JamiiForums Mount Kilimanjaro Climbing Tour March 2015

JamiiForums Mount Kilimanjaro Climbing Tour March 2015

Kama watamani kujumuika na mfuko hauruhusu, kuja hapa! SINGLE LADIES ONLY.
 
Ni wazo zuri mkuu, inabidi watu wawe serious kweli kama wanataka kupanda mlima...
 
How I wish ndani ya hema watu tumelala.Tunaruhusiwa kuwa na mapartner wakati wa kulala?.....:beer:

Toa gharama mapema tunaolipiwa tujue tunaanza kuwaandaaje walipaji

Ila wewee!
 
nakubaliana na members wengine kuwa ni wazo zuri ila tu ratiba ibadilike kidogo mlimani mwezi machi hadi mwanzoni mwa mwez juni kuna mvua ya hatari hata wazungu na maguide wazoefu wanashindwa so nashauri iwe may be katikati ya mwezi juni kuendelea.

Mkuu mwezi june kwa kweli mambo huwa magumu sana kwa sisi wakawaida kupata nafasi.

Mwezi wa pili tatu, nne na wa tano ni low season..
 
me nasubir hizo gharama ndo ntatoa uamuzi but am ready for the fursa
 
me nasubir hizo gharama ndo ntatoa uamuzi but am ready for the fursa

Karibu mkuu,
tunaepisha ubabaishaji..
better kujua mdhamini anatoa hela ngapi..

ila kwa kifupi gharama za bila udhamini nitaziambatanisha na uzi huu muda sio mrefu..
 
Makadirio ya gharama huwekwa mepema ili kuwe na maandalizi ya mapema kwa wapandaji, na gharama hizi huwekwa kwa makundi - mfano, group ya watu 10 sh.200,000@, watu 20 sh.150,000@ n.k.

Suala la wadhamin litakuja tu kupunguza makadirio ya gharama za awali. Kumbuka kwamba gharama ndio ushawishi mkubwa.

Nimekuelewa sana Mkuu asante, wazo lako nalifanyia kazi..

Na nitakuja hapa kwa majibu muda siyo mrefu.
 
Nasubiri gharama kamili na pia muongozo wa ma zoezi hasa wanaotoka kwenye joto la dar na Pwani !
 
GHARAMA ZA KUPANDA MLIMA
KILIMANJARO. (Bila udhamini)

Hapa tumechanganua kwa mchanganuo ufuatao.
Kama itakuwa ni kwa siku 5.. njia ya
Marangu.
Kwa Makundi ya watu wane wane,

Tunaweza kuwa na Gaidi moja kwa watu 4.
So
Mshahara wa guide ni sh. 150,000/= kwa
watu wanne

Mshahara wa wabeba mizigo (wawili kwa
watu wane) 75,000x2=150,000/=
Park fees + Rescue fee ni 72,000/= kwa siku
tano kwa mtu mmoja
Chakula, hapa sasa itakuwa ni interest ya sisi
wenyewe tununue nini…

Minimum nimekadiria 60,000/= kwa siku
tano.
Kuna Mpishi ni 20,000/= kwa siku.
Gesi mtungi mmoja ni 35,000/= one group

Permitte ya magaidi ni 32,000@
Kwa kuunganisha inakuwa hivi…

1. 150,000/4= 37,000/= watu wanne
wakilipia guide mmoja.

2. 150000/= 37000/= wabeba mizigo watu
wawili wanalipia mbeba mzigo mmoja.

3. National Park fees 72000/= kwa mtu mmoja

4. Food 60,000/= nimejumlisha mikate na
mboga za majani kwa ujumla

5. Gesi 9,000/= ( huwa mitungi inakodishwa
kwa sh. 35000)

6. Permit 8000/= (hii ni kwa ajili ya kibali
cha magaidi.)

Total ni sh. 223000 per individual.
So approximately ni Sh. 230,000/=

Utaratibu wa gears za kupandia kama vile makoti, buti, fimbo, mabegi na sleeping bags zinapatikana kwa kukodi.

Na unaweza ukapata full equipments kwa kukodi.


Ikumbukwe hapo ni bila ya udhamini,tukipata udhamini gharama inaweza kupungua mpk kwa kiwango cha asilimia 50,itategemea na wingi wetu sisi kwa watakaokuwa tayari kupanda.
 
Sawa ila pia tungependa zaidi tusitumie PM as hii ni shughuli halali so ukiweka kila kitu hapa wengi watajua ukweli wa mambo. Ni jambo jema na pia kwa kufanya hivi tunatangaza utalii wetu na kudumisha ushirikiano hapa JF. Wekeni gharama ili mtu ajipange asijekushtukizwa akakata tamaa. Pia weka condition za healthy! Je wanaotaka kupanda wawe fit kiasi gani! Je wanatakiwa mazoezi kwa muda gani etc!
 
Sawa ila pia tungependa zaidi tusitumie PM as hii ni shughuli halali so ukiweka kila kitu hapa wengi watajua ukweli wa mambo. Ni jambo jema na pia kwa kufanya hivi tunatangaza utalii wetu na kudumisha ushirikiano hapa JF. Wekeni gharama ili mtu ajipange asijekushtukizwa akakata tamaa. Pia weka condition za healthy! Je wanaotaka kupanda wawe fit kiasi gani! Je wanatakiwa mazoezi kwa muda gani etc!

Gharama imeshawekwa tayari angalia post namba 98.tukishapata idadi kamili ya member watakoenda ndo tutajua udhamini tutapata kiasi gani,ila ni matarajio yetu mpk january mwishoni tutakuwa tushajijua wangap watakaoenda so itakuwa rahs kupanga na kupeana taarifa zote zilzobakia za muhmu.!
 
Back
Top Bottom