Mlima Kilimanjaro ni chanzo kikuu cha maji katika maeneo yote ya uchagani. Mifereji, mito, yote imeanzia huko.
Mlima huo ulipata umaarufu zaidi kwa kuwa na theluji(glaciers) ilihali upo karibu na equator. Theluji hiyo ilifunika mlima ule kilele chote.
Ila kwa miaka ya karibuni, asilimia zaidi ya 85 ya glaciers zote imeyeyuka na kutokomea milele. Glaciers hazirudi.
Haya ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na shughuli za binadamu. Wachaga wamekuwa wakikata miti kwa kwenda mbele bila kujali future ya vizazi vya baadae. Hawajui maji ndio wanayafukuza wenyewe. Machine za chainsaw zinanguruma kwanzia Rombo mpaka Siha na wanaona ni sawa tu. Hawajali.
Rai yangu, wananchi wajihurumie, na serikali iongeze patrol na ikiwezekana kuwe na sensa za miti ya asili kwa kila shamba na wenyeviti wa vitongoji na vijiji wahusike.