Jana usiku nimejaribiwa na wachawi

Jana usiku nimejaribiwa na wachawi

Usiwe na hofu kaka. Anayeweza kukudhuru hawezi kukumwagia maji. Anayekumwagia maji ujue hana uwezo wa kukudhuru ndio anakuchanganya akili kwa kukufanyia vituko.
Kama wewe ni Mkristo, anza kufanya maombi kabla ya kulala. Usilale bila kuomba. Usipoomba, kitakachofuata watakutoa nje ili kukuonyesha kuwa wanaweza kukufanya lolote.
Anayekumwagia maji, ni Sawa na anayerusha mchanga juu ya Bati au kuchukua nguo zako kimiujiza. Huyu hawezi kukudhuru, anakutia hofu.
 
Mkuu pitia kwa pusher chukua puli zako nne za ganja. Usiku kabla hujalala puliza moja, amka baadae kidogo puliza jingine, baadae tena jingine.

Hakanyagi mchawi wala mwanga hapo.

Mimi niliwahi kupanga nyumba mama mwenye nyumba mchawi ukimpa kodi ya miezi sita anaanza kukuchezea ili uondoke kabla ya muda na kodi harudishi. Kabla sijahamia nilipewa hizo nyepesi nyepesi.

Nilimkomesha mpaka nikawa napitiliza kodi silipi mpaka nikaja kutolewa na serikali ya kijiji baada ya mama mchawi kukataa kuchukua pesa yangu na kudai anataka kurekebisha nyumba yake.
 
Nilipoangali muda ilikuwa ni saa 8:41 usiku. Tulimwagiwa maji tukiwa tumelala mimi na shemeji yenu na mtoto wangu wa mwaka na miezi mitatu. Maji yenyewe yalikuwa kama mtu aliyechovya mkono ndani ya maji kisha akakunguta mkono.
Sikuwa kwenye usingizi mzito, hata mama watoto naye hakuwa kalala fofofo. Basi baada ya kusikia kwa mara ya kwanza nikastuka ila nikasikilizia. Wakarudia tena kwa mara ya pili shemeji yenu akaniuliza ni nini hicho? Nikamwambia kama manyunyu hivi, kisha akawasha taa kulikuwa na bedswitch upande wake.

Tulipoangalia tukaona kuna maji kwenye miili yetu pamoja na mtoto. Nikatoka kitandani na kwenda kuangali dirishani kama kuna mtu alimwaga maji akiwa nje. Nilipoangalia sikuona dalili yoyote ya mtu kumwaga maji akiwa nje. Sikuona sehemu yoyote iliyokuwa na matone ya maji zaidi ya sisi na kitanda.

Nikatukana tusi kwa sauti kubwa ***** zenu wanga wakubwa nyie!. Mnatafuta kufirw@ kenge kasoro magamba nyie huku nikiwa na hofu kubwa. Tukajifuta ile mimaji nikafungua praise power radio nikakuta kuna maombi yanafanywa usiku huo. Sikuweza tena kulala japo nilikuwa ndani ya neti.

Sasa muda ndio huo unaenda. Usiku unakaribia na nishawatukana hawa wanga. Jana walinimwagia maji leo sijui nini kitajiri.

Cc. Mshana Jr

Repeat after me : " Innah Lilahi Wa Innah Lilahi Raajuni"
 
Wanaandaa mazingira ya kula apple
Kuna jamaa huku mtaani alifanyiwa
Ivyo ivyo kumwagiwa maji baada ya siku 3 akalawitiwa kuwa muangalifu ndugu
Duh hatari sana, Ila dawa ya mchawi ni Mungu tu, wachawi na mashetani hawana ujanja mbele ya Mwenyezi Mungu/ Allah. Muombe Mwenyezi Mungu kwa Imani kabla ya kulala na baada ya kuamka kila siku, huwezi kusumbuliwa tena na wachawi
 
Omba kabla ya kulala Mungu atakusikia na kukisaidia msiache kufanya toba maana moyo wenye dhambi uwepo wa Mungu haukai hivyo shetani atakufikia na kufanya chochote muda wowote ule autakao
 
Back
Top Bottom