Janga la ajali za barabarani linatisha. Ardhi inakunywa damu ya wasafiri wajameni

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
26,278
27,518
Watu wanakufa, wengi wanabaki vilema, watoto wanabaki yatima kwa ajali za barabarani ambazo zimekuwa nyingi sana kwenye nchi hii.

Ni kama vile watu wamekuwa sugu kwa hizi ajali sasa. Katika nchi zilizoendelea ikitokea watu 20 au 10 wamekufa mara 2 au 3 ndani ya mwaka mmoja kwa mpigo kwa chanzo kile kile kimoja basi Rais, wabunge, wanaharakati lazima wajitokeze na hata maandamano makubwa kutaka uwajibikaji. Hapa kwetu salamu za rambirambi tu zitatumwa na itakuwa kama siku kama siku nyingine baada ya ajali iliyoua watu 15 au 20.

Haya mambo matatu angalau tuanze nayo:

1. Iundwe WIZARA ya Usalama wa raia kusimamia polisi na kazi zao. Kuwachanganya polisi na RITA, uhamiaji, magereza, vitambulisho n.k kunafifisha sana usimamizi wa utendaji wao.

2. Iundwe mamlaka ya usimamizi na usalama BARABARANI inayojitegemea kwa ajili ya kupendekeza sera na sheria, kuweka miongozo na kushirikiana na polisi kusimamia leseni za wasafirashaji barabarani.

3. Mawaziri wa uchukuzi na mambo ya ndani kwa sasa wawajibishwe mpaka hayo mawili hapo juu yatakapofanyiwa kazi. Hawa mawaziri wawili kama hawawezi kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu kutatua janga la ajali basi hawafai, hawatoshi na hivyo waondolewe haraka na wakija wengine wakishimdwa nao waondolewe pia.

Maisha yetu raia yanahitaji kupewa uthamani stahiki na wale wanaolipwa kwa kodi zetu kwa kazi hiyo kuhakikisha yanakuwa salama muda wote.
 
HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
54,094
62,220
Tatizo ni barabara vinyu, siku hizi magari mengi mapya...

Barabara zimechimbwa na kuachwa hivo hivo
 
0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
4,083
10,222
Hizi ni ķafara za watawala,acheni kujifanya kama hamjui

Kuna matukio mengi sana ya kuuwana pia usiishie kusema vifo vya ajari tu
 
Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
63,666
72,839
Hizo nchi unazoona zina takwimu ndogo za ajali ni kwa sababu kadhaa...

1. Miundombinu mizuri na ya kisasa ya barabara.

2. Sheria kali ikiwemo ya ulazima wa magari kuwa na mandatory service ya muda fulani.

3. Ufahamu na utashi wa watu wao juu ya mambo ya kawaida ikiwemo usalama wao barabarani (Waafrika wengi tuna ulemavu wa akili, huwa tunafanya mambo yetu mengi pasipo kujali matokeo, angalia tu hata uchafu mitaani, utunzaji wa mali za umma, ufisadi n.k)

4. Uwepo wa usafiri mbadala kwa wingi kama treni na ndege.
 
Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
49,175
63,309
Unavyozidi kuboresha mindombinu na magari nayo yanaongezeka na baadhi ya madereva wanajisahau mara wengine waendeshe vyombo vibovu, yaani vurugu vurugu

Mungu atuepushe na hili janga linaondoka na raia wengi sana
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
5,133
11,863
Ajali SIO kazi ya Mungu it's someone Fault, barabara zetu bado sana tena sana,alama za usalama barabarani almost hakuna kabisa,hii T1 alama zake hazionekani kabisa hasa usiku, vibao vya umbali kati ya miji hakuna kabisa, ufinyu wake na magari mengi hayana sifa ya kuwa barabarani, trunks nyingi hazina kabisa tailing lights, pls waziri wangu wa mawasiliano fanya road trips ndani ya Zambia, Botswana na Namibia (usifike SA maana utaruka kichaa)angalia wenzetu walivyojenga hizi freeways zao.
 
Mtoto wa Shule

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
9,646
6,552
Watu wanakufa, wengi wanabaki vilema, watoto wanabaki yatima kwa ajali za barabarani ambazo zimekuwa nyingi sana kwenye nchi hii.

Ni kama vile watu wamekuwa sugu kwa hizi ajali sasa. Katika nchi zilizoendelea ikitokea watu 20 au 10 wamekufa mara 2 au 3 ndani ya mwaka mmoja kwa mpigo kwa chanzo kile kile kimoja basi Rais, wabunge, wanaharakati lazima wajitokeze na hata maandamano makubwa kutaka uwajibikaji. Hapa kwetu salamu za rambirambi tu zitatumwa na itakuwa kama siku kama siku nyingine baada ya ajali iliyoua watu 15 au 20.

Haya mambo matatu angalau tuanze nayo.

1. Iundwe WIZARA ya Usalama wa raia kusimamia polisi na kazi zao. Kuwachanganya polisi na RITA, uhamiaji, magereza, vitambulisho n.k kunafifisha sana usimamizi wa utendaji wao.

2. Iundwe mamlaka ya usimamizi na usalama BARABARANI inayojitegemea kwa ajili ya kupendekeza sera na sheria, kuweka miongozo na kushirikiana na polisi kusimamia leseni za wasafirashaji barabarani.

3.Mawaziri wa uchukuzi na mambo ya ndani kwa sasa wawajibishwe mpaka hayo mawili hapo juu yatakapofanyiwa kazi. Hawa mawaziri wawili kama hawawezi kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu kutatua janga la ajali basi hawafai, hawatoshi na hivyo waondolewe haraka na wakija wengine wakishimdwa nao waondolewe pia.

Maisha yetu raia yanahitaji kupewa uthamani stahiki na wale wanaolipwa kwa kodi zetu kwa kazi hiyo kuhakikisha yanakuwa salama muda wote.
Ndio dhana ya kufungua nchi. Ina apply kotekote. Enzi za Chuma ajali ziliishaanza kuwa historia. Sasa tunafungua nchi. Yaliyokuwa yamezuiliwa sasa yanarudi.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
26,278
27,518
Hilo la miondombinu ni tatizo la msingi ila hatuwezi kusubiria hiyo miondombinu ambayo ina weza kuja miaka 50 mbeleni huku watu wakipukutika na kubaki vilema kimya kimya tu.
Serikali ijenge miundombimu bora kwanza ndio hayo mengine yatasaidia
Barabara kama chakinze mlandizi , unatakiwa ushangae kwa nini ajali hazitokei kila siku , si kwa nini zinatokea
 
shamimuodd

JF-Expert Member
Jan 28, 2019
880
1,379
Watu wanakufa, wengi wanabaki vilema, watoto wanabaki yatima kwa ajali za barabarani ambazo zimekuwa nyingi sana kwenye nchi hii.

Ni kama vile watu wamekuwa sugu kwa hizi ajali sasa. Katika nchi zilizoendelea ikitokea watu 20 au 10 wamekufa mara 2 au 3 ndani ya mwaka mmoja kwa mpigo kwa chanzo kile kile kimoja basi Rais, wabunge, wanaharakati lazima wajitokeze na hata maandamano makubwa kutaka uwajibikaji. Hapa kwetu salamu za rambirambi tu zitatumwa na itakuwa kama siku kama siku nyingine baada ya ajali iliyoua watu 15 au 20.

Haya mambo matatu angalau tuanze nayo.

1. Iundwe WIZARA ya Usalama wa raia kusimamia polisi na kazi zao. Kuwachanganya polisi na RITA, uhamiaji, magereza, vitambulisho n.k kunafifisha sana usimamizi wa utendaji wao.

2. Iundwe mamlaka ya usimamizi na usalama BARABARANI inayojitegemea kwa ajili ya kupendekeza sera na sheria, kuweka miongozo na kushirikiana na polisi kusimamia leseni za wasafirashaji barabarani.

3.Mawaziri wa uchukuzi na mambo ya ndani kwa sasa wawajibishwe mpaka hayo mawili hapo juu yatakapofanyiwa kazi. Hawa mawaziri wawili kama hawawezi kuja na mikakati ya muda mfupi na mrefu kutatua janga la ajali basi hawafai, hawatoshi na hivyo waondolewe haraka na wakija wengine wakishimdwa nao waondolewe pia.

Maisha yetu raia yanahitaji kupewa uthamani stahiki na wale wanaolipwa kwa kodi zetu kwa kazi hiyo kuhakikisha yanakuwa salama muda wote.
Mfano lile kontena lililomdondokea the late Professor Ngowi, yaani just a container linaua msomi, ni aibu sana
 
Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,656
2,090
Tatizo sio miundo mbinu wala nini kwanini zamani kulikuwa hakuna barabara nzuri kama hizi leo ila ajari hazikuwa kama sasa, Tatizo ni ulimbukeni wa vyombo vya usafiri wengine mafunzo duni then wanajifanya madereva konk lakini pia abiria kutokemea miendo kasi ya madereva wao! watu wapewe elimu sana la sivyo ardhi iendelee kunywa tu!
 
7 Reactions
Reply
Top Bottom