Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,920
Naandika mada hii kwa mujibu wa mila za Kiafrika ambazo zinaeleweka kuwa Mwanaume niKiongozi wa familia na ndie anaetakiwa kuwa Mkuu wa nyumba
Tafadhali hapa sio mahali pa kujadili kama hilo la ukuu wa nyumba kuwa ni sawa au laa maana limeshajadiliwa sana hapa,tujadili kile ambacho ninakileta kwenu
Siku hizi baada ya dunia kuwa "kijiji" kumekuwa na muingiliano wa tamaduni kiasi kwamba kuna baadhi ya tamaduni ambazo zimepotea na zingine kukua kwa kuigwa na jamii fulani
Pamoja na hayo hii hiondoi ukweli kuwa kila jamii ina utamaduni wake,hili ndilo linalopelekea kila jamii kutambulika kwa mambo fulani fulani,yaani ukiona mtu anakunywa kisusio utajua huyu ni wa kabila fulani au jamii fulani
Leo nahitaji kila mmoja wetu atuambie kuwa kwa uzoefu wake na anavyojua ni wanawake wa kabila gani ambao wana hulka ya kutaka kuwatawala waume zao pindi wanapoingia kwenye ndoa?
Vijana ambao hawajaoa hili huwa wanaliwaza sana kwani ni moja kati ya mambo ambayo hawataki sana kukutana nayo,naomba hapa kila mmoja aseme na atoe uzoefu wake na sababu za kutaja kabila au jamii fulani ambayo yeye anadhani ina jambo hili
Tafadhalini sana,wale watu ambao wana chuki binafsi na makabila fulani hili sio jukwaa lakuonesha chuki hizo ila hapa tunajulishana ili kuwekana sawa kwenye eneo hili
Kujulishana kunakuwa na faida sana hasa kwa wale ambao wako kwenye mahusiano na watu wa kabila ambalo litaonekana na tabia hii ili aamue mwenyewe,hii ni sawa na kuambiwa kuwa familia fulani ina maradhi fulani ya kurithi,atakaekuambia hatakuwa ameidhalilisha familia husika au kukuchukia bali atakuwa amekupa taarifa ambayo itakufanya ujue ukweli na kama utaamua kuingia kwenye familia hiyo siku ikaona jambo hilo usiende kwenye ramli kumtafuta mchawi
Vivyo hivyo kwenye hili,kama kuna mtu ambae anajua kabila fulani au jamii fulani ina kawaida hii ya kutaka kuwatawala waume zao basi akipewa taarifa hii kupitia hapa atajua cha kufanya na siku mkewe akianza harakati hizi basi asije akafikiria kuwa mkewe karogwa au kudhani ana mchepuko unaompa kiburi bali ajue tu kuwa hiyo ni kawaida ya kabila au jamii yao
Nadhani nimeeleweka
Karibu!