Jamii Media yafungua Kesi ya Kikatiba kupinga Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
Kampuni ya Jamii Media ambayo ndiye wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya JamiiForums na FikraPevu wamewasilisha mashtaka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga ushuruti waliopewa na Polisi kutoa taarifa binafsi za wanachama wake.

Ushuruti unakuja kutokana Sheria ya Uhalifu Mitandaoni (Cyber crime law).

Taarifa ya kilichojiri zitawajia punde.

Mahakama.jpg

=======================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Logo.PNG

Kampuni ya Jamii Media, inayoendesha mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com imejijengea heshima na umaarufu kwa muda mrefu kutokana na namna inavyoendesha na kusimamia shughuli zake ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kimtandao.

Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na Duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 4 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe. Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wana JamiiForums.

Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamoto nyingi zinazopelekea waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara.

Kwa takribani miezi mitatu iliyopita, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao huu (kwa njia ya barua rasmi) kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake wanaoonekana kutoa taarifa zile ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaibua ufisadi mkubwa na ukwepaji wa kodi.

JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri (privacy) wa wateja wake, imekuwa ikihoji mashinikizo hayo yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja bila kupewa maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama hautatolewa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

Baada ya kupata mashinikizo takribani manne yanayoashiria kuwa haki ya watanzania watumiao mtandao wa intaneti na hasa watumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Jamii Media imeshauriana na Wanasheria wake na kuona ni wakati sasa wa Kuilinda haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa Uhuru wao wa Maoni na Kujieleza inayolindwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18 ambapo imefungua Shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwakuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mtandao wa JamiiForums utaendelea na shughuli zake kama kawaida na utaendelea kuwahakikishia watumiaji wake kuwa mahala salama pa kutolea madukuduku yao na hata kuisaidia Serikali kuonyesha nyufa zilipo kwa maslahi mapana ya Taifa (wakizingatia mwongozo wa ushiriki wa mijadala anuai).

Mwisho, JamiiForums inamuunga na itaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi kwa kutoa uwanja/fursa salama na rahisi kwa wananchi kuweza kuyaainisha yale wanayoyabaini kuwa yanachelewesha maendeleo ya Taifa lao.


Sign.png
Imesainiwa na


Maxence M. Melo

Mkurugenzi Mtendaji – Jamii Media

Machi 04, 2016




8c1016be1df44b946a10edc5925784cf.jpg

854c214106da08eed500c60f4ddd1c43.jpg


NB: Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia ameunganishwa katika kesi hii

=========

For the English Community:

JamiiForums drags the police to court over whistleblowers


Owners of the country’s most popular social media -- JamiiForums, have filed a lawsuit asking the High Court of Tanzania to stop the Police Force from compelling them to reveal names of graft and tax evasion whistleblowers.

JamiiForums claimed the Force had for the past three months been writing to them, demanding names of individuals giving them information on sensitive issues, including grand corruption and tax evasion.

The company, which commands about four million online readers a month, is asking the High Court to review Section 32 of the Cybercrime Act on disclosure of data and Section 38 on issues of court proceedings.

Section 32 allows the Police Force to order any person to disclose data required for criminal investigation or prosecution.

Under the law, if the owner of the data does not cooperate, a law enforcement officer may ask the court to compel the online service provider to submit particulars of its subscribers for investigation.

“We received four threats jeopardizing the right of Tanzanians using the internet, prompting us to recourse to court in a bid to protect the right to freedom of expression and opinion guaranteed by article 18 of the Constitution,” Jamii Media executive Director, Maxence Melo said.

Mr Melo said he wanted the court to review sections 32 and 38 of the Cybercrime Act for breaching of fundamental right of Tanzanians to use the internet as stipulated in Article 30(3) of the 1977 Constitution.

He pointed out that Section 32 of the Cybercrimes Act does not make it mandatory for the investigating police officer to seek judicial oversight while engaging in surveillance, and thus provides leeway for the abuse of surveillance powers.

"Section 38 on the other hand prevents a person to effectively challenge a government’s interference with his or her privacy given that request for surveillance is done ex parte. These provisions are clearly in violation of international standards on privacy and freedom of expression, and must be reformed" Melo insisted.

Under the Article, any person thinking that a certain provision in any law violates his right or duty may institute proceedings in the High Court for redress.

Mr Melo said for the meantime, JamiiForums would continue with its operations to ensure visitors of the forum were secure enough to vent their grudges and in so doing assisting the government in exposing the rot for the interest of the nation.

“JamiiForums supports President John Magufuli’s efforts to fight against graft by providing a secured platform for wananchi to expose things which delay national progress,” he said.

Mr Melo claimed that founders and other staff of the blog had been facing a number of challenges from the Police Force which were preventing them from executing their duties smoothly.

“JamiiForums wants to know provisions of the law we’ve breached, yet we end up getting unsatisfactory explanations and threats from the law enforcers,” he said.
 
Wanataka kuondoa uhuru wa habari.

Kama wanataka kuikandamiza JamiiForums na FikraPevu, sidhani kama JF itakuwa tena reliable source of information na kitakachotokea ni watu wengi kuikimbia JF.

Tundu Lissu, Mallya, Ole Milya, Kibatala na wengine, ipigieni JF maana Polisi na Serikali wanataka kutufukuza huku.
 
Hii ni mada muhimu sana. Binafsi nipo tayari kuwaunga mkono kwa hali na mali maana wanatupigania sisi ili Uhuru wetu usiminywe.

Uhuru wetu una faida isiyopimika kuliko faida wanayopata kupitia njia zao mbalimbali za kibiashara.
 
Kwa Heshima ya kipekee nawapongeza Jamii Media kwa kuamua kulinda Uhuru na faragha ya watumiaji wa Mitandao na pia kwa kupigania haki ya kikatiba ya watanzania na kupingana na masharti kandamizi yasiyo ya kistaarabu katika karne hii ya sayansi na Teknolojia

Nimekua mwanachama wa JamiiForums Tangu Tarehe 18 July,2007 nikiwa Mwaka wa Pili Chuo kikuu na hapo kabla nilikuwa Mwanachama ambaye sikuwa nimesajiliwa

Tumekuwa na WanaJF wengi hapa wenye fani na taaluma mbalimbali.Pia viongozi wa Vyama,Serikalini,Mashirika na hata viongozi wa Dini.Wengine kwa majina yao halisi na wengine ya kificho (Baadhi yao Tunatambuana).

Katika Uanachama wangu JF nimewahi kupata misukosuko mingi na Jeshi la Polisi kutokana na michango yangu humu likiwemo tukio la Kuitwa Polisi asubuhi ya Tarehe 20 December 2013 siku ya Ijumaa na kuhojiwa kisa nilianzisha mjadala dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kipindi Hicho Emmanuel Nchimbi.

Polisi waliniambiwa kuna jalada ambalo liletwa na Dr.Nchimbi.Nikiambatana na Wakili Msomi Peter Kibatala Nilihojiwa kwa masaa kadhaa hadi kufukua thread na kuomba Password zangu za JF na Barua Pepe .Niliwakatalia kwa kuwa hawakua na haki hiyo

Hata hivyo Jioni yake kufika saa 3 Usiku aliyepeleka Jalada Hakuwa Waziri tena(Rejea Operesheni Tokomeza Bungeni).Ilikuwa Coincidence au Mipango ya Mungu?

Ni katika mazingira hayo niliona tishio la haki ya uhuru wa faragha na jinsi ambavyo vyombo vya dola pasipo uhalali wowote wanaweza kuhujumu haki za Raia na pia kukandamiza kabisa uhuru wa habari,haki ya kupewa Taarifa na pia kukandamiza haki za msingi kabisa za binadamu na kutishia misingi ya ukuaji wa utawala bora ambayo inashikiliwa na nguzo kuu mbili za uwazi na uwajibikaji

Ni jambo la ajabu kuwa serikali iliyoahidi kurekebisha sheria ya mitandao inaendelea kutumia dola kukandamiza vyombo vya habari

Kwa uamuzi huu wa JamiiMedia,Nitaungana katika mapambano haya kuilinda sio Jamii Forums Pekee bali haki za watanzania

JF ni nyumbani,Ni Chuo .Tubuni njia ya kuisapoti JF kwa kishindo katika kipindi hiki
 
Watashinda kweli wakati Nape ndiyo katumwa kukamilisha mipango ya kuwabana zaidi vyombo vya habari
 
Hakika hawatashinda mipango ya Mungu haiwezi ingiliwa na kikundi cha wahuni wachache serikalini kutaka kupora haki ya wananchi kikatiba.

JF Mungu yupo nanyi naamini kesi hii mtashinda kwa niaba yetu tupo nanyi bega kwa bega pale mchango wetu mtakapouhitaji hatutasita kujumuika nanyi.

Muda huu sisi nanyi ni familia moja
 
hivi kwanini serikali isifanye kazi kwa maslah mapana ya umma na kuwapa wananchi uhuru wa kufanya, kuendesha maisha yao kwa uhuru bila kuvunja sheria za nchi.....? nini kinataka kufichwa? demokrasia inakuwa au inasinyaa?

Hongera sana JF.....
 
Napongeza uongozi wa Jamii Media kwa kupigania haki zetu, tunahitaji kuwaunga mkono kwa namna yoyote ile...hasa tukijikumbusha slogan yetu ya "Changia JF mkono mtupu haulambwi" . Hakika tunahitaji kusimama kwa pamoja katika hili kama familia ya Jamii Forum. JF forever
 
Back
Top Bottom