Janga lingine sekta ya Elimu: Walimu wafeli Mtihani

Janga lingine sekta ya Elimu: Walimu wafeli Mtihani

Ya Mulugo hayo....tuna mengi ya kushuhudia hadi 2015
 
Hivi ni rais gani vile wa Tanzania aliyeanzisha waalimu wa UPE? Watu ambao walikuwa wameshindwa kuingia sekondari lakini hawajafeli sana walikuwa wanachaguliwa kwenda kusomea ualimu?
Naombeni jina la rais huyo tafadhali.
 
Ukimcezea mpishi anaweka pilpili nyingi katika chakuala tuone kama mtakula.

Tutastandadaizi.

Halafu hili kwa Bongo sio tatizo kabisa
kuna kauli maalum zinaweza kutumika:-

1. Ni upepo tu JK
2. Liwalo na liwe
3. Tumechoka sasa,wapigwe tu MP

Adies amigos.
 
Hivi ni rais gani vile wa Tanzania aliyeanzisha waalimu wa UPE? Watu ambao walikuwa wameshindwa kuingia sekondari lakini hawajafeli sana walikuwa wanachaguliwa kwenda kusomea ualimu?
Naombeni jina la rais huyo tafadhali.

Walimu waliochaguliwa kwenda kifundisha upe siku hizi ni madokta na maprofesa. Wengine waliobaki wamejiendeleza sana. Walikuwa waajjlikana kama B/C. Huwezi kulinganisha Drs. 7 la wakati ule hata na F4 ya sasa. Wale walimudu kazi zao. Lakini sasa wanafunzi hawafunfishwi ili waelewe bali ili wafaulu mitihani. Sasa hata wao wamechoka liwalo na liwe. Unategemea nini from wrongly standardised marks? Not much of course. Bila shaka hali itakuwa mbaya zaidi mwakani. Pathetic.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Duuuuuh Khali Mbaya Jamani! Hata Hao Waliopata Daraja La 2 & 3 Ni Vilaza Vile Vile.....

kama wewe na familia yako mlivyo vilaza??.embu nenda wewe kasome diploma ya ualimu ndo utajua kwanini hakuna distiction hata moja tena nahisi kwa wewe hata hiyo pass itakuwa kizungumkuti,huwezi kufikiri ni kwanini vyuo vyote hali ipo ivo ilivo?? diploma sio sawa na degree mnazo peana vyuon kisa umeweza kumvulia chup prof (kwa wenye tabia hizo lakini).na nikuhakikishia hakuna elimu ngumu kwa sasa kama diploma ya ualimu nafikiri walio pitia diploma ya elimu kwa miaka ya hivi karibuni wananielewa, diploma ya sasa sio kama ile ya zamani hata ukiwa na sap unapita tu, hakuna hiyo kitu kwa sasa yaan hata ungekuwa na 'A' tisa ukipata F moja huna chako ,then mambo ni mengi ya kusoma halafu mda mchache nliwahi kuwa mkufunzi chuo fulan miaka ya nyuma nililiona hilo na lipo wazi nafikiri wahusika wanajua.ndio mana huwa wanasema mwalimu mmoja wa diploma ni sawa na walimu watatu wa degree katika ufanisi.diploma ya ualimu sio rahisi kama wengine wanavo dhani.
 
Haya ni matokeo mazuri, yakimaanisha kwamba wengi kati ya waliokwenda kusomea ualimu hawakuwa na sifa hizo, bali walifanya hivyo kwa kukosa njia mbadala! Hata hivyo mtihani umetuchagulia wachache tu ambao wanaweza kutoa elimu stahiki. Kama ukichunguza entry qualification zao utaweza kupata jibu. Kwahiyo kwa mtazamo wangu mimi, haya ni matokeo mazuri sana kwa fani ya ualimu. Mara nyengine, watu wa hovyo hovyo hawatakua na courage ya kujiunga vyuo vya ualimu.
yaaaaani nimetamani kama kungekuwa na like hata kumi sasa ndo ivo tena,kweli ndugu umefikiri critically wacha nikugongee like za live live ,:A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up::A S thumbs_up:😛oa
 
Mleta mada unashangaza kuliita hilo kuwa ni janga.

Mimi naona hapo mambo ni mazuri kabisa, tumepata Waalimu wapya waliofaulu zaid ya 6,000

1) Hatujawahi kutoa Waalimu wengi namna hii kwa mwaka mmoja Tanzania toka tupate Uhuru. Hilo ni jambo la kujivunia.

Swali; Ulitaka hao waliofeli wapitishwe tu hata kama hawakumudu?
 
Vipaumbele vya serikali ya DHAIFU. Kwanza, ni kushinda chaguzi kwa gharama yeyote sio elimu kwa gharama yeyote. Mbili, ni kuishughulikia CDM kwa gharama yeyote. Tatu, kuzima maandamano ya wanaharakati kwa gharama yeyote. Nne, Kuleta macelebrity wote wa duniani kwa gharama yeyote. Tano, kusafiri nje nchi zote kwa gharama yeyote. Sita, kuwawezesha wang'oaji mene na kucha, watesaji, wapigaji kwa gharama yeyote. Saba, kupeleka majeshi kupigana Dafur, DRC, Comoro na kwingineko kwa gharama yeyote. Nane, kuwezesha wasanii wa kibongo kwa gharama yeyote. Ongeza vipaumbele vingine vya serikali DHAIFU. Sasa basi katika vipaumbele hivi unategemea kuvuna nini katika elimu, afya n.k. Zingatia serikali dhaifu inavyotumia dola kudhibiti walimu na madaktari wanapodai haki zao. Tukubali tu tulikosea kuchagua majanga. Sasa tujipange tusirudie tena makosa ya kuchagua MAJANGA.
 
Hata serikali ije na kauli nyingi kiasi gani mfan BIG RESULT NOW, bila kuwa na nia ya dhati , iikiwa ni pamoja na kushughulikia matatizo ya WAKUFUNZI wa vyuo vya ualimu , elimu itazidi kushuka.

Uzembe wa serikali kutokushughulikia matatizo ya wakufunzi kama vile kutokuwapandisha madaraja( vyeo) kumesababisha kada hii kukata tamaa. Wakufunzi wapo bize na mambo binafsi kuliko kufundisha.

BIG RESULT NOW ndio kitu gani?!! JK inabidi ajue BIG RESULT NOW without big salary is a BIG PROBLEM NOW! Chezea walimu wewe?!
 
Walimu waliochaguliwa kwenda kifundisha upe siku hizi ni madokta na maprofesa. Wengine waliobaki wamejiendeleza sana. Walikuwa waajjlikana kama B/C. Huwezi kulinganisha Drs. 7 la wakati ule hata na F4 ya sasa. Wale walimudu kazi zao. Lakini sasa wanafunzi hawafunfishwi ili waelewe bali ili wafaulu mitihani. Sasa hata wao wamechoka liwalo na liwe. Unategemea nini from wrongly standardised marks? Not much of course. Bila shaka hali itakuwa mbaya zaidi mwakani. Pathetic.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

bavicha wanachekesha sana. eti walimu wa UPE wamekuwa maprofesa. Hakuna hata jina la mwalimu mmoja wa UPE ambaye leo hii amekuwa profesa. Waingereza wanasema "if wishes were horses, beggers would ride".
 
Kama mtendaji mkuu wa serikali amechoka kufanya kazi kwa nini walimu wasichoke kufundisha na wanafunzi kuchoka kusoma? Kila mtu amechoka isipokuwa polisi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Kupiga raha hata mie nisingechoka:love:
 
TUME - PINDA haya deal nyingine iyo tena ya kuchakachua matokeo

mix with yours
 
Kama kuna watu wenye data za elimu watusaidie...
Tuna shule ngapi kwa sasa Tz (Primary/Secondary), uhitaji wa walimu ukoje, na kwa kiwango cha sasa cha wahitimu wasiozidi 6000 kwa mwaka, Ni miaka mingapi inahitajika kucover gap la walimu wa astashahada na stashahada?...
 
Mleta mada unashangaza kuliita hilo kuwa ni janga.

Mimi naona hapo mambo ni mazuri kabisa, tumepata Waalimu wapya waliofaulu zaid ya 6,000

1) Hatujawahi kutoa Waalimu wengi namna hii kwa mwaka mmoja Tanzania toka tupate Uhuru. Hilo ni jambo la kujivunia.

Swali; Ulitaka hao waliofeli wapitishwe tu hata kama hawakumudu?

Inawezekana... Lakini pia inawezekana hatjawahi kuwa na shule nyingi kama tulizo nazo sasa toka uhuru, hatujawahi kuwa na mahitaji makubwa ya walimu kama tuliyo nayo sasa toka uhuru, hatujawahi kuwa na wanafunzi wengi mashuleni kama tulio nao sasa toka uhuru, lakini pia pengine hatujawahi kuwa na raslimali nyingi za kuwekeza kwenye elimu kama tulizo nazo sasa toka uhuru...

Ni bora tukajadili kwa proportions, kuliko plain numbers...
 
ualimu si imekua fani ya kupeleka watu waliofeli kila mahalai basi ndugu wanajichanga wanaenda kuhonga ndugu yao aende ualimu kana kwamba ndio fani ya watu wajinga iliyobaki matokeo yake ndio haya!!! na system nzima ndio iko ivyo kwani hakuna anayefaulu anaenda ualimu!!!
 
safi sana necta..
Tunahitaji walimu wenye AKILI.
 
Inawezekana... Lakini pia inawezekana hatjawahi kuwa na shule nyingi kama tulizo nazo sasa toka uhuru, hatujawahi kuwa na mahitaji makubwa ya walimu kama tuliyo nayo sasa toka uhuru, hatujawahi kuwa na wanafunzi wengi mashuleni kama tulio nao sasa toka uhuru, lakini pia pengine hatujawahi kuwa na raslimali nyingi za kuwekeza kwenye elimu kama tulizo nazo sasa toka uhuru...

Ni bora tukajadili kwa proportions, kuliko plain numbers...

Hayo yote uliyosema ndivyo ilivyo. Jee mlitaka wapasishwe hata vilaza kama ilivyokuwa hapo awali? mradi ni nanihii basi kapitishwa tu.

Hii itawafanya makanjanja warudi kupiga kitabu.

Kikwete anafanya kweli. Waalimu zaidi ya 6,000 na hao ni vyuo vya Waalimi tu. mbali walipo vyuo vikuu.

Hongera Kikwete, tunaona na tunakusifu unafanya kweli.
 
Mbona wamefaulu hawa,mnakumbuka sifa za kusomea diploma ya ualimu si principal 2 kama zamani siku hizi principle moja na subsiary.sasa kama ndo hivyo mnataka wafaulu kwa kiwango gani zaidi ya sifa walizoingilia vyuoni.
 
Mleta mada unashangaza kuliita hilo kuwa ni janga.

Mimi naona hapo mambo ni mazuri kabisa, tumepata Waalimu wapya waliofaulu zaid ya 6,000

1) Hatujawahi kutoa Waalimu wengi namna hii kwa mwaka mmoja Tanzania toka tupate Uhuru. Hilo ni jambo la kujivunia.

Swali; Ulitaka hao waliofeli wapitishwe tu hata kama hawakumudu?

Janga ni kwamba walimu zaidi ya 500 wamefeli na wengine 2900 wanatakiwa kurudia mtihani. Kodi za wananchi zimetumika bila kufikia malengo. Tujiulize kwa nini wamefeli?
 
Back
Top Bottom