Jane "Mkenya" na nyumba zao 50

JANE MKENYA NA NYUMBA ZAO

Mwaka 2008 nilikutanishwa na Dada Mmoja MKENYA, akiwa na shida na documents flani kwa ajili ya mradi wake. Tulikutana Steers, Mtaa wa Samora na Ohio.

Document aliyonitajia ilikuwa ndo mara yangu ya kwanza kuisikia. Nikamuomba anifafanulie.

Akaniambia Mumewe ni Mtanzania, yuko na Business Partners wake wako Dubai, wanataka kumtumia shehena kubwa ya Mafuta. Ili hiyo shehena iweze kuletwa Kuna hizo documents inabidi zipatikane.

Baada ya mazungumzo ya muda mrefu Jane akaanza stories mtambuka. Akanieleza jinsi anavyosikitishwa na Wanaume wa Tanzania kutokuwa sharp kama ilivyo kwa Wakenya. Akanipa mfano ya watu wanaopenda kwenda kula na kunywa Rose Garden.

Kipindi hicho Rose Garden ikiwa Rose Garden. Jane anadai Wanaume wa Tanzania wanapenda kushinda Bar kuangalia mpira au kupiga soga kwa kisingizio kwamba Bar Kuna connections nyingi sana. Jane anadai hiyo ni illusion tu, sio kweli Kuna hizo connections kama Wanaume wanavyojiaminisha.

Mwisho akaniahidi kunikutanisha na Joe, mumewe ambaye ni Mtanzania walioanzia maisha UK. Japo hakuniambia usoni, alikuwa anamaanisha Joe ni exceptional Tanzanian man. Na mimi nilipata kuwa na shauku sana ya kukutana na Joe.

Siku iliyofuata nilikuwa na mzuka sana, nikajikuta nampigia tu simu Jane kumsalimia. Ukweli ni kwamba stories za Jana yake zilinitia machungu, nikafanya tathmini Washkaji zangu wote, nikapekua namba zote za simu nilizonazo..

Sikuona connection yoyote ya maana kama alivyonichallenge Jane. Labda kwa sababu ilikuwa ndo kwanza nina miaka miwili baada ya kumaliza Chuo.

Jane akaniambia ataingia mjini, akimaliza shughuli zake tukutane Steers.

Na kweli, mida ya saa 11 nikakutana tena na Jane.. Tofauti na Jana yake, siku hiyo tone yake haikuwa ikimuinua zaidi Joe, aliamua kunisifia. Akasema hajawahi kukutana na Bwana Mdogo wa Kitanzania humble na anaweza kuarticulate vitu kama mimi.

Katikati ya mazungumzo akaleta tena stories za Uingereza, akaniambia laiti ningekuwa naishi Uingereza ningekuwa mbali sana kimaisha. Ulaya tofauti na Afrika inajali sana watu smart. Akaniambia tabu ya Watanzania watakuchukulia poa.

Na mwisho akaniambia atanikutanisha na mumewe siku inayofuata.

Zilikuwa siku mbili zenye kuendesha sana kichwa changu. Maneno ya Jane yalikuwa yanarindima kwenye mawazo yangu kila saa. Shauku yangu ilikuwa kukutana na Joe.

Siku ilipofika nilikuwa nataka kupiga simu saa mbili kujua muda. Ila nilijizuia mithili ya mlimbwende anayetaka kutoka na mtu the first date.

Kabla ya Saa 6 Jane akaniambia Makutano ni saa 10, Golden Tulip Hotel. Kipindi hicho Golden Tulip ilikuwa Golden Tulip.

Kuelekea saa 10 Jane alinipigia, wakanipitia yeye na mumewe Millennium Towers. Tofauti ya Jane, Joe yeye ni mkimya sana. Baada ya utambulisho, nikaambiwa tunaenda kukutana na Wawakilishi wa Business Partners wa Joe.

Hao tukaanza safari... Kufika Golden Tulip, baada ya kama Dakika 10 wale Wawakilishi wakaja.. Nikatambulishwa kama rafiki wa Joe ambae pia nitamsaidia kuchukua notes wakati wa mazungumzo.

Nikakumbuka maneno ya Jane siku 2 nyuma juu ya connections. I felt connected for minutes. Wale wakuu wakamuelekeza Joe documents zote zinazotakiwa in a layman language hadi mimi pia nikaelewa. Kwa hiyo akishaprocess hizo, ataanza kuletwa shehena kubwa ya Mafuta. Tukatambulishwa na Wadau wengine wa Mafuta walipo Dar es Salaam. Joe akapangiwa kukutana nao Ile awe mentored.

Kipindi chote cha mazungumzo, wale Wawakilishi, wanaume wawili walikuwa wakinitreat na mimi kama sehemu ya partners wa Joe. Na mimi nikawa najitutumua kupenyeza YES NO nyingi ili my presence iwe recognized.

Joe akaulizwa apart from Mafuta ana Biashara gani mjini? Akawaleza kwamba kuna nyumba zipatazo 50 anazijenga Kigamboni...

Anahitaji kuzikodisha zikikamilika. Suala sio kujenga nyumba 50, suala ni jinsi alivyozitaja kwa urahisi hizo nyumba. Kwa moment Ile nilijiona fala sana, the best thing nilikuwa naweza ni kumtoa out Sandra, mara moja moja. Joe, mtu aliyenizidi kama miaka 3 anajenga nyumba 50.

Baada ya kikao wakanirudisha Millennium Towers wakaendelea na safari zao.

Sikuwa najua kama nilikuwa inspired au frustrated. Kila nilipokaa nilikuwa naisikia sauti ya Jane. Nausikia ujumbe wake, nawasaili watu wanaonizunguka. Nilikuwa najiona nimefeli tu. Lakini nilimshukuru sana Mungu kunikutanisha na kina Joe.

Baada ya siku 2 Jane akanitafuta tena. Niliacha kila kitu tukakutana Steers.

Mara hii hakuwa muongeaji sana.. Ni kama Mtu aliyekuwa anajaribu kusoma mawazo yangu. Akaniprovoke kidogo, akaniuliza juzi nimejifunza nini? Sikuwa na jibu la moja kwa moja.. Kwa kuwa kwa siku zote 5 tangu nikutane na Jane mawazo yangu haya kuwa straight. Nikashindwa kujibu swali lake moja kwa moja, akadakia kunisaidia. Akasema alinikutanisha na Joe makusudi ili kunipa changamoto.

Sio kwamba Joe anahitaji expertise yangu kwenye Ile Biashara kwa kuwa sikuwa nayo, ila basi tu Jane alitaka nione changamoto za maisha. Nimuone Joe kama inspiration.

Kijana wa Rika langu mwenye Biashara kubwa na connections kubwa za Kibiashara. Ni rahisi kuwa inspired kwa kuwa Joe ni Mtanzania mwenzangu. Katika kuhitimisha somo, akawaponda tena wale Jamaa wa Rose Garden.
Baada ya wiki Jane aliniaga wanakwenda Uingireza na Joe, tutawasiliana wakirudi.

Baada ya wakina Jane kuondoka, walau Sasa japo kwa taratibu niliweza kuanza kurudi kwenye maisha yangu ya kawaida kifikra. Ile hali ya kujilaumu ilipungua. Ila nikiweka nadhiri, nikiwa na hela nitataka kuwa humble kama Joe. Nisiwe na show offs za mjini na kuongea ongea sana.

Kwa kuwa Jane yuko Uingireza, na Bahati mbaya nilisahau kuchukua email yake nilijikuta nawasahua kwa urahisi. Nikajisemea wakirudi watanitafuta kwenye simu, after all mara nyingi niko Steers hawawezi kushindwa kunipata.

Miezi miwili au mitatu baadae, nikiwa Sasa nsharudi katika maisha yangu ya mazoea, nilipanda Daladala kutokea Mwenge kwenda Posta.
Nikiwa nimezama katika kusoma gazeti langu la Rai. Ghafla kufika Palm Beach, kuinua Macho namuona Joe anateremka kwenye Ile Dala Dala niliyopanda, na shati lake jeupe na panki laki. Ni kama vile nilitaka kufikicha Macho ili kuthibitisha kama yule ni Joe au sie. Kwa hakika alikuwa yeye. Tokea awali sikuwahi kuwa na namba ya Joe, so njia rahisi ilikuwa kupiga namba ya Tanzania ya Jane. Simu haikupatikana.

Nikawa Nashindwa kupata jibu, imekuwaje kwa Joe. Lakini toka siku ya kwanza Joe alijionyesha kama Mtu humble sana asiye na makuu. Yawezekana ni life style yake tu.

Baada ya kitambo kupita, nilasahau tena Habari za kina Joe na Jane.

Jumapili moja jioni, niko kituo cha Daladala Mbezi Beach Makonde, nawaona watu kwa makumi wanakuja kutoka Kanisa la Siloam (sijui kama nimepatia jina, Kanisa moja lipo Mbezi Beach Makonde)..

Waumini wawamevaa nguo nyeupe, kwa hiyo kwa kuwa wanakuja kama kundi, ni rahisi kujikuta unaangalia sana. Nikiwa bado nimewakodolea Macho, ghafla nagongana Macho na Joe, akiwa miongoni mwa Waumini, anakuja kituoni kupanda basi. Joe kuniona akanikumbuka, nikatabasamu kama Mtu anayetaka kusalimiana na Rafiki yake waliyepotezana kwa muda mrefu.

Kwa ghafla Joe akakunja uso, body language yake ilikuwa inaniblock nisimsalimie wala kuleta kujuana. Kwa haraka sana akadandia Daladala akatafuta siti upande wa barabarani kule.

Nilikuwa puzzled.

Toka siku ile, ni vigumu sana Mtu kunizuzua na nyumba 50 anazojenga
...inaendelea au
 
Shida ya kujifanya we ni m social ndio Kama hivi mnataka kupigwa na akina Jane na Joe .....

Next time kuwa uso wa mbuzi usicheke check na kima
 
Back
Top Bottom