Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Thank you

We all know hamna watu wanapeta sana kwenye maisha kama wale ambao baba na mama wote wako vizuri kiuchumi
Hapa sikuelewi, baba na mama wote wapo vizuri kiuchumi. Wanaishi separate?
 
Hujui family structure. Hujui mpangilio wa malezi. Na hayo unayoshangaa eti yanatokea wapi ni kukimbia kivuli chako
 
Asikudanganye mtu
Furaha ya ndoa kipato kiwepo muweze kumudu maisha...
Na kuna kukosea kuoa na kuolewa na ndoa ni kifungo

Ukiwa umekosea utabaki huna furaha ama utaendelea na mengine ktk maisha yanayokupa raha?..
 
Hujui family structure. Hujui mpangilio wa malezi. Na hayo unayoshangaa eti yanatokea wapi ni kukimbia kivuli chako

Next time jifunze mwenyewe 'secure attachment' .bora uwe ignorant but uko willing kujifunza,kuliko hujui na hauko willing kujifunza..disaster!
 
Uelewa wako ndio umefikia mwisho, we dont have to agree on everything. Wewe una malezi yako so endelea hivyo. Mambo ya kuchukia wanawake eti kwa kukataliwa san na kukejeliwa ni ramli za kichawi ambazo hazinihusu, nimevuka huo upuuzi na siwezi kujisifia mambo machafu. Hao unaowawazia hivyo ni wale walioishi maisha ya kihuni na kuhusiana na makahaba, nawezaje kujisifia ujinga huo?

I am happy kwa jinsi nilivyo hata kama hufurahii, but FACT: wanawake mmeahama kwenye nafasi zenu na kujiweka kwenye majukumu ya wanaume.
 
Hii mambo ya kutaka kuwa sawa na wanaume mimi inipite tuu kwa kweli.
Niacheni mimi niendelee kundeka na kudekezwa, ndio raha ya uanamke wangu... nyie endeleeni kutunishiana misuli na wanaume muone mtakavyoachiwa majukumu ya kiume....
Halafu muanze kulialia wakati mmeyataka wenyewe
 
Truee
Hata Rebeca 83 amesema the same thing

Huyu kijana mwenye mada ana bias flani hivi abnormal unaiona kabisa kwny mada zake

Na mada zake zote ni about women...women this women that..
U can tell the frustration...

Ni km vile binti ambae mada zake mda wote ziwe about men..tena in a demeaning tone..utapata msg flani..ana maumivu abt men..

Nyenyere soothe ur soul bruhh..ts the soul that needs a surgery
 
Asikudanganye mtu
Furaha ya ndoa kipato kiwepo muweze kumudu maisha...
Na kuna kukosea kuoa na kuolewa na ndoa ni kifungo

Ukiwa umekosea utabaki huna furaha ama utaendelea na mengine ktk maisha yanayokupa raha?..
Umesema kweli, ukikosea kuoa utajuta hasa kama ni ndoa ya kikristo, ndio maana Biblia inasema mwanamume AKIPATA MKE apata jambo jema na atapata kibali kwa Mungu. Sio kila mwanamke ni wa kuwa mke na sio kila mwanamume ni wa kuwa mume. Hivyo basi mke bora atatoka kwa Bwana tu, ndivyo maandiko yasemavyo, nje ya hapo ni bahati nasibu.

Pia hoja ya kipato si kweli, kwani tunaona ndoa za matajiri zikiyumba kila siku na kuwa kama jehanamu ya moto. Kupata suluhu ya hili rejea hapo juu.
 
Wala hata siumizwi na mwanamke kuona mwanaume ni kitu cha ziada, kama kuna chochote kinachoniumiza basi ni aina ya jamii tunayoijenga kutokana na athari zitokanazo na maamuzi ya dizaini hiyo.

Mimi ni sehemu ya jamii na kukemea/kusema jambo lolote ninaloona sio zuri kwenye jamii yetu ni jukumu langu. Mimi Sio leftist ambaye kila kitu kinachukulia ni liberty.
 
Wewe umeelewa mada kweli wewe? Au umeisoma huku tayari una konyagi kichwani?
 

Kweli kabisa
Mama una saikolojia kalii
Ukisoma utaona his 'wishful thoughts' anazotamani ingekua hivyo kwenye jamii...uhalisia mtaani hauko hivyo....dunia tambara bovu na Mungu anaona sio kwamba haoni
Ss anateseka na conservatism ya kufikirika

Mawazo yake yaweza kuwa mazuri kiasi flani ila utekelezaji u need to keep an open mind dunia ya leo..dnt be rigid
 
Ni sawa
Ni kujitahidi kuangalia pande zote pia

Kwanini wanawake wana bidii sana miaka hii?..
Ni simply bcz wanawake ni viumbe wa bidii sana ama there is relief in independence flani hasa ya kiuchumi? Ama wamejifunza nini kutoka kwa wanaume?..
Mambo ni mengi mda mchache
 
Kwa kua inatambulika ndoa nzuri ni bahati nasibu ndo mana watu wa jinsia zote me na ke wanajikita ktk kujiboresha ktk nyanja zote ama nyingi za maisha mana ndani ya nyumba hamtatizamana th
Mtaendelea na maisha na shughuli na interest zenu nyingi
Zipo za kufanya as an individual na zipo za kufanya as a couple
Ndoa isnt the ultimate..keep an array of varities of things to make you happy..perhaps Mungu kakupangia yako itanoga baada ya mwaka wa 3 /5 au wa 10😅😅 u never knoww..its a process
 
Nioneshe hiyo self-contradiction ilipo kwenye maalezo yangu.

Money is Power ndio hatukatai, lakini je unaitumiaje hiyo power? Hii Ndio hoja kuu iliyopo mezani.

Hata hao wanaume wanaotumia pesa/mali kuwanyanyasia wanawake ni wanachangia kuiharibu jamii.

Halafu nyie wanawake hasa mliochangia huu uzi naona mna ulimbukeni sana, nyie ni ma HEDONISTS mnaoamini maisha ni hela tu na ukishakuwa nazo basi hata mambo mengine ni ya ziada tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Ndio maana mpaka mnaona mnaweza kuwanunua wanaume kisha mkawatumia mtakavyo.
 
Hasty conclusions and generalizations...wengi wetu ni waelewa wa uhalisia ktk jamii

Kama ni watu wanaoamini maisha ni hela tu ni wanaume...
 

Hilo suala la wanawake kuwa ni watu wa bidii liko conspicuous wala sio hoja yenye uzito sana hapa.

Hiyo economic independence ndio ajenda kuu kwa maana ya athari na faida na namna ya kuweza kuziepuka hizo athari.
 
Kama ni watu wanaoamini maisha ni hela tu ni wanaume...

Hell no, wanawake wanaamini hela ndio kila kitu kwenye maisha yao.

Mnaamini hela ni mbdala wa mwanaume na chochote kimuhusisho mwanaume.

Ni mara nyingi sana utawaskia wanawake wakisema "nina kazi yangu inaniingizia kipato kinachotosheleza mahitaji yangu yote, sasa mwanaume wa nini?"

Sasa ni mara ngapi ngapi umewahi kuskia mwanaume akiwa na hela anatamka maneno kama haya!? Kwamba akiwa na hela basi hata umuhimu wa mwanamke kwake unapungua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…