Jamii Media yafungua Kesi ya Kikatiba kupinga Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao

Kampuni ya Jamii Media ambayo ndiye wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums na FikraPevu wamewasilisha mashtaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga ushuruti waliopewa na Polisi kutoa taarifa binafsi za wanachama wake.

Ushuruti unakuja kutokana Sheria ya Uhalifu Mitandaoni (Cyber crime law).

Taarifa ya kilichojiri zitawajia punde.

View attachment 327323
=======================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

View attachment 327311

Kampuni ya Jamii Media, inayoendesha mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com imejijengea heshima na umaarufu kwa muda mrefu kutokana na namna inavyoendesha na kusimamia shughuli zake ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kimtandao.

Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums.

Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamoto nyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara.

Kwa takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huu (kwa njia ya barua rasmi) kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi.

JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wake, imekuwa ikihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja bila kupewa maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwakuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai).

Mwisho, JamiiForums inamuunga na itaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao.

View attachment 327308
Imesainiwa na

Maxence M. Melo

Mkurugenzi Mtendaji – Jamii Media

Machi 04, 2016

8c1016be1df44b946a10edc5925784cf.jpg

854c214106da08eed500c60f4ddd1c43.jpg

NB: Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia ameunganishwa katika kesi hii

HII TAARIFA MBONA YA MWEZI MARCH 2016 ? VIZURI MNGETUPA UPDATE YAKE YA DEC.2016 !
 
Muda mwingine unashindwa kuamini unachosoma. Unadhani npengine ni script za movie ya Hoollywood.

Kwa takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huu (kwa njia ya barua rasmi) kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi.
 
Kwa Heshima ya kipekee nawapongeza Jamii Media kwa kuamua kulinda Uhuru na faragha ya watumiaji wa Mitandao na pia kwa kupigania haki ya kikatiba ya watanzania na kupingana na masharti kandamizi yasiyo ya kistaarabu katika karne hii ya sayansi na Teknolojia

Nimekua mwanachama wa JamiiForums Tangu Tarehe 18 July,2007 nikiwa Mwaka wa Pili Chuo kikuu na hapo kabla nilikuwa Mwanachama ambaye sikuwa nimesajiliwa

Tumekuwa na WanaJF wengi hapa wenye fani na taaluma mbalimbali.Pia viongozi wa Vyama,Serikalini,Mashirika na hata viongozi wa Dini.Wengine kwa majina yao halisi na wengine ya kificho (Baadhi yao Tunatambuana).

Katika Uanachama wangu JF nimewahi kupata misukosuko mingi na Jeshi la Polisi kutokana na michango yangu humu likiwemo tukio la Kuitwa Polisi asubuhi ya Tarehe 20 December 2013 siku ya Ijumaa na kuhojiwa kisa nilianzisha mjadala dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kipindi Hicho Emmanuel Nchimbi.

Polisi waliniambiwa kuna jalada ambalo liletwa na Dr.Nchimbi.Nikiambatana na Wakili Msomi Peter Kibatala Nilihojiwa kwa masaa kadhaa hadi kufukua thread na kuomba Password zangu za JF na Barua Pepe .Niliwakatalia kwa kuwa hawakua na haki hiyo

Hata hivyo Jioni yake kufika saa 3 Usiku aliyepeleka Jalada Hakuwa Waziri tena(Rejea Operesheni Tokomeza Bungeni).Ilikuwa Coincidence au Mipango ya Mungu?

Ni katika mazingira hayo niliona tishio la haki ya uhuru wa faragha na jinsi ambavyo vyombo vya dola pasipo uhalali wowote wanaweza kuhujumu haki za Raia na pia kukandamiza kabisa uhuru wa habari,haki ya kupewa Taarifa na pia kukandamiza haki za msingi kabisa za binadamu na kutishia misingi ya ukuaji wa utawala bora ambayo inashikiliwa na nguzo kuu mbili za uwazi na uwajibikaji

Ni jambo la ajabu kuwa serikali iliyoahidi kurekebisha sheria ya mitandao inaendelea kutumia dola kukandamiza vyombo vya habari

Kwa uamuzi huu wa JamiiMedia,Nitaungana katika mapambano haya kuilinda sio Jamii Forums Pekee bali haki za watanzania

JF ni nyumbani,Ni Chuo .Tubuni njia ya kuisapoti JF kwa kishindo katika kipindi hiki
Where are you Ben?
 
sijui utakuwa hai wewe mshikaji.....
 
Back
Top Bottom