JamiiForums yashinda mapingamizi yaliyowekwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG)

Tanzania ni nchi ya sheria japokuwa saa zingine kuipata haki unapopambana na serikari inataka uwe maarufu na mwenye uwezo wa kuipeleka kesi mahakama za juu usiporidhika na maamuzi ya mahakama za chini.

Wanavijiji kila siku wanaibwaga serikari kwenye kesi za ardhi; hata serikari ya Magufuli ilipewa zuio la bomoa bomoa na kuamiliwa fidia ilipwe kwa wakazi wa mabondeni wenye hati

Kama kweli bunge live ni haki ya kikatiba au kufanya mikutano ya hadhara miaka mitano mfulululizo mbona UKAWA wasianze na mahakama? Wanajua hakuna haki hizo bali wamedhamiria kujaribu kufanya fujo kama njia ya kulazimisha agenda zao.
 
Inasikitisha sana kuona udhalimu mkubwa wa Serikali hadi kwenye uhuru wetu wa kujadiliana kuhusu mustakabali wa nchi yetu unavyotaka kuminywa.

Wanachama wengi waliopitia uzi huu wanaiunga mkono Jamii Forums badala ya Serikali. Kweli Serikali imekosa mwelekeo.

Hongera sana JF kwa kupigania haki za watanzania Na kuendelea kuhifanya JF kuwa mahali salama na amini kesi ya msingi Mtashinda
 
Kwa mwendo huu wa serikali kukiuka katiba, kuvunja sheria na haki za binadamu kwa makusudi, nina hakika serikali itaziba masikio na macho na kufanya cho chote kwa manufaa ya walio madarakani!!!


Serikali hii inahitaji na inapenda whistleblowers ili ufisadi utokomee kwa hiyo tuwe na positive attitude kwa mahakama zetu. Ila AG hakuwa na sababu ya kuweka hizo PO na badala yake angepeleka marekebisho ya hivyo vifungu bungeni.
 
Hongera Jamii Forums,

Hii ni hatua kubwa. Hongera kwa wote walioshiriki kuanzisha, kufuatilia, na kugharimia ufuatiliaji wa suala hili mpaka hapa lilipofikia.

Sigfrid
 
Hahahahaha nimefurahi sana uhuru wangu wa kutoa maoni umelindwa na JF badala ya Serikali hahahahaha, sasa wekeni na akaunti hapa hapa ili tutume michango yetu hongera JF
Nilivyoelewa Mahakama imekataa mapingamizi ya serikali kuhusu kesi kukubaliwa kueendelea au la. Kesi ya msingi yenyewe bado.
 
Inatia moyo. Endeleeni hivyo hivyo. Nahisi mitandao kama JF ndo sehem pekee unaweza kutoa mawazo yako (ambayo hayavunji sheria) ukiwa huna hofu.
 
Hivyo no PO imetupiliwa mbali.lakini kesi ya msingi inaendelea!! Tusubiri final verdict kwa sasa bado hakuna mshindi
Unajua kama hayo mapingamizi yangekubaliwa na mahakama yangeweza kuathiri kesi ya msingi na labda kesi yenyewe ingeondolewa mahakamani?

Kwa hiyo, kwa kuondolewa kwake tu ni sehemu ya ushindi. Kudos kwa JF!

Kaka ...
 
we need to trust our Judicial Systems, they are independent na wanasimamia haki , kwenye hili la Cyber crime niwape Hongera kea one step forward atleast there is a room wa hizo Preliminary Objections kusikilizwa. Big Up
 
Back
Top Bottom