kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 19,489
- 18,380
Wakuu, Salamu ziwafikie wote na Heri ya mwaka mpya.
Wadau wa mambo ya utalii wa ndani na mambo ya kijamii, Teamrafiki kwa uchache tumeandaa Tour ya kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa Tatu mwaka 2015 kwa Wanajamiiforums wote wenye willing ya kuupanda Mlima Kilimanjaro lengo kuu likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani na pia kushiriki katika shughuli mojawapo ya kijamii, katika taasisi zinazouzunguka Mlima Kilimanjaro.
Taratibu za kupanda na gharama zitaainishwa vizuri hapo baadae, pindi members watakapojipanga vizuri na idadi kamili kujulikana.
Ndugu wanajamiiforums, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtu binafsi ni gharama sana, na hii ndiyo inayowanyima Watanzania wengi fursa ya kufurahia tunu hii kubwa tulionayo.
Kupanda Mlima Kilimanjaro kama kundi inapunguza gharama kubwa. Kama vile mishahara ya waongozaji na wabeba mizigo + chakula wakati wote wa Upandaji.
Tutapanda kwa siku tano (5) kupitia njia ya Marangu
Ikumbukwe pia Mlima Kilimanjaro ndio unaoongoza kwa kukusanya fedha nyingi katika sekta ya utalii kuliko Kivutio kingine chochote ndani ya nchi yetu. Karibuni Tuupande Mlima Kilimanjaro.
Kwa wale wenye nia ya Kushiriki, Tafadhali nifuate PM ili tupeane maelekezo vizuri. Pia Kamati ndogo ya maandalizi ipo tayari
kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali yatakayoulizwa..
Mmoja wao ni mimi,
Tized,
Mr Rocky,
Mtoto halali na hela,
utafiti,
Mndengereko,
Ntuzu
Mrembo by Nature..
Katika maandalizi.
Ziada: Kuna watu wanapost hapa kuwaogopesha wengine juu ya afya...
Kama mtu huna matatizo ya kifua(pumu and alike) au mafua au usiwe na ugonjwa wowote, unaweza kupanda Mlima Kilimanjaro mpaka Kileleni endapo tu, utazingatia Mazoezi ya kujenga pumzi.
==================================================================================
Wadau wa mambo ya utalii wa ndani na mambo ya kijamii, Teamrafiki kwa uchache tumeandaa Tour ya kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa Tatu mwaka 2015 kwa Wanajamiiforums wote wenye willing ya kuupanda Mlima Kilimanjaro lengo kuu likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani na pia kushiriki katika shughuli mojawapo ya kijamii, katika taasisi zinazouzunguka Mlima Kilimanjaro.
Taratibu za kupanda na gharama zitaainishwa vizuri hapo baadae, pindi members watakapojipanga vizuri na idadi kamili kujulikana.
Ndugu wanajamiiforums, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtu binafsi ni gharama sana, na hii ndiyo inayowanyima Watanzania wengi fursa ya kufurahia tunu hii kubwa tulionayo.
Kupanda Mlima Kilimanjaro kama kundi inapunguza gharama kubwa. Kama vile mishahara ya waongozaji na wabeba mizigo + chakula wakati wote wa Upandaji.
Tutapanda kwa siku tano (5) kupitia njia ya Marangu
Ikumbukwe pia Mlima Kilimanjaro ndio unaoongoza kwa kukusanya fedha nyingi katika sekta ya utalii kuliko Kivutio kingine chochote ndani ya nchi yetu. Karibuni Tuupande Mlima Kilimanjaro.
Kwa wale wenye nia ya Kushiriki, Tafadhali nifuate PM ili tupeane maelekezo vizuri. Pia Kamati ndogo ya maandalizi ipo tayari
kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali yatakayoulizwa..
Mmoja wao ni mimi,
Tized,
Mr Rocky,
Mtoto halali na hela,
utafiti,
Mndengereko,
Ntuzu
Mrembo by Nature..
Katika maandalizi.
GHARAMA ZA KUPANDA MLIMA
KILIMANJARO. (Bila udhamini)
Hapa tumechanganua kwa mchanganuo ufuatao.
Kama itakuwa ni kwa siku 5.. njia ya
Marangu.
Kwa Makundi ya watu wane wane,
Tunaweza kuwa na Gaidi moja kwa watu 4.
So
Mshahara wa guide ni sh. 150,000/= kwa
watu wanne
Mshahara wa wabeba mizigo (wawili kwa
watu wane) 75,000x2=150,000/=
Park fees + Rescue fee ni 72,000/= kwa siku
tano kwa mtu mmoja
Chakula, hapa sasa itakuwa ni interest ya sisi
wenyewe tununue nini
Minimum nimekadiria 60,000/= kwa siku
tano.
Kuna Mpishi ni 20,000/= kwa siku.
Gesi mtungi mmoja ni 35,000/= one group
Permitte ya magaidi ni 32,000@
Kwa kuunganisha inakuwa hivi
1. 150,000/4= 37,000/= watu wanne
wakilipia guide mmoja.
2. 150000/= 37000/= wabeba mizigo watu
wawili wanalipia mbeba mzigo mmoja.
3. National Park fees 72000/= kwa mtu mmoja
4. Food 60,000/= nimejumlisha mikate na
mboga za majani kwa ujumla
5. Gesi 9,000/= ( huwa mitungi inakodishwa
kwa sh. 35000)
6. Permit 8000/= (hii ni kwa ajili ya kibali
cha magaidi.)
Total ni sh. 223000 per individual.
So approximately ni Sh. 230,000/=
Utaratibu wa gears za kupandia kama vile makoti, buti, fimbo, mabegi na sleeping bags zinapatikana kwa kukodi.
Na unaweza ukapata full equipments kwa kukodi.
Ikumbukwe hapo ni bila ya udhamini,tukipata udhamini gharama inaweza kupungua mpk kwa kiwango cha asilimia 50,itategemea na wingi wetu sisi kwa watakaokuwa tayari kupanda.
Ziada: Kuna watu wanapost hapa kuwaogopesha wengine juu ya afya...
Kama mtu huna matatizo ya kifua(pumu and alike) au mafua au usiwe na ugonjwa wowote, unaweza kupanda Mlima Kilimanjaro mpaka Kileleni endapo tu, utazingatia Mazoezi ya kujenga pumzi.
==================================================================================
Herini ya mwaka wadau, japo kwa kuchelewa kuchangia suala hili ila naona mwelekeo mzuri kutokana na maoni yaliyotangulia. Binafsi nanuiwa sana kuwa miongoni mwa watu watakaoridhia kupanda mlima, japo nitakuwa kama muongozaji wenu endapo itatokea hivyo. Baada ya utangulizi huo, nipende kuzungumzia kwa uchache kuhusu suala la afya. Afya nitakayoisemea hapa ni ya katika mazingira ya mlima ambapo yeyote anayepanda, sharti asiwe na athma kwa kuwa ni moja ya ugonjwa unaoteketeza watalii wengi kwa kuwa wanaficha. Cha msingi ni mtu kuwa anaijua afya yake vyema, kwa kuwa uwapo kwenye high altitude oxygen huwa inashuka sana. Pili tatizo la kuumwa kichwa kwa mbali linawakumba wengi, vivyo ni muhimu kuzingatia unywaji wa vimiminika walau lita tatu kwa siku. Hii itasaidia sana kuepukana na tatizo hili, nakaribisha maswali.
Heshima yenu Wakuu. Poleni na hongereni kwa juhudi mlizozifanya mpaka sasa. Tuko pamoja sana. Sikukuu ilikuwa njema sana.
Nashukuru kwa ufafanuzi na michango iliotolewa so far, Ni mizuri na yenye kujenga na kuboresha tunachokiendea. nami nina machache.
1. Ninatamani ifahamike kuwa huu sio mradi au kaproject ka watu wachache kupata fedha au maslahi yeyote, bali imelenga kutoa fursa kwa kila mwenye NIA kuufurahia na kuupanda Mlima Kilimanjaro.
2. Kuwa juhudi zinazofanyika hadi sana, ni kujitolea kwa namna na kadiri mtu anavyoweza yeye mwenyewe kadiri ya moyo na mapenzi yake mema alionayo. Ndugu kiwatengu asante sana kwa kuwa mfano kwenye hili.
3. Lengo letu kwa umoja wetu ni kuhamasishana kuufurahia utalii wa ndani, kujifunza na kujenganga kwa namna moja au nyingine.
4. Kuwa ufadhili wowote utakaopatikana utawekwa wazi kwa uongozi wa JF hatua kwa hatua ili kuondoa mashaka au maneno ambayo yanaweza zushwa tu ili kuharibu lengo letu jema kabisa la #TEAM RAFIKI. Pia kwa ajili ya kuappreciate wafadhili wetu na kuwatangaza pia.
5. Kuwa Uongozi wa JF unashirikishwa na umekua ukishirikishwa kila hatua, tulikoanzia hadi tunakoenda. Tunawashukuru wamekua bega kwa bega na sisi hadi hapa. 'Like' zao kwenye post says it all.
6. Yeyote mwenye nia njema, mawazo, njia mbali mbali za ufadhili n.k anakaribishwa kwa mikono miwili ili ikiwezekana tuwe na ufadhili wa kila kitu kwa wote watakao kuwa tayari.
7. Kuwa ila ikitokea mmoja wa wanaJF akawa na ujuzi/vifaa au utaalamu unaotakikana, tutapenda wao wapewe priority kutoa huduma kwetu ndio wengine wafikiriwe kulinganga na ubora na viwango tutakaokuwa tunataka. watakaopenda kujitolea tunawakaribisha saana.
8. ...................
NB: Kupanda mlima Kilimanjaro ni moja kati ya changamoto nzuri na tamu kuliko unavyoweza kufikiri. Si tu kwa umaarufu wake au urefu wake, bali kwa vivutio mbali mbali, maisha yanavyojitokeza kwa namna zote kwako na wale wanaokuzunguka, Changamoto ya mazoezi, changamoto pia ya kufikia malengo.
Mara ya mwisho mimi kupanda miaka mitatu minne iliopita tulikua watanzania 24, Nane tulifika kileleni (Wanaume 5 na wadada 3) , 10 walifika Gilman's point (Mwinuko wa Mita kama 5,600 Juu ya mlima ila kabla ya kileleni Mita 285 za mwinuko kutoka kileleni ambako ni mwinuko mita 5,895) wengine 6 waliishia katikati ya Kibo (last sleeping point) na Gilmans Poing.
Hakuna aliyedhurika au kupata tatizo lolote (wanaume 13 wanawake 11 - rika mbali mbali tulirejea salama kabia na bado wengi wetu tunapenda kupanda na tutapanda tena.. its a very exciting expedition)
Changamoto kubwa nilioiona ni mazoezi ya viungo na pumzi Baasi.... Ukijitahidi kufanya mazoezi ya viungo na ya kutafuta kuwa na pumzi ndefu na ukawa huumwi, safari itakuwia taamu sana.
Karibuni sana, Wale tulioko Dar, tuendelee na mazoezi ya kuimarisha misuli ya miguu na ikiwezekana kukimbia beach (mchangani) ni zoezi saafi sana kuongezea pumzi na kuimarisha misuli.
Asanteni. Pamoja sana
[TABLE="width: 604"]
[TR]
[TD]GHARAMA ZA KUPANDA MLIMA
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KILIMANJARO. (Bila udhamini) siku 5 njia ya Marangu
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hapa mmechanganua kwa mchanganuo ufuatao.
[/TD]
[TD][/TD]
[TD]Idadi
[/TD]
[TD] Gharama
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kwa Makundi ya watu wane wane,
[/TD]
[TD]Wapandaji
[/TD]
[TD]4
[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Gaidi moja kwa watu 4/inatakiwa na wasaidizi .
[/TD]
[TD]Kiongozi/Guides
[/TD]
[TD]2
[/TD]
[TD] 300,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kuna Mpishi ni 20,000/= kwa siku.
[/TD]
[TD]Mpishi
[/TD]
[TD]1
[/TD]
[TD] 100,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mshahara wa wabeba mizigo (wawili kwa watu 4)
[/TD]
[TD]Mabeba/Porters
[/TD]
[TD]2
[/TD]
[TD] 150,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Park fees + Rescue fee ni 72,000/= kwa siku
[/TD]
[TD]Ada kiingilio
[/TD]
[TD]5
[/TD]
[TD] 200,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Chakula, hapa sasa itakuwa wenyewe tununue nini
[/TD]
[TD]Nyumba/hut
[/TD]
[TD]4
[/TD]
[TD] 80,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Gesi mtungi mmoja ni 35,000/= one group
[/TD]
[TD]ada wokoaji
[/TD]
[TD]4
[/TD]
[TD] 8,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Permitte ya magaidi ni 32,000@ ?
[/TD]
[TD]Chakula
[/TD]
[TD]5
[/TD]
[TD] 300,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]Gesi
[/TD]
[TD]1
[/TD]
[TD] 35,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]1. 150,000/4= 37,000/= watu wanne? 37,500/=
[/TD]
[TD]Ada ya wapagazi
[/TD]
[TD]8
[/TD]
[TD] 28,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]wakilipia guide mmoja.
[/TD]
[TD]Jumla
[/TD]
[TD]4
[/TD]
[TD] 1,201,000.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2. 150000/= 37000/= wabeba mizigo watu? 37,500/=
[/TD]
[TD]Kwa mmoja
[/TD]
[TD]1
[/TD]
[TD] 300,250.00
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]wawili wanalipia mbeba mzigo mmoja.
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3. National Park fees 72000/= kwa mtu mmoja?
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4. Food 60,000/= nimejumlisha mikate na
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]mboga za majani kwa ujumla
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5. Gesi 9,000/= ( huwa mitungi inakodishwa
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]kwa sh. 35000)
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6. Permit 8000/= (hii ni kwa ajili ya kibali
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]cha magaidi.)?
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Total ni sh. 223000 per individual.
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]So approximately ni Sh. 230,000/=
[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD]Hebu linganisha na quote yako wapi ulisahau[/TD]
[/TR]
[/TABLE]