janja na janjaure.

janja na janjaure.

fundiaminy

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2009
Posts
354
Reaction score
52
jamaa baada ya kutoka dili mida ya saa mbili usiku alijisachi na akapata hana nauli ya taxi.hivyo akasimamisha taxi huku akipiga mahesabu itakuaje.alipouliza bei dereva akamuambia elfu tano.hakusita akaingia na taxi ikampeleka na alipokaribia kwake akamuambia dereva tafadhali simamisha hapo niwahi pale dukani nikanunue kiberiti manake nimeangusha pochi yangu ndani ya taxi yako na ina laki mbili ndani.dereva akamuambia wahi fasta tuendelee na safari.jamaa kwenda dukani na kurudi dakika tano tu kapata dereva keshachomoka kitaaambo.jamaa taratibu huku akicheka akamalizia hatua chache zilizobaki mpaka kwake..
UKIJIFANYA JANJA IKO JANJA ZAIDI YAKO.
 
Kweli ugumu wa maisha ni kipimo cha akili
 
alidhan kapanda kumbe ndiye kavunwa, kwel kuzaliwa mjn ni elimu ya form 6 tayari
 
Dah! Jamaaa ni ni noma bwana! Dereva tax imekula kwake hapo!!!
 
Na akijaribu kurudi kwa jamaa, atadaiwa laki mbili hewa na pochi na vitambulisho, hivyo itabidi auchune tu
 
Hivi nani zaidi kati ya janja na janjaure?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom