kila mtu na mtazamo wake sawa
kaa ukijua tunaishi ndani ya jamii ambayo ukienda nayo tofauti lazima ina haki ya kuuliza nini tatizo maana utakuwa hauko sawa ingawa ndani yako inaweza isiwe hivyo
pamoja na yote huu ni mtizamo wangu
Jamii zote zilizoendelea zimepata kuendelea kwa kujali faragha na maamuzi ya watu binafsi. Hata wanapokuwa tofauti na jamii.
Kwa sababu hakuna jamii isiyo na watu binafsi, na hata hawa watu binafsi walio tofauti na dominant streams within jamii, ni sehemu ya jamii.
Hivyo ndivyo watu walivyopata kujua kwamba dunia si bapa bali ni tufe karibu na mduara.
Hivyo ndivyo watu walivyogundua kwamba jua halizunguki dunia, bali dunia inazunguka jua.
Hivyo ndivyo watu walivyogundua kwamba muda si kitu kimoja kwa ulimwengu mzima (I am not talking about time zones, rather Einstein's relativity) na unategemea kasi na sehemu ya mtazamaji.
Kama binadamu angekuwa anaaangalia na kuheshimu taratibu za jamii muda wote, tungekuwa bado tunaishi mapangoni na hata moto hatujagundua mpaka leo.
Kwa sababu hata ugunduzi maana yake ni kuibua kitu kipya na tofauti, ambacho hakijakubalika wala kujulikana na jamii.
Kwa hivyo, kama jamii inataka kuendelea, haina budi kuwakubali qanaoenda tofauti nayo na ku challenge maoni fulani ambayo yanaonekana kuwa kweli kama injili.
Kwa sababu kushikilia maoni ya jamii kwa sababu ni ya jamii tu kungetufanya tuamini dunia ni bapa na inazungukwa na jua mpaka leo.