Janga la ajali za barabarani linatisha. Ardhi inakunywa damu ya wasafiri wajameni

Kuna sehemu za barabara matukio ya ajali huwa yanajirudia rudia mara nyingi
Mkuu lawama msiwe mnashushia Madereva tu TANROADS ndio wanatakiwa walaumiwe sana Ukitoka Dumila kuelekea Gairo kuna kurabati unaendelea wanaweka Mapipa Barabarani bila Ishara yoyote

Halafu wanatoa kazi kwa Wakandarasi wababaishaji unakuta Pothole imezibwa imekuwa kama kichuguu.
 
Sie kama nchi kwanini tusiweke contract Google map, magari yote yakafungwa vts, yakafungwa na software, uko very speed unakutana na mwamala wa mpesa wa faini,

Hebu tujiulize, Tata mpya kiwandani ni 35m, sisi huku unauziwa 135m? Hizi nauli za elfu mbili bado mgawane na wapiga debe na trafik,

Hili gari lina kunywa mafuta oil hydronic matairi bima spare, kote huko kuna kodi, kwanini tusitoe ruzuku yakauzwa 20m, hakuna wa kuweka michomoko barabarani
 
Hakuna Janga la njaa Tz, kuna akiba ya chakula cha kutosha, maghala ya taifa yamejaaaa chakula cha kutosha.

Ukiachila mbali wafanya biashara wakubwa wa tz wana akiba ya kutosha kwenye maghala ya kuweza kulisha nchi miaka 2 mfululizo, sasa hapo njaa inapitia wapi?!

kuna wahuni wachache ambao wana lengo la kuzua taharuki na kusababisha hofu kwa wananchi na kusababisha wafanya biashara kupandisha nafaka kwa lengo la kujinufaisha.
 
Hizo nchi unazoona zina takwimu ndogo za ajali ni kwa sababu kadhaa...

1. Miundombinu mizuri na ya kisasa ya barabara.

2. Sheria kali ikiwemo ya ulazima wa magari kuwa na mandatory service ya muda fulani.

3. Ufahamu na utashi wa watu wao juu ya mambo ya kawaida ikiwemo usalama wao barabarani (Waafrika wengi tuna ulemavu wa akili, huwa tunafanya mambo yetu mengi pasipo kujali matokeo, angalia tu hata uchafu mitaani, utunzaji wa mali za umma, ufisadi n.k)

4. Uwepo wa usafiri mbadala kwa wingi kama treni na ndege.
Umemaliza kila kitu. Hali tuliyofikia ni mbaya sana sana. Tumefika hapa kwa sababu ya watawala kulea uzembe na kutowajibika kwa muda mrefu. Na ili hali ibadilike, tunahitaji uongozi wenye fikra mpya. Inatakiwa tujaribu kutatua matatizo yote yanayoletwa na sababu ulizoorodhesha. Pa kuanzia ni ni kwenye mindset zetu madereva na watumiaji wa barabara pamoja na miundombinu.
 
Mara ngapi umewahi kusikia ajali za magari Marekani zinazoua watu 10 au 20 kwa mpigo?
Kuna TV kabisa inayofuatilia na kutangaza Ajali.

Amerika kila siku Watu takriban 200 wanakufa kwenye Ajali za Barabarani.
 
Watu 200 ni wachache sana kwenye taifa la watu milioni 330. Hapa Tanzania unaweza kukuta wanakufa kiasi hicho au zaidi ya hao kwa siku ila hatuna hata TV au chombo cha habari mahususi kufuatilia.
Kuna TV kabisa inayofuatilia na kutangaza Ajali.

Amerika kila siku Watu takriban 200 wanakufa kwenye Ajali za Barabarani.
 
Watu 200 ni wachache sana kwenye taifa la watu milioni 330. Hapa Tanzania unaweza kukuta wanakufa kiasi hicho au zaidi ya hao kwa siku ila hatuna hata TV au chombo cha habari mahususi kufuatilia.
Mimi nilikuwa Dereva wa Lori na bado siku hizi huwa nawasaidia jamaa wanaoumwa Madereva wanahusika kwa asilimia ndogo tu Authorities ndio wanahusika kwa kiasi kikubwa

Unakuta Traffic Police anayasimamisha magari kwenye blind corner ajali ikitokea ajali anapotea wanakuja wenzake kupima ajali na kutafuta Rushwa.
 
Watu wanakufa, wengi wanabaki vilema, watoto wanabaki yatima kwa ajali za barabarani ambazo zimekuwa nyingi sana kwenye nchi hii.

Ni kama vile watu wamekuwa sugu kwa hizi ajali sasa. Katika nchi zilizoendelea ikitokea watu 20 au 10 wamekufa mara 2 au 3 ndani ya mwaka mmoja kwa mpigo kwa chanzo kile kile kimoja basi Rais, wabunge, wanaharakati lazima wajitokeze na hata maandamano makubwa kutaka uwajibikaji. Hapa kwetu salamu za rambirambi tu zitatumwa na itakuwa kama siku kama siku nyingine baada ya ajali iliyoua watu 15 au 20.

Haya mambo matatu angalau tuanze nayo:

1. Iundwe WIZARA ya Usalama wa raia kusimamia polisi na kazi zao. Kuwachanganya polisi na RITA, uhamiaji, magereza, vitambulisho n.k kunafifisha sana usimamizi wa utendaji wao.

2. Iundwe mamlaka ya usimamizi na usalama BARABARANI inayojitegemea kwa ajili ya kupendekeza sera na sheria, kuweka miongozo na kushirikiana na polisi kusimamia leseni za wasafirashaji barabarani.

3. Mawaziri wa uchukuzi na mambo ya ndani kwa sasa wawajibishwe mpaka hayo mawili hapo juu yatakapofanyiwa kazi. Hawa mawaziri wawili kama hawawezi kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu kutatua janga la ajali basi hawafai, hawatoshi na hivyo waondolewe haraka na wakija wengine wakishimdwa nao waondolewe pia.

Maisha yetu raia yanahitaji kupewa uthamani stahiki na wale wanaolipwa kwa kodi zetu kwa kazi hiyo kuhakikisha yanakuwa salama muda wote.
Ajali zinaua Watanzania wengi kuliko HIv. Very sad indeed.
 
Hizo nchi unazoona zina takwimu ndogo za ajali ni kwa sababu kadhaa...

1. Miundombinu mizuri na ya kisasa ya barabara.

2. Sheria kali ikiwemo ya ulazima wa magari kuwa na mandatory service ya muda fulani.

3. Ufahamu na utashi wa watu wao juu ya mambo ya kawaida ikiwemo usalama wao barabarani (Waafrika wengi tuna ulemavu wa akili, huwa tunafanya mambo yetu mengi pasipo kujali matokeo, angalia tu hata uchafu mitaani, utunzaji wa mali za umma, ufisadi n.k)

4. Uwepo wa usafiri mbadala kwa wingi kama treni na ndege.

Magari mengi yanatembea barabarani ila ni mabovu service za kuunga unga tu.

Mfano hii Dar express inafanya safari za mikoani nadhani Dar-Arusha au Dar-Rombo, hii picha ya leo kabla hata haijatoka nje ya Dar, saa 12 asubuhi napita mitaa ya mwenge naona kuna mtu yuko chini pale kama anarekebisha kitu sasa kwa service za aina hii katikati ya barabara lazma kutokee ya kutokea huko njiani.
20220726_062253.jpg
 
Back
Top Bottom