JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Mfano nikikumention Maxence Melo halafu nikaclick hiyo username nikiwa kwenye app inafungukia kwenye browser badala ya kwenye app tena

Usernames na link zote zinadirect kwenye browser hata kama unatumia app... Rekebisheni hiyo kitu
 
Last edited:
jamani hii JF APPS lini itapatikana katika PC's moja kwa moja ili tuachane na matumizi ya imulators ambazo zinakula sana ram
 
hongera boss maXmellO,,, taratibu taratibu ku run social media so mchezo mchezo,, pamoja na changamoto mnazokumbana nazo still mko kwa hewa,, mi nlikuwa nahofia labda kungekuwa na kulipia acc,,, naomba msije fika huko
 
Aina gani ya simu? Maana ni mojawapo ya vitu vilivyorekebishwa


Nilisema tangu awali: DISLIKE ilishaleta mgogoro humu!
kwa mimi naona bora kiwepo ili kuwe na uhalisia wa mambo maana kama hakipo hata hiko cha LIKE kitakuwa hakina maana sana mkuu

ila kwa haya maboresho kwakweli HONGERENI SANAAAAAAAAAAAAAAA BIG UP UONGOZI WA JAMIIFORUMS
 
Aina gani ya simu? Maana ni mojawapo ya vitu vilivyorekebishwa


Nilisema tangu awali: DISLIKE ilishaleta mgogoro humu!
HTC DESIRE 820. nimejiridhisha kukagua hicho kitufe kabla sijapandisha hii comment. Unless otherwise Kama kinachagua aina ya simu
 
Nichukue fursa hii kuwashukuru wote kwa uvumilivu.

Tunaomba radhi kwa kupitisha muda, posts za JF ni nyingi na hatua ya kuzipitia upya ilikuwa ndefu.

Kwa sasa emojis zote ziko supported na mengine mengi.

Kuna vitu tunaendelea kuvirekebisha; ndani ya saa 48 zijazo mapendekezo yenu yatafanyiwa kazi.

Asante
Habari boss..
Mkuu mbona kile kipengele cha simmilar threads (kama niko sahihi) hakipo? Fanyeni mpango mkirudishe
 
Mkuu sana Maxence Melo

Hongera na asante kwa marekebishi haya. Kifupi ni mazuri. Ila ninatatizo moja naomba kama itawapendeza mlifanyie marekebisho.

Ninaposoma heading ya habari kuna nyakati huwa sipendi kusoma page ya kwanza kwa sababu mbali mbali. Kuna wakati nataka nifungue moja kwa moja mfano page ya sita au ya mwisho kabisa.

Tatizo ukifungua page hiyo komenti ya kwanza si ile ya mleta mada aliyoianzisha (kama ilivyo katika uzi wako huu), utakuta unasoma komenti za wachangiaji pasipo kujua mleta uzi ameongelea nini!

Hii imetomea katika nyuzi zote isipokuwa uzi wako huu tu.

Nadhani mngerudisha utaratibu ule ambao unalofungua page tu unakutana na na maelezo ya kwanza kabisa ya mleta uzi.
 
Mkuu sana Maxence MeloNadhani mngerudisha utaratibu ule ambao unalofungua page tu unakutana na na maelezo ya kwanza kabisa ya mleta uzi.
Tulibaini kuwa watu wana-abuse pia hii. Walikuwa wana-quote bandiko reeeeefu na kuwaumiza wanaotumia simu. So, ni selected threads tunachagua 1st post ionekane kila unapoperuzi kurasa zaidi.

Hata hivyo, tunaliangalia upya hili
 
Tulibaini kuwa watu wana-abuse pia hii. Walikuwa wana-quote bandiko reeeeefu na kuwaumiza wanaotumia simu. So, ni selected threads tunachagua 1st post ionekane kila unapoperuzi kurasa zaidi.

Hata hivyo, tunaliangalia upya hili
Vema mkaangalia upya. Kwani pia mwaweza kuiweka kwa mtindo wa "Click to expand"
 
Wakuu JamiiForums naomba mtakapofanya maboresho mzingatie yafuatayo:

1. Tenganisha option ya EDIT na DELETE kutoka MODERATE. Hakuna haja ya kuunganisha haya maneno....yatenganishwe yakae mbalimbali. Inauddhi sana kufunguafungua mara nyingi. Mbona zamani hayo maneno yalikuwa yametenganishwa na maisha yalikuwa poa.

2. Kwa tunaotumia simu, ukishaingiza jina/email na password, neno LOGIN halionekani. Panakuwa blank ila tunatumia tu uzoefu kubonyeza kwenye hiyo blank space ili ku-login. Member ambaye hawezi kujiongeza hawezi ku-login.

3. Turudishie zile emoj zote zilizokuwepo kwenye JF ya zamani. Hata mtu ukitumia PC huwa napata emoj za vichwa tu....sipati zaidi ya hizo.

4. Rudisha ule muonekano wa zamani wa mobile app kwani ulikuwa rahisi kutumia kuliko huu "ulioboreshwa". Afadhali hata mtu ambaye hakupakua upya application anaenjoy kutumia JF kwa ufanisi kuliko sisi tuliopakua.

Nawasilisha.
 
Last edited:
Back
Top Bottom