually very intergent! Hata zile audio alizopost, ameweka kimtego sana, maana ni vipende tu. Hakuna anayejua mwendelezo wake kamili! lakini, hatua yake pia ya kusema she is buying time to allow the victim to talk, ni ya hatari zaidi, na haionyeshi kama huyu binti ni mjinga kama wengi wanavyofikiri.
 
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. .

Mkuu umetumia nguvu nyingi kama mtu unayemwandikia hajui wajibu wake na hajui kama ana vyombo vya kumsaidia.
Kwa taarifa yako kabla Rais hajazungusha panga lake, huchukua baadhi ya hatua kujiridhisha, kwa mfano kama issue hii ya JM inaharufu ya rushwa ndani yake maana yake kama JPM anashawishika kwenye maelezo ya awali kuwa huenda kuna Jinai imetendeka atakachofanya ni kuviamuru vyombo vyake vipelelezi na kumpa ukweli juu ya jambo husika. Maana yake vyombo hivyo vitapeleleza na kuchunguza kwa kuwahoji wahusika wazi na kisirisiri, watakusanya vielelezo na kuvipitia, Kisha wataandika taarifa na baadaye watampatia Rais ambaye baada ya kupewa briefing na kuisoma Taarifa bado akijiridhisha kuwa kuna makosa aidha ya Jinai au ya kimaadili atamwaita washauri wake wa masuala ya Utawala, na mshauri wa mambo ya Siasa atazungumza nao juu ya hiyo kadhia. Baada ya kushauriana na hao washauri atamwita mhusika na kumpa nafasi ya kujitetea, akishindwa kujiclear kuna option mbili, aidha apishe au asubili kutumbuliwa.

Sasa unachotaka kutuaminisha ni kuwa Presida akisikia jambo anakimbia kushika mkasi kutumbua bila kuangalia kama ni Jipu, Kovu, Upele au chunusi, yeye ni tumbu tumbua tu. Rais ana mikono Mingi, ana PCCB, Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi (CID), Ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali, Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya Jinai (DCI), Tume ya maadili kwa watumishi wa Umma, nk una maana vyombo vyote hivi vikisema fulani mchafu vitakuwa vimeshinikizwa na vijimaneno vya Mtandaoni.
 
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Na Paul Mwandemele

Rais wangu mpendwa, nakuandikia kwa heshima kubwa. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanyia nchi yetu, hasa safishasafisha ya viongozi wabovu. Kazi hii imepokelewa vizuri na wananchi.

Hata hivyo watu wengi tunaoishi huku mitaani na kufuatilia mwendeno wa Serikali yako tumebaini mwelekeo mmoja ambao napenda nikujulishe ili hili suala lisije kukuharibia na kuharibu kazi nzuri inayofanywa.

Majuzi nilikuwa kwenye mgawaha mmoja unaitwa Cruz-In Mikocheni. Wadau tuliokuwa nao walikuwa na mjadala mzito kuhusu Serikali yako. Upande mmoja wanasema Serikali yako inafukuza watu kwa ajili tu ya sifa kwa umma na kwamba kuna watu wengi wanaonewa. Wanasema kwamba ukitaka mtu afukuzwe na Rais wewe mchafue tu kwenye vyombo vya habari, tengeneza mazingira kama hatakiwi na jamii na utaona kama Rais hatamfukuza. Kwa upande mwingine, ambao nami nimo, tulikuwa tunapinga na tunasema Rais ni mtu wa haki, anafuata sheria na ukiona mtu katimuliwa ujue uchunguzi umefanyika na uchunguzi sio lazima utangazwe na kwamba mtu huyo kapewa haki ya kuelezea upande wake. Sisi tukasema Rais ni mtu wa haki. Lakini tulibishiwa sana.

Rais wangu jamii yetu imeharibika. Watu wanafurahia wengine wakidhalilika. Watu wanapenda kuona damu. Watu wanapenda visasi. Watu wanachukiana. Wengine wanafurahia safishasafisha sio kwasababu inasaidia nchi, bali kwasababu kuna watu wanaumbuka. Kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuna watu sasa wanatengeneza orodha ya nani anayefuatia kwenye kuumbuliwa. Dhana ya utumbuaji majipu wanaipotosha. Visasi vyao wanataka vikamilishwe na Serikali yako. Naomba usikubali kabisa. Moja ya sifa ya kiongozi ni kutenda haki. Rais ameshika upanga mkuu na upanga huo una makali na anaweza kuutumia atakavyo. Rais wangu usikubali watu wakushinikize kuzungusha upanga kwasababu tu ya raha ya kuona kichwa kinadondoka.

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. Pamoja na kujua kabisa kwa uhakika kwamba wanayozungusha ni ya kutunga, wanajihakikishia kwamba Magufuli anaamka na upanga na akisikia tu mabaya haulizi, anakata. Lakini mimi najua huyu siye Magufuli niliyempa kura yangu. Magufuli niliyempa kura yangu ni mtu wa haki.

Tuendelee na safishasafisha Rais wangu. Ila ni muhimu watu wanaopenda kufitiniana wajue Rais wangu ni mtu wa haki. Sio ukimsema tu kiongozi kwenye Serikali yake basi upanga unampitia. Wakijua hivyo Rais hayumbi, fitina zitapungua kwenye Serikali na kwenye siasa. Umechagua timu imara kwenye Serikali yako. Nimefurahi kwamba pamoja na mashinikizo na fitina kuhusu Prof Muhongo na Prof Maghembe bado umewapa nafasi wakusaidie. Umetengeneza sifa nzuri kwamba maneno ya magazeti na mitandaoni hayasukumi uamuzi wako. Kuna ambao hawapendi kwamba baadhi ya watu wamo kwenye Serikali yako. Simama imara na timu yako, anayeharibu atolewe, anayesakamwa kwa fitina simama naye, utaijengea timu yako kujiamini katika kazi zao na watakufanyia kazi nzuri. Tusikubali kurudi kule kwenye miaka 10 iliyopita ambapo nchi ilipitia Mawaziri 121 kwasababu fitina ziliruhusiwa, na Mawaziri wakawa wanapukutishwa kila miezi sita. Unayo nafasi kubwa ya kuisaidia nchi kumaliza fitina kwenye siasa nchini kwa kuonyesha kwamba huchukui hatua kwa kufuata upepo, ambao zama hizi unatengenezwa mezani.

Nisamehe kama nimekukwaza kwa kutoa ushauri lakini mimi nimekupa kura yangu na ni mdau mkubwa wa kutaka Serikali yako ifanikiwe.


Amekuwa Mh Rais akituomba tumuombee ili Mwenezi Mungu amjalie hekima na busara katika kututumikia. kamwe hawezi kufanya kwa mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom