Jamii kuhusu watu wenye changamoto ya ulemavu wa akili

JOSIA PATRICK

New Member
Jul 24, 2021
4
2
Ulemavu ni nini!Ni hitilafu ya Kidumu ambayo inaweza kumkuta mtu yoyote yule awe mtu mzima au mtoto kwa nyakati tofauti ambapo inaweza kuwa wakati wa kuzaliwa kabla na baada ya kuzaliwa​

Walemavu ni kundi ambalo limetengwa sana na kusahaulika katika Jamii zetu ambapo watu wengi sana tumekuwa tukichukulia ulemavu kama jambo la aibu kama kitu cha ajabu ambapo hupelekea hata watu kuwaweka walemavu ndani bila kuwatoa yaan hawapati haki zao za msingi.

Jamii nyingi sana zimekuwa Na mtazamo ambao sio mzur ambapo tunachangia sana kuharibu vizazi vyetu ivi tunachangia sana wazaz ambao wanahudumia watoto wenye changamoto ya ulemavu kuwafungia ndan kutokuwachangamanisha na watoto wengine kwa sababu tu ya mawazo ambayo ni kama potofu kwetu sisi Jamii.

Jamii inabidi kubadilika na kuachana na kuwaza imani potofu kwa sababu wote tunaamini kwamba ulemavu unasababishwa na mambo mbalimbali wala sio mambo ya kishirikina kama ambavyo watu wengi tumekuwa tukizania.Ni wakati sasa wa sisi kubadilika na kuweza kujumuika na ndugu zetu katika kuwasaidia na kuchangamana nao katika kuleta hamasa katika jamiii na kuweza kufikia malengo kwa sababu pia walemavu wana haki zao kama ambavyo watu wengine.

Asante Napenda kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom