January Makamba ajihami kupitia

January Makamba ajihami kupitia

Mkuu, ungehudhuria mkutano wa yule Muitaliano leo pale Hyatt Hotel ili umbane kwa maswali, na kama ametunga uongo yote yatadhihirika kupitia majibu atakayokuwa anadefend. Sasa unamtetea jamaa bila kielelezo chochote zaidi ya stori za hapo Cruz-In, wakati Muitaliano anamuangamiza kwa vielelezo bila kupingwa, unadhani watu watamuamini nani kati yako na Muitaliano?
Unajua stori za kwenye migahawa huwa zinaambatana na ulevi kwa mbaaali..
 
halafu tunaambiwa hawa vijana ni wasomi na wana akili sana , sasa kwanini wanashindwa kuanzisha mambo mengine zaidi ya kung'ang'ania ajira za babazao ? mfano wa karibu ni mimi erythrocyte , pamoja na kwamba sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania lakini nilitumia vizuri elimu yangu na sasa nimeajiri watz zaidi ya 300 , hawa wanaogopa nini , si wana akili sana ?
NYUMBU UMEAJIRI NANI ZAIDI YA KUKESHA HUMU UNATUKANA WATU.
 
Magu angekuwa anaufuata ushauri wa kwenye mitandao mwaziri wengi wasingeingia kwenye cabinet yake mfano Muhongo, Mwakyemebe na huyo januari wako.
 
Rais ni taasisi inayojitegemea, ni taasisi yenye vitendea kazi vyote muhimu, ni taasisi yenye watendaji wenye utashi na wanaojua wajibu wao, kama umefuatilia kwa makini baadhi ya hotuba za Rais, anasema:
  • Hayupo kwa ajili ya kumuonea mtu yeyote...
  • Yeye ni Rais wa watanzania wote bila kujali itikadi, dini wala makabila...
  • Anajua majipu yako mengi na mengine tena makubwa yapo ndani ya chama chetu...
  • naomba watanzania wa dini zote mniombee nitakapokuwa natekeleza wajibu wangu...
  • nk
Kwa maneno hayo machache kati ya mengi ambayo Rais amekuwa anasema karibu katika kila hotuba zake yanaashiria ufahamu wake juu ya mambo anayoyafanyia kazi ni wa kutosha na maamuzi yake yanafanywa kwa umakini zaidi ya vile tujuavyo mimi na wewe;

Nakushauri ndugu yangu, senior member mwenzangu Bak byzo I.Ttumwache Rais atupeleke tulikomwomba atupeleke, maana sisi kama abiria tuna mitazamo mingi yenye maslahi binafsi nk. (kumchomea au kumtetea Makamba) ningeshauri tena tutambue kuwa chombo kipo safarini, tumwache rubani afanye kazi yake nasi kwa upande mwingine tuendelee kutimiza wajibu wetu
 
Mimi nadhani Rais ana taarifa nyingi za viongozi waandamizi kuliko tunavyoweza kujidai kumshauri kwa nyepesi nyepesi tunazosikia huku mtaani. Rais anaousalama wa taifa ambao bila shaka wanapatia taarifa zozote za mhusika pale anapozihitaji. Hawezei kushindwa kupata nyeti za Makamba hadi aliyetoa bango ajifanye kuwa mshauri wa Rais katika hili.
 
Naona kuna uzi jamaa kauleta ambao unaelezea yule mtaliano yupo tayari hayt hotel kwa kuyatoa ya moyoni na kuweka mambo wazi huo uzi naona umefutwa na mods
 
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Na Paul Mwandemele

Rais wangu mpendwa, nakuandikia kwa heshima kubwa. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanyia nchi yetu, hasa safishasafisha ya viongozi wabovu. Kazi hii imepokelewa vizuri na wananchi.

Hata hivyo watu wengi tunaoishi huku mitaani na kufuatilia mwendeno wa Serikali yako tumebaini mwelekeo mmoja ambao napenda nikujulishe ili hili suala lisije kukuharibia na kuharibu kazi nzuri inayofanywa.

Majuzi nilikuwa kwenye mgawaha mmoja unaitwa Cruz-In Mikocheni. Wadau tuliokuwa nao walikuwa na mjadala mzito kuhusu Serikali yako. Upande mmoja wanasema Serikali yako inafukuza watu kwa ajili tu ya sifa kwa umma na kwamba kuna watu wengi wanaonewa. Wanasema kwamba ukitaka mtu afukuzwe na Rais wewe mchafue tu kwenye vyombo vya habari, tengeneza mazingira kama hatakiwi na jamii na utaona kama Rais hatamfukuza. Kwa upande mwingine, ambao nami nimo, tulikuwa tunapinga na tunasema Rais ni mtu wa haki, anafuata sheria na ukiona mtu katimuliwa ujue uchunguzi umefanyika na uchunguzi sio lazima utangazwe na kwamba mtu huyo kapewa haki ya kuelezea upande wake. Sisi tukasema Rais ni mtu wa haki. Lakini tulibishiwa sana.

Rais wangu jamii yetu imeharibika. Watu wanafurahia wengine wakidhalilika. Watu wanapenda kuona damu. Watu wanapenda visasi. Watu wanachukiana. Wengine wanafurahia safishasafisha sio kwasababu inasaidia nchi, bali kwasababu kuna watu wanaumbuka. Kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuna watu sasa wanatengeneza orodha ya nani anayefuatia kwenye kuumbuliwa. Dhana ya utumbuaji majipu wanaipotosha. Visasi vyao wanataka vikamilishwe na Serikali yako. Naomba usikubali kabisa. Moja ya sifa ya kiongozi ni kutenda haki. Rais ameshika upanga mkuu na upanga huo una makali na anaweza kuutumia atakavyo. Rais wangu usikubali watu wakushinikize kuzungusha upanga kwasababu tu ya raha ya kuona kichwa kinadondoka.

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. Pamoja na kujua kabisa kwa uhakika kwamba wanayozungusha ni ya kutunga, wanajihakikishia kwamba Magufuli anaamka na upanga na akisikia tu mabaya haulizi, anakata. Lakini mimi najua huyu siye Magufuli niliyempa kura yangu. Magufuli niliyempa kura yangu ni mtu wa haki.

Tuendelee na safishasafisha Rais wangu. Ila ni muhimu watu wanaopenda kufitiniana wajue Rais wangu ni mtu wa haki. Sio ukimsema tu kiongozi kwenye Serikali yake basi upanga unampitia. Wakijua hivyo Rais hayumbi, fitina zitapungua kwenye Serikali na kwenye siasa. Umechagua timu imara kwenye Serikali yako. Nimefurahi kwamba pamoja na mashinikizo na fitina kuhusu Prof Muhongo na Prof Maghembe bado umewapa nafasi wakusaidie. Umetengeneza sifa nzuri kwamba maneno ya magazeti na mitandaoni hayasukumi uamuzi wako. Kuna ambao hawapendi kwamba baadhi ya watu wamo kwenye Serikali yako. Simama imara na timu yako, anayeharibu atolewe, anayesakamwa kwa fitina simama naye, utaijengea timu yako kujiamini katika kazi zao na watakufanyia kazi nzuri. Tusikubali kurudi kule kwenye miaka 10 iliyopita ambapo nchi ilipitia Mawaziri 121 kwasababu fitina ziliruhusiwa, na Mawaziri wakawa wanapukutishwa kila miezi sita. Unayo nafasi kubwa ya kuisaidia nchi kumaliza fitina kwenye siasa nchini kwa kuonyesha kwamba huchukui hatua kwa kufuata upepo, ambao zama hizi unatengenezwa mezani.

Nisamehe kama nimekukwaza kwa kutoa ushauri lakini mimi nimekupa kura yangu na ni mdau mkubwa wa kutaka Serikali yako ifanikiwe.
Hapa mtu Kama no jipu azima utumbuliwe na makamba nilazima uwajibishwe
 
Kama mfanyakazi kafukuzwa kwa kuonewa kwa nini asiende mahakamani. China wamefukuza wafanyakazi 300,000 mwaka jana tu kwa rushwa na uzembe. Kufunza ndio njia pakee tulikuwa nayo kupambana na rushwa lakini hakuna njia nyingine tujulishe. JPM andelea kutumbua majipu.
Akimfukuza huyo makamba ndio watu watamuelewa
 
Mkuu, ungehudhuria mkutano wa yule Muitaliano leo pale Hyatt Hotel ili umbane kwa maswali, na kama ametunga uongo yote yatadhihirika kupitia majibu atakayokuwa anadefend. Sasa unamtetea jamaa bila kielelezo chochote zaidi ya stori za hapo Cruz-In, wakati Muitaliano anamuangamiza kwa vielelezo bila kupingwa, unadhani watu watamuamini nani kati yako na Muitaliano?
Mkuu kilio cha watanzania ni kuona makamba anatupiwa vilago
 
Tunataka harakati za ujenzi wa viwanda alivyoahidi ziende sambamba na hiyo safisha safisha vinginevyo ni propanda
Mkuu viwanda bila ya umeme wa uhakika ni ndoto za mwenda wazimu
 
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Na Paul Mwandemele

Rais wangu mpendwa, nakuandikia kwa heshima kubwa. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanyia nchi yetu, hasa safishasafisha ya viongozi wabovu. Kazi hii imepokelewa vizuri na wananchi.

Hata hivyo watu wengi tunaoishi huku mitaani na kufuatilia mwendeno wa Serikali yako tumebaini mwelekeo mmoja ambao napenda nikujulishe ili hili suala lisije kukuharibia na kuharibu kazi nzuri inayofanywa.

Majuzi nilikuwa kwenye mgawaha mmoja unaitwa Cruz-In Mikocheni. Wadau tuliokuwa nao walikuwa na mjadala mzito kuhusu Serikali yako. Upande mmoja wanasema Serikali yako inafukuza watu kwa ajili tu ya sifa kwa umma na kwamba kuna watu wengi wanaonewa. Wanasema kwamba ukitaka mtu afukuzwe na Rais wewe mchafue tu kwenye vyombo vya habari, tengeneza mazingira kama hatakiwi na jamii na utaona kama Rais hatamfukuza. Kwa upande mwingine, ambao nami nimo, tulikuwa tunapinga na tunasema Rais ni mtu wa haki, anafuata sheria na ukiona mtu katimuliwa ujue uchunguzi umefanyika na uchunguzi sio lazima utangazwe na kwamba mtu huyo kapewa haki ya kuelezea upande wake. Sisi tukasema Rais ni mtu wa haki. Lakini tulibishiwa sana.

Rais wangu jamii yetu imeharibika. Watu wanafurahia wengine wakidhalilika. Watu wanapenda kuona damu. Watu wanapenda visasi. Watu wanachukiana. Wengine wanafurahia safishasafisha sio kwasababu inasaidia nchi, bali kwasababu kuna watu wanaumbuka. Kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuna watu sasa wanatengeneza orodha ya nani anayefuatia kwenye kuumbuliwa. Dhana ya utumbuaji majipu wanaipotosha. Visasi vyao wanataka vikamilishwe na Serikali yako. Naomba usikubali kabisa. Moja ya sifa ya kiongozi ni kutenda haki. Rais ameshika upanga mkuu na upanga huo una makali na anaweza kuutumia atakavyo. Rais wangu usikubali watu wakushinikize kuzungusha upanga kwasababu tu ya raha ya kuona kichwa kinadondoka.

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. Pamoja na kujua kabisa kwa uhakika kwamba wanayozungusha ni ya kutunga, wanajihakikishia kwamba Magufuli anaamka na upanga na akisikia tu mabaya haulizi, anakata. Lakini mimi najua huyu siye Magufuli niliyempa kura yangu. Magufuli niliyempa kura yangu ni mtu wa haki.

Tuendelee na safishasafisha Rais wangu. Ila ni muhimu watu wanaopenda kufitiniana wajue Rais wangu ni mtu wa haki. Sio ukimsema tu kiongozi kwenye Serikali yake basi upanga unampitia. Wakijua hivyo Rais hayumbi, fitina zitapungua kwenye Serikali na kwenye siasa. Umechagua timu imara kwenye Serikali yako. Nimefurahi kwamba pamoja na mashinikizo na fitina kuhusu Prof Muhongo na Prof Maghembe bado umewapa nafasi wakusaidie. Umetengeneza sifa nzuri kwamba maneno ya magazeti na mitandaoni hayasukumi uamuzi wako. Kuna ambao hawapendi kwamba baadhi ya watu wamo kwenye Serikali yako. Simama imara na timu yako, anayeharibu atolewe, anayesakamwa kwa fitina simama naye, utaijengea timu yako kujiamini katika kazi zao na watakufanyia kazi nzuri. Tusikubali kurudi kule kwenye miaka 10 iliyopita ambapo nchi ilipitia Mawaziri 121 kwasababu fitina ziliruhusiwa, na Mawaziri wakawa wanapukutishwa kila miezi sita. Unayo nafasi kubwa ya kuisaidia nchi kumaliza fitina kwenye siasa nchini kwa kuonyesha kwamba huchukui hatua kwa kufuata upepo, ambao zama hizi unatengenezwa mezani.

Nisamehe kama nimekukwaza kwa kutoa ushauri lakini mimi nimekupa kura yangu na ni mdau mkubwa wa kutaka Serikali yako ifanikiwe.

Ulianza jenga hoja yako vizuri sana, lakini katikati nikagundua kumbe ulikuwa unalenga wapi. kumbuka Rais Magufuli kachaguliwa si tu na wana CCM bali watanzania nikiwamo mimi ambaye si mwanachama wa chama chochote kile na baada ya kuwa Rais, kimsingi anatakiwa asiangalie chama bali watanzania (ingawa ni vigumu sana kuwa full neutral).

Kwa mwennendo wake ni kweli anajaribu sana labda hadi sasa kuliko watangulizi wake. Naoma uangalie hii quote ya meaning ya dectorship hapa chini.

"Dictatorship is a form of government where a country is ruled by one person or political entity, and exercised through various mechanisms to ensure the entity's power remains strong". Pamoja na maana hii, system yetu inampa Rais almost power kama hiyo, lakini pia anaweza kuitumia kurekebisha mfumo uzo kama wetu na ninaamini ndicho anacho kifanya Rais. Katika kufanya hivyo anaweza onea wengine na hata kupendelea kwa nia nzuri sana ya kurekebisha mfumo ozo.

January anaweza kufukuzwa hata kesho kama Rais atalidhika kufanya hivyo ni sehemu ya kutoa mfumo ozo na hakuna haja ya kulia kaonewa. Ndio maana pia kuna mahakama kusaidia kuzuia hili kuvuka mpaka kwa kutoa haki, na yeyote yule atakaye ona si sawa ana uhuru mkubwa tu wa kuchallenge ili apate haki yake.

Mimi suala kubwa kwangu why discuss about January, hakuna mambo mengine ya maana ya kubadilishana mawazo? Wametoleana skendo zao ni juu ya Rais kupima waziri wake kuingizwa katika skendo amtoe amwache na kuna madhala gani kwa pande zote. Nyerere aliwahi sema, kiongozi wa uuma hastahili hata kushutumiwa tu. Sasa Rais aangalie uzito mwenyewe, sio ninyi wapambe kwa sababu zenu binafsi.
 
Hii ishu ilikuwa ya weekend, ishapoteza mvuto jinsi ilivyokuwa hyped! Kama kuna maamuI yoyote, mwachieni mkuu!
indueni topic nyeti zingine.
 
Usiku wa jana watu wamelipwa wakakesha kuandaa nyaraka za kumtetea yule dogo anayeuza rasimali sambamaba na papuchi ya dafaye.
Mkuu hiyo haitasaidia kitu kama no maji ndiyo tayari yamesha mwagika
 
Usiku wa jana watu wamelipwa wakakesha kuandaa nyaraka za kumtetea yule dogo anayeuza rasimali sambamaba na papuchi ya dafaye.
Kwani papuchi ya dafaye nayo ni rasiliamali, acha bhana!!!!
 
Hii ishu ilikuwa ya weekend, ishapoteza mvuto jinsi ilivyokuwa hyped! Kama kuna maamuI yoyote, mwachieni mkuu!
indueni topic nyeti zingine.
 
Tunataka harakati za ujenzi wa viwanda alivyoahidi ziende sambamba na hiyo safisha safisha vinginevyo ni propanda
Ni kweli kabisa, maisha ya mtanzania wa chini yanazidi kuwa magumu. Kubana na ku create fursa vilikuwa viendane pamoja.
 
Back
Top Bottom