Wakuu, Salamu ziwafikie wote na Heri ya mwaka mpya.
Wadau wa mambo ya utalii wa ndani na
mambo ya kijamii,
Teamrafiki kwa uchache tumeandaa Tour ya
kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa Tatu
mwaka 2015 kwa Wanajamiiforums wote
wenye willing ya kuupanda Mlima Kilimanjaro
lengo kuu likiwa ni kuhamasisha utalii wa
ndani na pia kushiriki katika shughuli moja
wapo ya kijamii, katika taasisi zinazouzunguka
Mlima Kilimanjaro.
Taratibu za kupanda na gharama zitaainishwa
vizuri hapo baadae, pindi members watakapo
jipanga vizuri na idadi kamili kujulikana.
Ndugu wanajamiiforums, kupanda Mlima
Kilimanjaro kwa mtu binafsi ni gharama sana,
na hii ndiyo inayowanyima Watanzania wengi
fursa ya kufurahia tunu hii kubwa tulionayo.
Kupanda Mlima Kilimanjaro kama kundi
inapunguza gharama kubwa.
kama vile mishahara ya waongozaji na
wabeba mizigo + chakula wakati wote wa
Upandaji.
Tutapanda kwa siku tano (5) kupitia njia ya Marangu
Ikumbukwe pia Mlima Kilimanjaro ndio
unaoongoza kwa kukusanya fedha nyingi
katika sekta ya utalii kuliko Kivutio kingine
chochote ndani ya nchi yetu.
Karibuni Tuupande Mlima Kilimanjaro.
Kwa wale wenye nia ya Kushiriki, Tafadhali
nifuate PM ili tupeane maelekezo vizuri.
Pia Kamati ndogo ya maandalizi ipo tayari
kwa ajili
ya kujibu maswali mbalimbali
yatakayoulizwa..
Mmoja wao ni mimi,
Tized,
Mr Rocky,
Mtoto halali na hela,
utafiti,
Mndengereko,
Ntuzu
Mrembo by Nature..
Katika maandalizi.