JamiiForums Usiku wa manane

JamiiForums Usiku wa manane

1791914484165.jpg
 
Aliahidiwa IPhone na hakuipata,alichopata ni Ngoma

Hizi ambazo huwa nakuletea hapa sio habar za kutunga ni a real time event ambazo zinatokea kitaa

Ni mume na mkewe ambao wapo kwa ndoa for almost 5 years, mume ni mtu wa kusafiri safiri sana kutokana na nature ya kazi zake

Lakini kila wiklend mume hutoka Nairobi na kuelekea Eldoret kuiona familia yake,kwa wakazi wa Kenya wanajua umbali uliopo kati ya sehemu hizo mbili

Mume akiwa huko kwenye majukumu yake,mke huku akapata majaribu ya kukutana na sponsor

Ilikuwa ni club, so mke aliahidiwa atanunuliwa Iphone na huyo sponsor

Je mchongo au mbanga nzima ilijulikanaje?

Twende kazi......

Katika pekua pekua mameseji kwenye simu rununu/smart phone ndio mpango mzima ukaja kwenye dashboard

Yes, mke anachat na best yake,anamwambia " yani hapa nilipo naregret nimepima leo nipo positive"

Mke akaendelea kusema " unamjua yule mbaba ambaye tulikutana nae club,sijui ilikuwaje nikaingia kwenye hii trap,aliniahidi atanipa Iphone"

Mdada akaendelea kutiririka kwa kusema " lakini Iphone yenyewe sikupata na wala hata nilipo lala nae wala sikuinjoy"

Best yake akamwambia "sasa usimwambie mtu yoyote habar hizi hata yule unayemuamini si unajua stigma is real"

Best mtu akendelea kumfunda mwenzake " si una ona hata mimi Nilikuambia kwamba nipo positive,ila si unajua Steve na tumeachana,nilimwambia yeye ndio kaniambukiza na nikamkomalia anipe hela nisimtangaze"

Best mtu hana baya akaendelea kutoa somo la bure " Kwahiyo na wewe msingizie mumeo kwamba ndio amekuambukiza,na hivi ni mtu wa safari safari basi mwambie amekuletea ugonjwa"

Naam wasomaji wangu, Iphone imeleta balaa nyumbani,mke kaingia tamaa ya kupata iphone na ambayo hakupewa lakini badala yake kaambukizwa maradhi.

Tuna la kujifunza hapa,mke akaulizwa na mume wake yani mimi kuhangaika kote huko saa nyingine nafanya kazi usiku na mchana ili familia muishi gud ndio malipo ni haya? Mke akajibu am sorry it's a mistake nilikuwa nimelewa

Mume akahoji tangu tuishi wote ushawahi sikia ninanukia harufu ya pombe? Au marafiki zangu wamekwambia nakunywa pombe?


View: https://youtu.be/0eaMT_BwYH8?si=8QgdrgB1zQ2lVA3L

Mume akauliza tena,tangu nimekuoa je nilishawahi kukupeleka club? Mke akajibu hapana, mume akasema imekuwaje ukaenda club na bila kuniomba ruhusa?

Mambo ni mengi na muda ni mchache ngoja niweke kalamu chini nichape lapa

Adios!
 
Back
Top Bottom