JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Vitu laiiiìni
Screenshot_20180728-092817.jpg
 
kila mara app inanidai ni-login ili kushiriki ktk mada.....
yani imekua kama adhabu ss maana ina-logout yenyewe.
 
hongera boss maXmellO,,, taratibu taratibu ku run social media so mchezo mchezo,, pamoja na changamoto mnazokumbana nazo still mko kwa hewa,, mi nlikuwa nahofia labda kungekuwa na kulipia acc,,, naomba msije fika huko [emoji23]
Hivi jamaa anapata faida gani na huu Jf financially?
 
Embu punguzeni kulalamika basi mbona Fb na insta wanaupdate na kubadili na hamuwalaamikii
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45
5) Search itakuwa inaleta matokeo haraka na relevant zaidi
6) Wanaotumia app wataona baadhi ya vitu ambavyo walikuwa wakikwama vikiwa vimetatuliwa
7) Emoji nyingi zitakuwa rahisi kutumiwa na yeyote (ziko supported)
8) JF itaanza kufunguka kwa kasi zaidi ya awali

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Mkuu Maxence Melo katika pitia pitia maboresho kuna vya zamani naona vimebadiloshwa ambavyo naona ni muhimu bado...

1. Page list yaani ile 1,2,3,4,5.....26 kwa sasa imetolewa imebakizwa option ya "prev na next" ile page list ni muhimu mtu anaweza kwenda page husika ya thread bila kupitia kila page...kwasasa inamaana nikitaka kwenda page ya 10 nalizmika kupitia zote kitu ambaacho sio sawa haswa kama nilishapitia page za mwanzo

2. Kuondolewa original post katika mwanzo wa page. Version iliopita ilikuwa inaweka original post juu ya kila page. Hii ni muhimu mfano mchangajia au msomaji akiingilia page za mbele anaweza kujua post inahusu nini. Kwasasa itamlazimu kupitia page ya kwanza kujua post inahusu nini kitu ambacho hakitoi machagua ya kutosha.
 
bado kuna tatizo sehem ukienda next page bado unakutana na mada za previous page.
kwa tunaotumia free basic naona shida inazidi
2.kwenye page list naomba ibaki 1,2,3,4,......nk unamsaidia sana msomaji
 
Back
Top Bottom