JamiiForums Mount Kilimanjaro Climbing Tour March 2015

JamiiForums Mount Kilimanjaro Climbing Tour March 2015

Tutakuja lakini hakuna kuulizana a.k.a. zetu za humu jamvini!
 
Naomba unitafutie wa kunisukuma kwenye vilima, kama mlivyofanya kule njia nyembamba mapangoni Amboni

Tutakusukuma mimi na Blaki Womani............tumeanza mazoezi leo mlima Kijenge........hivyo usihofu shostito..........
 
Last edited by a moderator:
Wazo zuri na gharama zilizooneshwa siyo mbaya sana.

Kima nitashindwa kupanda mlima basi naweza kutuma mwakilishi.
 
Wakuu, Salamu ziwafikie wote na Heri ya mwaka mpya.

Wadau wa mambo ya utalii wa ndani na mambo ya kijamii, Teamrafiki kwa uchache tumeandaa Tour ya kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa Tatu mwaka 2015 kwa Wanajamiiforums wote wenye willing ya kuupanda Mlima Kilimanjaro lengo kuu likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani na pia kushiriki katika shughuli mojawapo ya kijamii, katika taasisi zinazouzunguka Mlima Kilimanjaro.

Taratibu za kupanda na gharama zitaainishwa vizuri hapo baadae, pindi members watakapojipanga vizuri na idadi kamili kujulikana.

Ndugu wanajamiiforums, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa mtu binafsi ni gharama sana, na hii ndiyo inayowanyima Watanzania wengi fursa ya kufurahia tunu hii kubwa tulionayo.

Kupanda Mlima Kilimanjaro kama kundi inapunguza gharama kubwa. Kama vile mishahara ya waongozaji na wabeba mizigo + chakula wakati wote wa Upandaji.

Tutapanda kwa siku tano (5) kupitia njia ya Marangu

Ikumbukwe pia Mlima Kilimanjaro ndio unaoongoza kwa kukusanya fedha nyingi katika sekta ya utalii kuliko Kivutio kingine chochote ndani ya nchi yetu. Karibuni Tuupande Mlima Kilimanjaro.

Kwa wale wenye nia ya Kushiriki, Tafadhali nifuate PM ili tupeane maelekezo vizuri. Pia Kamati ndogo ya maandalizi ipo tayari
kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali yatakayoulizwa..

Mmoja wao ni mimi,
Tized,
Mr Rocky,
Mtoto halali na hela,
utafiti,
Mndengereko,
Ntuzu
Mrembo by Nature..
Katika maandalizi.




Ziada: Kuna watu wanapost hapa kuwaogopesha wengine juu ya afya...
Kama mtu huna matatizo ya kifua(pumu and alike) au mafua au usiwe na ugonjwa wowote, unaweza kupanda Mlima Kilimanjaro mpaka Kileleni endapo tu, utazingatia Mazoezi ya kujenga pumzi.

nimewasiliana na makerting &promotion officer wa mlima kasema kama mtahitaji msaada kutoka kwake hasa kwenye park fee tuwasiliane nae namba yake ni 0713 403387
 
Samahani hao Magaidi ni kutoka Somalia, Nigeria, Iraq au Korea?
 
Last edited by a moderator:
Unarudi kutoka wapi.....wewe......leo jioni saa kumi tukutane mlima Kijenge kwa mazoezi.........naomba usije na njumu.......njoo na viatu vya kupanda mlima.........mpitie PakaJimmy na Valentina.............

Nasubiri uje unichukue na popobawa ujue...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom