Jamii Media yafungua Kesi ya Kikatiba kupinga Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao

wanapaswa washindwe kwa hili najua ni nape na group lake wakijaribu kutumia ubabe hakuna sabab ya ss kushindwa kuwadhibiti wachache wenye lengo la kudhoofisha jf malengo tunayo nguvu tunazo
 
polisi kudai taarifa za watu wanaoibua matukio ya kifisadi wanafanya hivyo kwa lengo la kumtetea nani tatizo tulishajadili kuhusu jeshi letu la polisi livunjwe kwani liko kwa ajili ya kutetea maslahi ya watu wachache na wengi hawajui nini wajibu wao
 
Anzisheni namba za e-pesa tuanze kuchangia haps tafadhali. Ila be aware of wapigaji.
Naahidi 20,000 let us go.
 
Hivi hii serikali ya magufuli mbona inaendeleza mambo yaliyopingwa na umma utawala uliopita....
 
Wale vijana 46 nao watusaidie katika hili!!! maana wanajua faida ya jukwaa hili la pekee hapa Tanzania.
 
Inasikitisha sana, hawa viongozi wanajisahau sana, wanasahau wao wanatuwakilisha sisi, Ila wao wanajiona Ndio wenye haki Na mamlaka yote juu yetu! Binafsi nipo Nyuma yenu WAKUU wote wa JF, shoulder to shoulder until the last drop! Sisi wanaCDM tunakamsemo ketu "sauti ya wengi Ni sauti ya Mungu". Tushirikiane sote! Imagine Maisha bila JF yatakuaje!!
 
1.jpg


2.jpg


Septemba Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.


Leo March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com na Fikrapevu.com imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza unaolindwa kwa mujibu wa katiba ya Nchi.


Jamii Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38 cha sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya. Akizungumza kwa niaba ya Jamii Media,wakili Shukuru Mlwafu ameeleza…


"Baadhi ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo kikatiba.


"Njia pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu hivyo na kuiomba mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni batili kwa kuwa vinaenda kinyume na ibara 16 na 18 ya katiba" Amesema Shukuru Mlwafu


Hatua hiyo ya kufungua shauri Mahakamani imekuja baada ya kuwepo na shinikizo kutoka Jeshi la polisi kuwataka Jamii Forum kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Maxence Melo amesema..


"Kuanzia uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa jamii forum kitu ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za wateja, majina halisi na hata maeneo waliopo.Sasa tunaona hii itapekea kuvunjwa kwa haki ya watumiaji wa Jamii forum":-Amesema Maxence Melo
 
mapambano ni kwa wote na sio kuachiwa uongozi tu.. Wote tupaze sauti katika kukemea huu ukandamizaji unaofanywa na watu wasio na Uelewa katika Kazi Zao. Vyama pembeni pamoja tupambane kuifanya Jf iwe sehemu salama zaidi
 
Tusimame kwa pamoja kuitetea JF bila kujali itikadi zetu.

Natamani kila member atie neno kwenye uzi huu.
 
Binafsi nitaanza kuunga mkono mchakato wa utumbuaji majipu pale sheria za hovyo kama hii zitakapoanza kufutwa au kurekebishwa.
 
Hahaha...walianza kwa kusingizia kuwa tunawatukana,kuwavunjia heshima na kuwadhalilisha Viongozi,sasa wameona jinsi gani wananchi wanafuatilia kwa ukaribu kujua ni jinsi gani fedha za umma pamoja na kodi zetu zinavyotumika wanataka kutublock.

Nape aache huu utoto,ikiwa ninyi ni Viongozi mnaojikubali kuwa ni viongozi bora na hamna kona kona zozote ni kwanini hamjiamini kiasi hiki?
 
niko pamoja nanyi jamii media katika hili,hawa ntarahamwe wakiruhusiwa kupata taarifa zetu tutakwisha.
 
Nipo pamoja na jamii media kwenye hili.......sehemu pekee ya kutoa maduku duku yoote ni hii.....JK kwenye habari alijitahidi
 
Back
Top Bottom