Janga lingine sekta ya Elimu: Walimu wafeli Mtihani

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
headline_bullet.jpg
Hakuna daraja la kwanza kwa vyuo vyote
headline_bullet.jpg
Watalazimika kurudia mtihani kufikia viwango

Wakati serikali ikisuasua kutoa ripoti ya tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyokuwa ikichunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, matokeo ya mtihani wa ualimu ya mwaka huu nayo ni janga.

Katika matokeo ya mtihani wa ualimu waliofanya Mei mwaka huu ambayo yametolewa jana na Baraza la Mtihani la Taifa (Necta), wahitimu 2,906 wa ngazi ya stashahada wanatakiwa kurudia mitihani (supplementary) ndani ya miaka miwili huku wengine 533 wakiwa wamefeli kwa daraja la 0.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa kwenye tovuti ya Necta na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini, yanaonyesha kwamba hakuna kabisa mhitimu aliyefaulu kwa kiwango cha juu (distinction), 27 wamefaulu kwa daraja pili (credit) na waliofaulu kwa daraja tatu (pass) ni 6,374.

Madaraja ya mitihani huo yamepangwa kwa distinction (sawa na daraja la kwanza), credit (sawa na daraja la pili), pass (sawa na daraja la tatu), supplementary (kurudia baadhi ya masomo) na fail (daraja sifuri)Jumla ya vyuo 139 vilifanya mtihani huo, kati yake vya astashahada ni 90 na stashahada ni 49.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo kama Mpwapwa yenye wahitimu 442 ni mhitimu mmoja tu aliyepata daraja pili yaani credit wakati waliofaulu kwa daraja tatu yaani pass ni 295, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 136 na waliofeli ni tisa.

Chuo cha Marangu chenye wahitimu 1,026 daraja pili ni 7, la tatu ni 630, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 343 wakati waliopata daraja 0 ni 38. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba chuo cha Monduli waliopata daraja pili ni 9, la tatu ni 295, wanaorudia ni 66 na 0 ni wawili.

Chuo cha Korogwe kati ya wahitimu 1,080 matokeo yanaonyesha kwamba hakuna waliopata daraja la pili, la tatu ni 655, wanaorudia ni 328 na 0 ni 77 wakati Eckenforde hakuna pia aliyepata daraja la pili, wakati daraja la tatu 51, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo vya Arusha, Mtwara, Benjamin Mkapa, Dakawa, Butimba, Chuo cha Ualimu Zanzibar, Pemba Islamic na Bukoba Lutheran hakuna waliopata daraja pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Pemba Islamic waliopata daraja la tatu ni wanne, wanaorudia ni 29 na 0 ni 19; wakati Chuo cha Ualimu Zanzibar daraja la tatu ni sita, wanaorudia ni 31 na 0 ni 16 wakati Bukoba Lutheran daraja la tatu ni 12, wanaorudia ni wanne na waliopata 0 ni watatu.

Dakawa waliofaulu kwa daraja la tatu ni 352, wanaorudia ni 124 na 0 ni 24; Mtwara daraja la tatu ni 304, wanaorudia ni 145 na 0 ni 27; Benjamin Mkapa daraja la tatu ni watano, wanaorudia ni saba na 0 ni wawili; Arusha daraja la tatu ni 14, wanaorudia ni wanane na 0 ni saba wakati Butimba daraja la tatu ni 497, wanaorudia ni 283 na 0 ni 18.

Klerruu wahitimu 227 waliofaulu kwa daraja pili ni wawili, daraja la tatu ni 175, wanaorudia ni 39 na 0 ni saba; Patandi la pili ni mmoja, daraja la tatu ni 60, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16; Bunda hakuna hata mmoja aliyepata C, wakati daraja la tatu ni 313, wanaorudia ni 159 na 0 ni 23 wakati Morogoro mmoja amefaulu kwa daraja pili, 665 wamefaulu kwa daraja la tatu ni 274 wanarudia na 49 wanamepata 0.

Tukuyu hakuna daraja la pili na 445 wamepata daraja la tatu, 107 wanarudia wakati 12 wamepata 0. Kasulu hakuna daraja la pili, 204 wamepata daraja la tatu, wanaorudia ni 77 na 0 ni 14 wakati St. Mary's hakuna waliopata daraja la pili wala wanaorudia, daraja la tatu ni watano na 0 ni mmoja.

Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa katika vyuo vyote kwa ngazi ya cheti (Grade A) yaani astashahada, wahitimu 5,608 wamefaulu kwa daraja pili wakati waliopata daraja la tatu ni 17,339. Pia wapo 207 waliopata 0.

Matokeo yaliyopo kwenye tovuti hiyo ni ya jumla ya vyuo 86 vya ngazi ya astashahada ya ualimu, elimu maalum vinne, stashahada (diploma) ya ualimu vyuo 48 na kimoja cha ufundi.

SOURCE: NIPASHE

Kama hali hii ikiachiwa iendelee tunaelekea kubaya zaidi. Kama walimu wanafeli kwa kiasi hicho itakuwaje wanafunzi wa sekondari ambao bado ni watoto? Serikali ya JMT inayoundwa na CCM imeshindwa kazi? JK rais msikivu, embu sikiliza wananchi wako kwa kumwondoa Kawambwa katika wizara hiyo. Weka mtu makini kama Magufuli au Mwakyembe vinginevyo wananchi tunaangamia kwa kupata elimu duni.
 
Halafu magamba bado hawataki kuachia ngazi
 
Wapo kwa ajili ya kuchumia matumbo yao badala ya kutumikia wenye nchi. Watoto wao wanasomo shule bora kwa mamilioni ya walalahoi. Watanzania tusivumilie hali; INATOSHA TUCHUKUE HATUA YA KUIKATAA CCM KAMA TUNAVYOKATAA MAGONJWA NA MAJANGA. CCM NI JANGA
 
Mode hii mada peleka jukwaa husika

Apeleke jukwaa lipi gamba? Mada hii inahusu siasa; siasa mbovu ya CCM ndio imepelekea matokeo haya mabovu ya elimu. Mod naomba usihamishe uzi huu
 
headline_bullet.jpg
Hakuna daraja la kwanza kwa vyuo vyote
headline_bullet.jpg
Watalazimika kurudia mtihani kufikia viwango

Wakati serikali ikisuasua kutoa ripoti ya tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyokuwa ikichunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, matokeo ya mtihani wa ualimu ya mwaka huu nayo ni janga.

Katika matokeo ya mtihani wa ualimu waliofanya Mei mwaka huu ambayo yametolewa jana na Baraza la Mtihani la Taifa (Necta), wahitimu 2,906 wa ngazi ya stashahada wanatakiwa kurudia mitihani (supplementary) ndani ya miaka miwili huku wengine 533 wakiwa wamefeli kwa daraja la 0.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa kwenye tovuti ya Necta na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini, yanaonyesha kwamba hakuna kabisa mhitimu aliyefaulu kwa kiwango cha juu (distinction), 27 wamefaulu kwa daraja pili (credit) na waliofaulu kwa daraja tatu (pass) ni 6,374.

Madaraja ya mitihani huo yamepangwa kwa distinction (sawa na daraja la kwanza), credit (sawa na daraja la pili), pass (sawa na daraja la tatu), supplementary (kurudia baadhi ya masomo) na fail (daraja sifuri)Jumla ya vyuo 139 vilifanya mtihani huo, kati yake vya astashahada ni 90 na stashahada ni 49.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo kama Mpwapwa yenye wahitimu 442 ni mhitimu mmoja tu aliyepata daraja pili yaani credit wakati waliofaulu kwa daraja tatu yaani pass ni 295, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 136 na waliofeli ni tisa.

Chuo cha Marangu chenye wahitimu 1,026 daraja pili ni 7, la tatu ni 630, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 343 wakati waliopata daraja 0 ni 38. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba chuo cha Monduli waliopata daraja pili ni 9, la tatu ni 295, wanaorudia ni 66 na 0 ni wawili.

Chuo cha Korogwe kati ya wahitimu 1,080 matokeo yanaonyesha kwamba hakuna waliopata daraja la pili, la tatu ni 655, wanaorudia ni 328 na 0 ni 77 wakati Eckenforde hakuna pia aliyepata daraja la pili, wakati daraja la tatu 51, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo vya Arusha, Mtwara, Benjamin Mkapa, Dakawa, Butimba, Chuo cha Ualimu Zanzibar, Pemba Islamic na Bukoba Lutheran hakuna waliopata daraja pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Pemba Islamic waliopata daraja la tatu ni wanne, wanaorudia ni 29 na 0 ni 19; wakati Chuo cha Ualimu Zanzibar daraja la tatu ni sita, wanaorudia ni 31 na 0 ni 16 wakati Bukoba Lutheran daraja la tatu ni 12, wanaorudia ni wanne na waliopata 0 ni watatu.

Dakawa waliofaulu kwa daraja la tatu ni 352, wanaorudia ni 124 na 0 ni 24; Mtwara daraja la tatu ni 304, wanaorudia ni 145 na 0 ni 27; Benjamin Mkapa daraja la tatu ni watano, wanaorudia ni saba na 0 ni wawili; Arusha daraja la tatu ni 14, wanaorudia ni wanane na 0 ni saba wakati Butimba daraja la tatu ni 497, wanaorudia ni 283 na 0 ni 18.

Klerruu wahitimu 227 waliofaulu kwa daraja pili ni wawili, daraja la tatu ni 175, wanaorudia ni 39 na 0 ni saba; Patandi la pili ni mmoja, daraja la tatu ni 60, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16; Bunda hakuna hata mmoja aliyepata C, wakati daraja la tatu ni 313, wanaorudia ni 159 na 0 ni 23 wakati Morogoro mmoja amefaulu kwa daraja pili, 665 wamefaulu kwa daraja la tatu ni 274 wanarudia na 49 wanamepata 0.

Tukuyu hakuna daraja la pili na 445 wamepata daraja la tatu, 107 wanarudia wakati 12 wamepata 0. Kasulu hakuna daraja la pili, 204 wamepata daraja la tatu, wanaorudia ni 77 na 0 ni 14 wakati St. Mary’s hakuna waliopata daraja la pili wala wanaorudia, daraja la tatu ni watano na 0 ni mmoja.

Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa katika vyuo vyote kwa ngazi ya cheti (Grade A) yaani astashahada, wahitimu 5,608 wamefaulu kwa daraja pili wakati waliopata daraja la tatu ni 17,339. Pia wapo 207 waliopata 0.

Matokeo yaliyopo kwenye tovuti hiyo ni ya jumla ya vyuo 86 vya ngazi ya astashahada ya ualimu, elimu maalum vinne, stashahada (diploma) ya ualimu vyuo 48 na kimoja cha ufundi.

SOURCE: NIPASHE

Kama hali hii ikiachiwa iendelee tunaelekea kubaya zaidi. Kama walimu wanafeli kwa kiasi hicho itakuwaje wanafunzi wa sekondari ambao bado ni watoto? Serikali ya JMT inayoundwa na CCM imeshindwa kazi? JK rais msikivu, embu sikiliza wananchi wako kwa kumwondoa Kawambwa katika wizara hiyo. Weka mtu makini kama Magufuli au Mwakyembe vinginevyo wananchi tunaangamia kwa kupata elimu duni.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni rais aliyefaninkiwa sana kati ya marais wote waliopita wa JMT. Maendeleo kila mahali!! By FaizaFoxy
 
kila kona majanga watu wanalalamika inabidi kwenye katiba mpya tuunde kipengele cha ulalamishi bila kuchukua hatua thabiti.
 
poleni walimu tarajali ambao matokeo haya yanawahusu, ushauri ni kuendelea kujielimisha kwa ambao mmebahatika kuwa walimu; na hata wale ambao wanarudia mitihani wafanye maandalizi mazuri. waliopata daraja 0 nao wasikate tamaa, wajaribu mambo mengine, maisha yanaendelea, sio lazima uwe mwalimu tu!

hata hivyo pengine mtaala unatakiwa kuangaliwa upya, mambo ya kutungiwa mtihani kwa kufuata tu syllabus bila kuzingatia kama walimu wamesambaa ktk vyuo vyote kwa uwiano sawa au la hayafai! kama vyuo vina walimu tunaowaamini; tuwaache watunge mitihani kwa wanafunzi wao kulingana na pale walipofundisha
 
Duuuuuh Khali Mbaya Jamani! Hata Hao Waliopata Daraja La 2 & 3 Ni Vilaza Vile Vile.....
 
headline_bullet.jpg
Hakuna daraja la kwanza kwa vyuo vyote
headline_bullet.jpg
Watalazimika kurudia mtihani kufikia viwango

Wakati serikali ikisuasua kutoa ripoti ya tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, iliyokuwa ikichunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka jana, matokeo ya mtihani wa ualimu ya mwaka huu nayo ni janga.

Katika matokeo ya mtihani wa ualimu waliofanya Mei mwaka huu ambayo yametolewa jana na Baraza la Mtihani la Taifa (Necta), wahitimu 2,906 wa ngazi ya stashahada wanatakiwa kurudia mitihani (supplementary) ndani ya miaka miwili huku wengine 533 wakiwa wamefeli kwa daraja la 0.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa kwenye tovuti ya Necta na kusambazwa kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini, yanaonyesha kwamba hakuna kabisa mhitimu aliyefaulu kwa kiwango cha juu (distinction), 27 wamefaulu kwa daraja pili (credit) na waliofaulu kwa daraja tatu (pass) ni 6,374.

Madaraja ya mitihani huo yamepangwa kwa distinction (sawa na daraja la kwanza), credit (sawa na daraja la pili), pass (sawa na daraja la tatu), supplementary (kurudia baadhi ya masomo) na fail (daraja sifuri)Jumla ya vyuo 139 vilifanya mtihani huo, kati yake vya astashahada ni 90 na stashahada ni 49.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo kama Mpwapwa yenye wahitimu 442 ni mhitimu mmoja tu aliyepata daraja pili yaani credit wakati waliofaulu kwa daraja tatu yaani pass ni 295, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 136 na waliofeli ni tisa.

Chuo cha Marangu chenye wahitimu 1,026 daraja pili ni 7, la tatu ni 630, wanaotakiwa kurudia mitihani ni 343 wakati waliopata daraja 0 ni 38. Matokeo hayo yanaonyesha kwamba chuo cha Monduli waliopata daraja pili ni 9, la tatu ni 295, wanaorudia ni 66 na 0 ni wawili.

Chuo cha Korogwe kati ya wahitimu 1,080 matokeo yanaonyesha kwamba hakuna waliopata daraja la pili, la tatu ni 655, wanaorudia ni 328 na 0 ni 77 wakati Eckenforde hakuna pia aliyepata daraja la pili, wakati daraja la tatu 51, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba vyuo vya Arusha, Mtwara, Benjamin Mkapa, Dakawa, Butimba, Chuo cha Ualimu Zanzibar, Pemba Islamic na Bukoba Lutheran hakuna waliopata daraja pili.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Pemba Islamic waliopata daraja la tatu ni wanne, wanaorudia ni 29 na 0 ni 19; wakati Chuo cha Ualimu Zanzibar daraja la tatu ni sita, wanaorudia ni 31 na 0 ni 16 wakati Bukoba Lutheran daraja la tatu ni 12, wanaorudia ni wanne na waliopata 0 ni watatu.

Dakawa waliofaulu kwa daraja la tatu ni 352, wanaorudia ni 124 na 0 ni 24; Mtwara daraja la tatu ni 304, wanaorudia ni 145 na 0 ni 27; Benjamin Mkapa daraja la tatu ni watano, wanaorudia ni saba na 0 ni wawili; Arusha daraja la tatu ni 14, wanaorudia ni wanane na 0 ni saba wakati Butimba daraja la tatu ni 497, wanaorudia ni 283 na 0 ni 18.

Klerruu wahitimu 227 waliofaulu kwa daraja pili ni wawili, daraja la tatu ni 175, wanaorudia ni 39 na 0 ni saba; Patandi la pili ni mmoja, daraja la tatu ni 60, wanaorudia ni 21 na 0 ni 16; Bunda hakuna hata mmoja aliyepata C, wakati daraja la tatu ni 313, wanaorudia ni 159 na 0 ni 23 wakati Morogoro mmoja amefaulu kwa daraja pili, 665 wamefaulu kwa daraja la tatu ni 274 wanarudia na 49 wanamepata 0.

Tukuyu hakuna daraja la pili na 445 wamepata daraja la tatu, 107 wanarudia wakati 12 wamepata 0. Kasulu hakuna daraja la pili, 204 wamepata daraja la tatu, wanaorudia ni 77 na 0 ni 14 wakati St. Mary’s hakuna waliopata daraja la pili wala wanaorudia, daraja la tatu ni watano na 0 ni mmoja.

Matokeo hayo pia yanaonyesha kuwa katika vyuo vyote kwa ngazi ya cheti (Grade A) yaani astashahada, wahitimu 5,608 wamefaulu kwa daraja pili wakati waliopata daraja la tatu ni 17,339. Pia wapo 207 waliopata 0.

Matokeo yaliyopo kwenye tovuti hiyo ni ya jumla ya vyuo 86 vya ngazi ya astashahada ya ualimu, elimu maalum vinne, stashahada (diploma) ya ualimu vyuo 48 na kimoja cha ufundi.

SOURCE: NIPASHE

Kama hali hii ikiachiwa iendelee tunaelekea kubaya zaidi. Kama walimu wanafeli kwa kiasi hicho itakuwaje wanafunzi wa sekondari ambao bado ni watoto? Serikali ya JMT inayoundwa na CCM imeshindwa kazi? JK rais msikivu, embu sikiliza wananchi wako kwa kumwondoa Kawambwa katika wizara hiyo. Weka mtu makini kama Magufuli au Mwakyembe vinginevyo wananchi tunaangamia kwa kupata elimu duni.

wangeyatengeneza kabla ya kuyatoa bana
 
Haya ni matokeo mazuri, yakimaanisha kwamba wengi kati ya waliokwenda kusomea ualimu hawakuwa na sifa hizo, bali walifanya hivyo kwa kukosa njia mbadala! Hata hivyo mtihani umetuchagulia wachache tu ambao wanaweza kutoa elimu stahiki. Kama ukichunguza entry qualification zao utaweza kupata jibu. Kwahiyo kwa mtazamo wangu mimi, haya ni matokeo mazuri sana kwa fani ya ualimu. Mara nyengine, watu wa hovyo hovyo hawatakua na courage ya kujiunga vyuo vya ualimu.
 
Hata serikali ije na kauli nyingi kiasi gani mfan BIG RESULT NOW, bila kuwa na nia ya dhati , iikiwa ni pamoja na kushughulikia matatizo ya WAKUFUNZI wa vyuo vya ualimu , elimu itazidi kushuka.

Uzembe wa serikali kutokushughulikia matatizo ya wakufunzi kama vile kutokuwapandisha madaraja( vyeo) kumesababisha kada hii kukata tamaa. Wakufunzi wapo bize na mambo binafsi kuliko kufundisha.
 
Wasiwasi waondoe,serikali sikivu itarudia mtihani na hii aibu itajimuvuzisha pembeni. Chezea CCM wewe!
 
Kuna jamaa yangu anafundisha kigoma amenambia jana kuna mhitimu aliyekuwa anasoma tabora...sijui chuo gani amejinyonga hadi kufa sababu ya kufeli mtihani huo wa mwisho, mtu huyo aliyejinyonga amefahamika kwa jina la 'Musa' au Moses...anazikwa kesho huko huko kigoma
 
Tutastandadaizi.

Halafu hili kwa Bongo sio tatizo kabisa
kuna kauli maalum zinaweza kutumika:-

1. Ni upepo tu JK
2. Liwalo na liwe
3. Tumechoka sasa,wapigwe tu MP

Adies amigos.
 
Tutastandadaizi.

Halafu hili kwa Bongo sio tatizo kabisa
kuna kauli maalum zinaweza kutumika:-

1. Ni upepo tu JK
2. Liwalo na liwe
3. Tumechoka sasa,wapigwe tu MP

Adies amigos.
 
Kama mtendaji mkuu wa serikali amechoka kufanya kazi kwa nini walimu wasichoke kufundisha na wanafunzi kuchoka kusoma? Kila mtu amechoka isipokuwa polisi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom