JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Sawa, msisahau usalama wa taarifa zetu. Pia wekeni option ya ku delete a/c, mfano mtu amefungua akaunti mbili ila anataka aifute mojawapo..wezesheni na hapo pia
 
Mwonekano wa JF kwa tuliotumia jf 2011ff, ulikuwa mzuri zaidi kuliko wa sasa.

Enzi zile kuona page ya JF kwenye pc au simu bila app ulikuwa wenye mvuto mkali aisee
 
Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Mbona nikitaka kuangalia nyuzi nilizo following ainanionyesha baadhi tu kisha inaleta kitu cha namna hii
Screenshot_2018-07-23-21-33-09.jpg
 
Weka uwanja katika kila jukwaa ambapo mtu ukiingia humo unaona list ya link zote zilizowahi kutumwa kwenye jukwaa hilo mfano mtu anashida no magrupu ya ujasiliamari na biashara ata-click sehemu iyo kwenye group la biashara inakuwa rahisi.

Pia mukiongeza jukwaa la wasomaji vitabu itaongeza radha na tija ya jamiiforums.
 
Pamoja sana,kwa maboresho [HASHTAG]#maxence melo[/HASHTAG]
 
Wekeni pia option ya kubadili user details kama email nk
 
Sawa. Ahsante kwa taarifa.

Mtukumbuke na sie tusio na access ktk jukwaa la Dini na lile la wakubwa.
 
me mwenye nashauri hii kitu iwepo kwa store zote, ndg Maxence Melo nimetengeneza app ya JF itakayotumiwa na watu wa simu za kawaida kabisa (java) naomba ruhusa niitupie
Nitumie CV yako na hiyo app nione kama unafaa kuongezwa kwenye payroll yetu JF
 
Back
Top Bottom