siyawezimatatizo
Member
- Apr 29, 2019
- 36
- 25
MWALIMU NA JAMII
Kumekuwa na tabia za kumshambulia mwalimu kila mara anapofanya kosa hasa kwenye mitandao ya kijamii. Ni rahisi sana jamii yetu kukimbilia kuona makosa ya mwalimu na sio mema yake.
Mwalimu ni binadamu kama wengine.
Anaweza kushikwa na hasira za kupindukia kutegemea mazingira yaliyomkuta kama binadamu wengine.
Mwalimu anaweza kuamua vibaya na kufanya makosa kama binadamu wengine.
Hii ni sehemu ndogo tu ya kazi yake. Tusipende kuwahukumu walimu kama vile ni majangili .
Siamini kabisa kuna mwalimu anaamua maksudi kuwa yeye atakuwa anatoa adhabu za kupitiliza namna hii. Huwa hii inatokea kwenye mazingira fulani na kumsababisha ajisahau na kutenda hivi. Ni kama ajali tu zinazowakuta watu mbalimbali kwenye majukumu yao.
Siungi mkono matukio haya ya ukatili . Sisemi walimu waachwe ili waendelee kuwaumiza wanafunzi, LA. Tena napendekeza ikitokea uchunguzi umeonyesha mwalimu alidhamiria kumuumiza mtoto maksudi, sheria ifate mkondo na kutoa adhabu sitahiki. vinginevyo nashauri tu, ikitokea limemkuta mwalimu kwa bahati mbaya, tujaribu kuelewa chanzo na kumsaidia kujifunza kutokana na kosa.
Lakini hii tabia ya kuwabebea mabango walimu wanapokosea itakuja kusababisha matatizo makubwa hapo mbele. Inawezekana upo muda utafika walimu wataamua wasiwaguse wanafunzi wanapokosea ili kujiepusha na mambo kama haya. Naomba ujiulize vizuri, hivi siku moja walimu wakiamua kuwafumbia macho wanafunzi wanapotenda makosa tutapata watoto wa namna gani? Siku watawaona wanaenekeza mienendo mibovu wakaamua kukaa kimya tutajenga taifa la namna gani?
Ipo haja ya kutafuta mbinu mbadala za kuwasaidia walimu wetu. Ipo haja za kushirikisha wadau tofauti tofauti kusaidia walimu kulea watoto wetu vizuri.
Inabidi tutafakari kwa kina. Inatulazimu tubadilishe mtazamo. Mimi najiuliza, Ni lini mazuri ya walimu yatasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kama mabaya yao yanavyokolezwa? Je matokeo ya kuwaenzi walimu wetu yatakuwaje?
Naamini kabisa walimu wetu wanafanya mengi mazuri sana kila siku yasiyosimuliwa.
Wapo wanaotoa sadaka za muda wao bila malipo kuwasaidia watoto wetu.
Wapo wanaotoa sadaka za fedha zao kuwanunulia wanafunzi wanaotoka kwenye mazingira magumu mahitaji muhimu kutoka kwa mishahara yao midogo.
Wapo walimu wanatembea mwendo mrefu kuwatafuta watoro warudi shuleni.
Wapo walimu wanaotembea mtaani wakiwahimiza wazazi umuhimu wa elimu.
Wapo walimu wanaishi kwao na watoto wasio na pa kuishi.
Mifano ni mingi mno. Ni lini sasa matendo yao mazuri yatasambazwa kwenye mitandao ya kijamii?
Lini watapongezwa na kutiwa moyo kwa wanayoyapitia ili tu kuhakikisha watoto wetu wanafaulu?
Mwalimu ni mzazi.
Mwalimu ni mlezi.
Mwalimu ni ndugu wa karibu na watoto wetu. Mwalimu ni malighafi inayotengeneza kizazi cha kesho.
Kumbuka:
Mwalimu anakaa masaa mengi na mtoto kuliko hata mzazi. Mwalimu anatumia nguvu zake, muda wake, elimu yake, huruma yake na upendo wake kumlea mtoto. Mwalimu anajinyonya kupita kiasi ili wanafunzi wafaulu.
Mwalimu ni tunu katika taifa letu.
Tusim-beze, tusimdharau, tumsimfitinishe na tusimchukie.
Tumpende, tumheshimu, tumtie moyo. Zaidi tumsaidie pale anapokosea ajirekebeshi vizuri. Tukimtumia vizuri hakika tutavuna mema.
Wasiojua ugumu wa kazi na maisha ya kuwa mwalimu, waulizeni walimu.
Mwalimu sio adui. Mwalimu ni LULU.