January Makamba ajihami kupitia

Bak byzo I.T

JF-Expert Member
Jun 29, 2014
264
122
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Na Paul Mwandemele

Rais wangu mpendwa, nakuandikia kwa heshima kubwa. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanyia nchi yetu, hasa safishasafisha ya viongozi wabovu. Kazi hii imepokelewa vizuri na wananchi.

Hata hivyo watu wengi tunaoishi huku mitaani na kufuatilia mwendeno wa Serikali yako tumebaini mwelekeo mmoja ambao napenda nikujulishe ili hili suala lisije kukuharibia na kuharibu kazi nzuri inayofanywa.

Majuzi nilikuwa kwenye mgawaha mmoja unaitwa Cruz-In Mikocheni. Wadau tuliokuwa nao walikuwa na mjadala mzito kuhusu Serikali yako. Upande mmoja wanasema Serikali yako inafukuza watu kwa ajili tu ya sifa kwa umma na kwamba kuna watu wengi wanaonewa. Wanasema kwamba ukitaka mtu afukuzwe na Rais wewe mchafue tu kwenye vyombo vya habari, tengeneza mazingira kama hatakiwi na jamii na utaona kama Rais hatamfukuza. Kwa upande mwingine, ambao nami nimo, tulikuwa tunapinga na tunasema Rais ni mtu wa haki, anafuata sheria na ukiona mtu katimuliwa ujue uchunguzi umefanyika na uchunguzi sio lazima utangazwe na kwamba mtu huyo kapewa haki ya kuelezea upande wake. Sisi tukasema Rais ni mtu wa haki. Lakini tulibishiwa sana.

Rais wangu jamii yetu imeharibika. Watu wanafurahia wengine wakidhalilika. Watu wanapenda kuona damu. Watu wanapenda visasi. Watu wanachukiana. Wengine wanafurahia safishasafisha sio kwasababu inasaidia nchi, bali kwasababu kuna watu wanaumbuka. Kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuna watu sasa wanatengeneza orodha ya nani anayefuatia kwenye kuumbuliwa. Dhana ya utumbuaji majipu wanaipotosha. Visasi vyao wanataka vikamilishwe na Serikali yako. Naomba usikubali kabisa. Moja ya sifa ya kiongozi ni kutenda haki. Rais ameshika upanga mkuu na upanga huo una makali na anaweza kuutumia atakavyo. Rais wangu usikubali watu wakushinikize kuzungusha upanga kwasababu tu ya raha ya kuona kichwa kinadondoka.

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. Pamoja na kujua kabisa kwa uhakika kwamba wanayozungusha ni ya kutunga, wanajihakikishia kwamba Magufuli anaamka na upanga na akisikia tu mabaya haulizi, anakata. Lakini mimi najua huyu siye Magufuli niliyempa kura yangu. Magufuli niliyempa kura yangu ni mtu wa haki.

Tuendelee na safishasafisha Rais wangu. Ila ni muhimu watu wanaopenda kufitiniana wajue Rais wangu ni mtu wa haki. Sio ukimsema tu kiongozi kwenye Serikali yake basi upanga unampitia. Wakijua hivyo Rais hayumbi, fitina zitapungua kwenye Serikali na kwenye siasa. Umechagua timu imara kwenye Serikali yako. Nimefurahi kwamba pamoja na mashinikizo na fitina kuhusu Prof Muhongo na Prof Maghembe bado umewapa nafasi wakusaidie. Umetengeneza sifa nzuri kwamba maneno ya magazeti na mitandaoni hayasukumi uamuzi wako. Kuna ambao hawapendi kwamba baadhi ya watu wamo kwenye Serikali yako. Simama imara na timu yako, anayeharibu atolewe, anayesakamwa kwa fitina simama naye, utaijengea timu yako kujiamini katika kazi zao na watakufanyia kazi nzuri. Tusikubali kurudi kule kwenye miaka 10 iliyopita ambapo nchi ilipitia Mawaziri 121 kwasababu fitina ziliruhusiwa, na Mawaziri wakawa wanapukutishwa kila miezi sita. Unayo nafasi kubwa ya kuisaidia nchi kumaliza fitina kwenye siasa nchini kwa kuonyesha kwamba huchukui hatua kwa kufuata upepo, ambao zama hizi unatengenezwa mezani.

Nisamehe kama nimekukwaza kwa kutoa ushauri lakini mimi nimekupa kura yangu na ni mdau mkubwa wa kutaka Serikali yako ifanikiwe.
 
Kama mfanyakazi kafukuzwa kwa kuonewa kwa nini asiende mahakamani. China wamefukuza wafanyakazi 300,000 mwaka jana tu kwa rushwa na uzembe. Kufunza ndio njia pakee tulikuwa nayo kupambana na rushwa lakini hakuna njia nyingine tujulishe. JPM andelea kutumbua majipu.
 
... Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. ...
Mkuu, ungehudhuria mkutano wa yule Muitaliano leo pale Hyatt Hotel ili umbane kwa maswali, na kama ametunga uongo yote yatadhihirika kupitia majibu atakayokuwa anadefend. Sasa unamtetea jamaa bila kielelezo chochote zaidi ya stori za hapo Cruz-In, wakati Muitaliano anamuangamiza kwa vielelezo bila kupingwa, unadhani watu watamuamini nani kati yako na Muitaliano?
 
Walipopigwa chini wengine kwa visa vinavyokaribiana mlikaa kimya,Leo yamemkuta jamaa yenu ndio mnapiga kelele?
WARAKA KWA RAIS MAGUFULI

Rais Magufuli usikubali watu wakutumie kumalizana

Na Paul Mwandemele

Rais wangu mpendwa, nakuandikia kwa heshima kubwa. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanyia nchi yetu, hasa safishasafisha ya viongozi wabovu. Kazi hii imepokelewa vizuri na wananchi.

Hata hivyo watu wengi tunaoishi huku mitaani na kufuatilia mwendeno wa Serikali yako tumebaini mwelekeo mmoja ambao napenda nikujulishe ili hili suala lisije kukuharibia na kuharibu kazi nzuri inayofanywa.

Majuzi nilikuwa kwenye mgawaha mmoja unaitwa Cruz-In Mikocheni. Wadau tuliokuwa nao walikuwa na mjadala mzito kuhusu Serikali yako. Upande mmoja wanasema Serikali yako inafukuza watu kwa ajili tu ya sifa kwa umma na kwamba kuna watu wengi wanaonewa. Wanasema kwamba ukitaka mtu afukuzwe na Rais wewe mchafue tu kwenye vyombo vya habari, tengeneza mazingira kama hatakiwi na jamii na utaona kama Rais hatamfukuza. Kwa upande mwingine, ambao nami nimo, tulikuwa tunapinga na tunasema Rais ni mtu wa haki, anafuata sheria na ukiona mtu katimuliwa ujue uchunguzi umefanyika na uchunguzi sio lazima utangazwe na kwamba mtu huyo kapewa haki ya kuelezea upande wake. Sisi tukasema Rais ni mtu wa haki. Lakini tulibishiwa sana.

Rais wangu jamii yetu imeharibika. Watu wanafurahia wengine wakidhalilika. Watu wanapenda kuona damu. Watu wanapenda visasi. Watu wanachukiana. Wengine wanafurahia safishasafisha sio kwasababu inasaidia nchi, bali kwasababu kuna watu wanaumbuka. Kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kuna watu sasa wanatengeneza orodha ya nani anayefuatia kwenye kuumbuliwa. Dhana ya utumbuaji majipu wanaipotosha. Visasi vyao wanataka vikamilishwe na Serikali yako. Naomba usikubali kabisa. Moja ya sifa ya kiongozi ni kutenda haki. Rais ameshika upanga mkuu na upanga huo una makali na anaweza kuutumia atakavyo. Rais wangu usikubali watu wakushinikize kuzungusha upanga kwasababu tu ya raha ya kuona kichwa kinadondoka.

Mifano ya mashinikizo haya ipo mingi. Lakini mfano wa karibuni ni wa Waziri wako, January Makamba. Lipo kundi limejiapiza kwamba lazima aanguke na tunapowasoma mitandaoni wanasema wazi kabisa namna ya kumuangusha kijana wako huyu ni kumtengenezea uchafu wa kutunga ili Magufuli aone raha kuzungusha upanga. Pamoja na kujua kabisa kwa uhakika kwamba wanayozungusha ni ya kutunga, wanajihakikishia kwamba Magufuli anaamka na upanga na akisikia tu mabaya haulizi, anakata. Lakini mimi najua huyu siye Magufuli niliyempa kura yangu. Magufuli niliyempa kura yangu ni mtu wa haki.

Tuendelee na safishasafisha Rais wangu. Ila ni muhimu watu wanaopenda kufitiniana wajue Rais wangu ni mtu wa haki. Sio ukimsema tu kiongozi kwenye Serikali yake basi upanga unampitia. Wakijua hivyo Rais hayumbi, fitina zitapungua kwenye Serikali na kwenye siasa. Umechagua timu imara kwenye Serikali yako. Nimefurahi kwamba pamoja na mashinikizo na fitina kuhusu Prof Muhongo na Prof Maghembe bado umewapa nafasi wakusaidie. Umetengeneza sifa nzuri kwamba maneno ya magazeti na mitandaoni hayasukumi uamuzi wako. Kuna ambao hawapendi kwamba baadhi ya watu wamo kwenye Serikali yako. Simama imara na timu yako, anayeharibu atolewe, anayesakamwa kwa fitina simama naye, utaijengea timu yako kujiamini katika kazi zao na watakufanyia kazi nzuri. Tusikubali kurudi kule kwenye miaka 10 iliyopita ambapo nchi ilipitia Mawaziri 121 kwasababu fitina ziliruhusiwa, na Mawaziri wakawa wanapukutishwa kila miezi sita. Unayo nafasi kubwa ya kuisaidia nchi kumaliza fitina kwenye siasa nchini kwa kuonyesha kwamba huchukui hatua kwa kufuata upepo, ambao zama hizi unatengenezwa mezani.

Nisamehe kama nimekukwaza kwa kutoa ushauri lakini mimi nimekupa kura yangu na ni mdau mkubwa wa kutaka Serikali yako ifanikiwe.
 
Usiku wa jana watu wamelipwa wakakesha kuandaa nyaraka za kumtetea yule dogo anayeuza rasimali sambamaba na papuchi ya dafaye.
Nitawaona malofa sana kama kwa kumtetea huku tangia jana washindwe hata kutengeneza pesa ya kununua vits...

Kama kwa kazi hii wanayoifanya tangia jana wanalipwa bundle la elfu 7 nitawaona wapuuzi sana...
 
Usiku wa jana watu wamelipwa wakakesha kuandaa nyaraka za kumtetea yule dogo anayeuza rasimali sambamaba na papuchi ya dafaye.
halafu tunaambiwa hawa vijana ni wasomi na wana akili sana , sasa kwanini wanashindwa kuanzisha mambo mengine zaidi ya kung'ang'ania ajira za babazao ? mfano wa karibu ni mimi erythrocyte , pamoja na kwamba sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania lakini nilitumia vizuri elimu yangu na sasa nimeajiri watz zaidi ya 300 , hawa wanaogopa nini , si wana akili sana ?
 
Utetezi kama huu ndo unatufanya hata wengine ambao bado tunampa benefit of doubt Makamba tuanze kuchoka.Bora kukaa kimya mjipange kwanza mtoe utetezi unaoeleweka vinginevyo hata kama anasingiziwa mnazidi kumchimbia "kaburi"
 
halafu tunaambiwa hawa vijana ni wasomi na wana akili sana , sasa kwanini wanashindwa kuanzisha mambo mengine zaidi ya kung'ang'ania ajira za babazao ? mfano wa karibu ni mimi erythrocyte , pamoja na kwamba sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania lakini nilitumia vizuri elimu yangu na sasa nimeajiri watz zaidi ya 300 , hawa wanaogopa nini , si wana akili sana ?
Mkuu wasomi wetu ni majipu, wasoni wetu wapiga dili, wasomi wetu wezi, wasomi wetu waongo wanapenda kuishi unafiki, bora hata mie mkulima wa maharage Na mihogo kuliko hawa wanojiita wasomi
 
Tumeshasahau kabisa kuhusu Uchaguzi wa Wazanzibar, Na ule uhuni wa Ras pamoja Na wanasheria wake kuhusu meya wa jiji, kweli sie wadanganyika
Kuja kushituka Zanzibar ina Rais na Meya kachaguliwa afu tutapigwa stori nyingine ya nguvu tuzidi kupotea haaaa haaa
 
Back
Top Bottom