JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

JamiiForums - Maboresho ya mwaka 2018

Wakuu,

Napenda kutoa taarifa mapema kuwa kutakuwa na maboresho kadhaa ili kutekeleza baadhi ya maombi ya wadau na kurekebisha kasoro kadhaa katika tovuti na app yetu.

Aidha, baada ya utafiti tulioufanya (tunawashukuru wote walioshiriki katika utafiti huu), kuna mengine yataendelea kuongezwa na kuboreshwa ndani ya siku 45 zijazo.

JF inayoonekana na kutumika sasa ilifanyiwa maboresho yaliyotokana na utafiti kwa wadau kati ya mwaka 2012 hadi 2016 ambapo Januari 2016 ilianza kutumika rasmi. Ni hii hii inayoboreshwa zaidi mwaka 2018 ili kuzidi kuifanya JF iwe rahisi kwa wengi kuitumia na kuifurahia.

Yanayotarajiwa:
1) Kuna ambao hawataona utofauti haraka kwani hatujacheza mbali na kilichozoeleka lakini wataona urahisi zaidi wa kuitumia JF
2) Kuna watakaoona baadhi ya vitu vimeondolewa - hivi vitatolewa sababu za kuondolewa kwake na kuoneshwa maboresho yaliyofanywa ili kutopoteza vitu hivyo
3) App: Waliokuwa wakikwama kwa mambo kadha wa kadha - yamerekebishwa kwa kadiri tulivyoweza
4) Mapendekezo ya wadau baada ya JF kufanyiwa maboresho haya yatafanyiwa kazi ndani ya siku hizo hizo 45

Tunawashukuru kwa uvumilivu wenu na kushiriki katika utafiti uliofanywa (nje ya mtandao) ili kuboresha jinsi mnavyoutumia mtandao huu.

Asante
Thank you.!!
 
Hawawezi wakaweka kitufe cha dislike,kwa maoni yangu mimi hapa ni vyema wakafuata nyao za mitandao ya kijamii iliyofanikiwa zaidi duniani kama vile facebook ambao hawana kitufe cha dislike!!
Mbn youtube kipo
 
Mkuu melo hongera kwa hatua hiyo ila msisahau katika app inayopatikana play store kwa android (kwale ambao ni Mara yao ya kwanza kuingia kwa ku-install app ya jf katika simu zao ) app inakosa option ya ku-log in kinachofanyika ni kubofya kwa chini tuu ila ile option ni muhimu sana nakumbuka those days Niko na kasimu kapya na nilikua nahitaji ku-istall hii app ilinipa shida sana naomba kuwasirisha
 
Angalau mmesikia kilio chetu maana huwa nashindwa kabisa kulog in kwa kutumia simu yangu
Mkuu nadhani ulikua na shida kama yangu kwani ilikua Niki install app ya jf nikitaka sasa ku log in ikawa inazingua (kama tatizo ni hilo )

Solution
Fanya hivi kwenye app yako katika cm yako kuna username/gmail account
Then chini yake kuna password
Basi bhana ukiweka tuu password we bonyeza kwa chini yake hata kama huoni log in option ndo log in option yenyewe ilipo
 
We jamaa ungekuwa 'mbelez' huko naamini ungekuwa kundi moja na akina Mark Zuckerberg, bahati mbaya unayafanya haya ndani ya nchi masikini, masikini wa vipato na fikra.

Hongera sana.
 
Back
Top Bottom