Jamii inamchukuliaje Mwalimu?

Apr 29, 2019
36
25
MWALIMU NA JAMII

Kumekuwa na tabia za kumshambulia mwalimu kila mara anapofanya kosa hasa kwenye mitandao ya kijamii. Ni rahisi sana jamii yetu kukimbilia kuona makosa ya mwalimu na sio mema yake.

Mwalimu ni binadamu kama wengine.
Anaweza kushikwa na hasira za kupindukia kutegemea mazingira yaliyomkuta kama binadamu wengine.

Mwalimu anaweza kuamua vibaya na kufanya makosa kama binadamu wengine.
Hii ni sehemu ndogo tu ya kazi yake. Tusipende kuwahukumu walimu kama vile ni majangili .

Siamini kabisa kuna mwalimu anaamua maksudi kuwa yeye atakuwa anatoa adhabu za kupitiliza namna hii. Huwa hii inatokea kwenye mazingira fulani na kumsababisha ajisahau na kutenda hivi. Ni kama ajali tu zinazowakuta watu mbalimbali kwenye majukumu yao.

Siungi mkono matukio haya ya ukatili . Sisemi walimu waachwe ili waendelee kuwaumiza wanafunzi, LA. Tena napendekeza ikitokea uchunguzi umeonyesha mwalimu alidhamiria kumuumiza mtoto maksudi, sheria ifate mkondo na kutoa adhabu sitahiki. vinginevyo nashauri tu, ikitokea limemkuta mwalimu kwa bahati mbaya, tujaribu kuelewa chanzo na kumsaidia kujifunza kutokana na kosa.

Lakini hii tabia ya kuwabebea mabango walimu wanapokosea itakuja kusababisha matatizo makubwa hapo mbele. Inawezekana upo muda utafika walimu wataamua wasiwaguse wanafunzi wanapokosea ili kujiepusha na mambo kama haya. Naomba ujiulize vizuri, hivi siku moja walimu wakiamua kuwafumbia macho wanafunzi wanapotenda makosa tutapata watoto wa namna gani? Siku watawaona wanaenekeza mienendo mibovu wakaamua kukaa kimya tutajenga taifa la namna gani?

Ipo haja ya kutafuta mbinu mbadala za kuwasaidia walimu wetu. Ipo haja za kushirikisha wadau tofauti tofauti kusaidia walimu kulea watoto wetu vizuri.

Inabidi tutafakari kwa kina. Inatulazimu tubadilishe mtazamo. Mimi najiuliza, Ni lini mazuri ya walimu yatasambazwa kwenye mitandao ya kijamii kama mabaya yao yanavyokolezwa? Je matokeo ya kuwaenzi walimu wetu yatakuwaje?

Naamini kabisa walimu wetu wanafanya mengi mazuri sana kila siku yasiyosimuliwa.
Wapo wanaotoa sadaka za muda wao bila malipo kuwasaidia watoto wetu.
Wapo wanaotoa sadaka za fedha zao kuwanunulia wanafunzi wanaotoka kwenye mazingira magumu mahitaji muhimu kutoka kwa mishahara yao midogo.
Wapo walimu wanatembea mwendo mrefu kuwatafuta watoro warudi shuleni.
Wapo walimu wanaotembea mtaani wakiwahimiza wazazi umuhimu wa elimu.
Wapo walimu wanaishi kwao na watoto wasio na pa kuishi.
Mifano ni mingi mno. Ni lini sasa matendo yao mazuri yatasambazwa kwenye mitandao ya kijamii?
Lini watapongezwa na kutiwa moyo kwa wanayoyapitia ili tu kuhakikisha watoto wetu wanafaulu?

Mwalimu ni mzazi.
Mwalimu ni mlezi.
Mwalimu ni ndugu wa karibu na watoto wetu. Mwalimu ni malighafi inayotengeneza kizazi cha kesho.

Kumbuka:
Mwalimu anakaa masaa mengi na mtoto kuliko hata mzazi. Mwalimu anatumia nguvu zake, muda wake, elimu yake, huruma yake na upendo wake kumlea mtoto. Mwalimu anajinyonya kupita kiasi ili wanafunzi wafaulu.

Mwalimu ni tunu katika taifa letu.

Tusim-beze, tusimdharau, tumsimfitinishe na tusimchukie.
Tumpende, tumheshimu, tumtie moyo. Zaidi tumsaidie pale anapokosea ajirekebeshi vizuri. Tukimtumia vizuri hakika tutavuna mema.

Wasiojua ugumu wa kazi na maisha ya kuwa mwalimu, waulizeni walimu.

Mwalimu sio adui. Mwalimu ni LULU.
 
Ualimu ni wito na mteja ni mwanafunzi na kwasababu waalimu hawajitambui watz wanapiga wanafunzi na kuwatukana matusi machafu na kusahahu kuwa ao wanafunzi ndo wateja wao na ndo wanasababisha wao Kupata mshahara, hivyo nahitimisha kwa kusema waalimu wote watz hawajitambui isipokuwa wachache na hawazidi 10%
 
Respect kwenu maticha, nikimwangalia yule kid ana miaka 4 tuu anajua kuandika A up Z na kuhesabu mpk 100 hongereni. Ila kuwapiga watoto na kubaki hapo mmmh nawavua vyeo vyote nilivyowapa.
 
Ulichoandika ni kweli. Kama wewe ni mwalimu, na uliyoyaandika yanaakisi unachofanya, basi hongera sana, na Mungu akubariki na kukuzidishia baraka zake, upande vyeo na kuongezewa kipato mpaka wewe mwenyewe ushangae!

Watu wanalalamika kuona baadhi ya walimu wanawapa wanafunzi adhabu hatarishi; adhabu ambazo hazipo katika miongozo ya ualimu! Angalia ile adhabu ya kikatili aliyowapa watoto yule mwalimu mkuu wa shule fulani kule Kagera, ni sahihi? Kama aliyeadhibiwa kwa namna hiyo, angekuwa mwanao, ungeridhia?

Hatukatai watoto wetu kuadhibiwa pindi wafanyapo makosa, lakini wapewe adhabu iliyoainishwa katika miongozo ya elimu. Tunawathamini na kuwapenda walimu, maana tunajuwa wao dio huwatoa ujinga watoto wetu, na ni chimbuko la wataalam katika njanja mbalimbali.

Tunajuwa kuwa sio wote wenye matarizo haya, bali wachache ndio wanaowatia doa walimu wengine. Kuna mchangiaji mmoja amesema kuwa, ualimu ni wito, tunaamini walimu wanaowapa watoto wetu adhabu za kikatili namna hii, huenda waliingia kwenye fani hii kimakosa!
 
Baba yangu alikua Mwalimu, ila kupitia yeye nilitokea kuichukia sana kazi ya ualimu Mungu anisamehe, lakini simchukii mwalimu
Ulifanya maamuzi sahihi kuuchukia ualimu. Maana kwa nchi kama Tanzania, walimu wanachukuliwa kama malaika, na pia punching bags wa kila mtu. Kuanzia jamii, wanasiasa, wakuu wao, nk.

Kila mtu anajiona ana haki ya kumdharau na kumtukana mwalimu! Kila mtu anamuona mwalimu kama malaika! Yaani hakosei.

Kila mtu anamuona mwalimu ni maskini, failure (maana matokeo ya mtihani yakitoka mabaya, mzigo anaangushiwa mwalimu! Yakitoka mazuri, sifa zinaenda kwa mwanafunzi), ana madeni, na asiye na option nyingine yoyote ile katika maisha, nk.
 
Mtoa mada umeandika kitu kikubwa sana,..Changamoto iliyopo kwa sasa ni mitandao ya kijamii,jambo dogo linakuzwa na mitandao,..wale waliopata elimu miaka ya 2005 kurudi nyuma,tumepigwa sana huko mashuleni lkn hakukua na haya mambo ya matangazo na kelele nyingi,..na hii imetusaidia kuweka hivi tulivyo leo,ukiona mtu amekua bora,jua wazazi na walimu walifanya kazi kumuweka hapo alipo...kwa hali iliyopo sasa walimu kufungwa wasitoe adhabu,tutegemee kizaz cha hovyo miaka ijayo....walimu kwa sasa wamejikatia tamaa,anasema hata mtoto afanye kosa hawez mpa adhabu.
 
Ualimu ni wito na mteja ni mwanafunzi na kwasababu waalimu hawajitambui watz wanapiga wanafunzi na kuwatukana matusi machafu na kusahahu kuwa ao wanafunzi ndo wateja wao na ndo wanasababisha wao Kupata mshahara, hivyo nahitimisha kwa kusema waalimu wote watz hawajitambui isipokuwa wachache na hawazidi 10%
Mara wote mara isipokuwa!
Ebu weka sawa hapo.
 
Mtoa mada umeandika kitu kikubwa sana,..Changamoto iliyopo kwa sasa ni mitandao ya kijamii,jambo dogo linakuzwa na mitandao,..wale waliopata elimu miaka ya 2005 kurudi nyuma,tumepigwa sana huko mashuleni lkn hakukua na haya mambo ya matangazo na kelele nyingi,..na hii imetusaidia kuweka hivi tulivyo leo,ukiona mtu amekua bora,jua wazazi na walimu walifanya kazi kumuweka hapo alipo...kwa hali iliyopo sasa walimu kufungwa wasitoe adhabu,tutegemee kizaz cha hovyo miaka ijayo....walimu kwa sasa wamejikatia tamaa,anasema hata mtoto afanye kosa hawez mpa adhabu.
Ni mwendo wa kulinda zone yako tu.
Mtoa mada hajatetea wala kuunga mkono ukatili,kaweka mpira kati kwa ufasaha kabisa.
 
Mwalimu ni “kuku mweupe” ukianzia hapo utajijibu maswali mengi mno yakiwamo ya Mpwayungu village linakoendaga li-mshikamano safaris.
 
Back
Top Bottom