JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 4,991
Kesi ya Kikatiba: JamiiForums yashinda mapingamizi yaliyowekwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG)
Wakuu,
Mtakuwa mnakumbuka kuwa Jamii Media mnamo mwezi Machi mwaka huu walifungua KESI YA KIKATIBA kupinga matumizi ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015 kuwa vinavunja Haki ya Kikatiba na hivyo kuitaka Mahakama kuingilia kati nguvu kubwa iliyokuwa ikitumiwa na Jeshi la Polisi ili kulinda usiri na uhuru wa watumiaji wa mitandao nchini.
Serikali, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) iliweka mapingamizi (Preliminary Objections) sita ikitaka kesi nzima ifutwe na Jamii Media walipe gharama zilizoingiwa.
Leo hii, Mahakama Kuu ya Tanzania imezipitia hoja zilizowasilishwa na Serikali na Wanasheria wa Jamii Media na kuamua kuwa mapingamizi yote sita ya Serikali hayana mashiko na hivyo kesi ya msingi itaendelea kusikilizwa haraka iwezekanavyo.
Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Bw. Maxence Melo akiwa na Wakili wa kampuni, Benedict Ishabakaki muda mchache baada ya kupata maamuzi ya mahakama.
Hii ni hatua kubwa kufikiwa kuelekea Uhuru wa Maoni kwa watumiaji wa Mitandao(Online Freedom of Expression) na jitihada za kulinda watoa taarifa ndani na nje ya mtandao(Whistleblowers).
HAYA NDIYO MAPINGAMIZI(Preliminary Objections) YA SERIKALI DHIDI YA SHAURI LA JAMII MEDIA:
Tutaambatanisha maamuzi ya mahakama(ruling) baadae.
Asanteni