Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Jamii imempora mwanamke nafasi yake

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,842
Reaction score
10,765
Wakuu niwatakieni weekend njema na yenye amani tele. Leo nitaandika kifupi tu kwani wengi wamekuwa wakilalamika mada ziwapo ndefu. Tuendelee na mada:

Mwanamke na mwanamume wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti. Utofauti huo haufanyi mmoja awe inferior kwa mwenzake bali wawe umoja ili kutimiliza malengo ya uwepo wao duniani ambayo lengo kuu ni kuendeleza kizazi (procreation). Nasema wameumbwa tofauti kwa malengo tofauti kwa sababu zifuatazo:

Maisha ya kijamii
Mfumo wa maisha wa mwanamke umetofautiana kwa kiasi kikubwa na mwanamume. Mwanamke amepewa maisha ya kuhusiana na jamii inayomzunguka, ndio maana utaona wanawake wanakuwa na makundi mtaani, kwamba huyu ni rafiki yangu wa karibu huyu sio. Wanakutana kupeana simulizi za kuhusu maisha ya wengine, nani kapigwa na mume, nani hajui kuvaa, nani kanyang'anya mchumba wa mwingine n.k. Kama huamini fuatilia aina ya maongezi ya wanawake wote bila kujali elimu zao. Hili si baya hata kidogo, ndivyo walivyoumbwa. Mwanamke ni kiumbe anayestahili kuwa kwenye mazingiri ya nyumbani kwake kwa muda mwingi zaidi, ni mlezi.

Mwanamume kwa upande wake ameumbiwa maisha ya kutangatanga. Maongezi yao mengi ni kuhusu nani kapataje utajiri, nani kamtapeli mwingine, nani kavusha mzigo nje ya nchi n.k. Mwanamume ni mtafutaji, kwa ajili ya mke na watoto, tena kwa ajili ya wazazi. Mwanamume ni mlezi wa jamii kwa ujumla wake na ndio maana akili yake imeumbwa kufikiri namna ya kupata mali kwa ajili ya familia. Hivi umewahi kujiuliza ni kwa nini hatuna majambazi wanawake?

Uumbaji
Mwanamke na mwanamume hushiriki uumbaji kwa kuunganisha mbegu na yai. Kwa sababu mwanamke sio mtafutaji kiasili, yeye amewekewa mfuko wa uzazi na mfumo wa uleaji wa mtoto mpaka awapo mtu mzima. Mwanamume hajapewa mfumo huo ili awe mtafutaji, amepewa kuwa na nguvu zake mwaka mzima apate kumtunza mke na familia. Kila mfumo uliwekwa kwa kusudi lake.

Jinsi jamii ilivyopora nafasi ya mwanamke
Mapinduzi ya wanawake kuingia kwenye majukumu ya kufanya kazi yalianza wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Hapa kuna hoja nyingi mno lakini siongelei kwa sasa kwa kuogopa kuifanya thread kuwa ndefu. Lakini niseme tu, tuchunguze mfumo wa elimu sasa na kabla.

Zamani mtoto wa kike alipewa elimu yenye ubora wa hali ya juu, iliyomjenga vema kutambua majukumu yake. Shule yao kuu ilikuwa ni wazazi wake ambao aliumia muda mwingi kuwa nao nyumbani. Elimu hii ilimfanya kuwa mwanamke bora aliyejitambua nafasi yake na majukumu yake pia. Mwanamke ni mlazi wa familia, hivyo elimu ililenga kumjengea uwezo kwenye eneo hilo.

Kwa mtoto wa kiume elimu yake iliendana na majukumu yake pia, utafutaji. Kwa kuwa kiasili mwanamume ni mtafutaji, jamii ilijikita kumpatia elimu itakayomwezesha kutafuta mali ili kumudu majukumu ya kumtunza mke na watoto. Ndio maana zamani mtoto wa kiume alipewa nafasi kubwa kusoma elimu ya kizungu (mashuleni na vyuoni). Wapi mambo yalipobadilika?

Pale dunia ilipobadili mfumo na kuanza kuwajengea mtazamo wanawake na jamii kwa ujumla kuwa mwanamke anastahili kuwa na kipato chake, asiwe tegemezi kwa mume (hoja inayoondoa kabisa maana ya ndoa na majukumu yaliyomo humo), ndoa zikatazamwa kama gereza la mwanamke. Kwamba mwanamke anapoingia kwenye ndoa kwa mtazamo wa zamani ananyimwa uhuru wa kujitafutia kipato chake mwenyewe. Ndipo likaja swala la elimu.

Mwanamke akatakiwa kupatiwa elimu sawa na mwanamume, mambo ya haki sawa. Hili lilikuwa jambo jema kwa kulitazama kwa juu juu, lakini ukiangalia kwa undani, mwanamke kupatiwa elimu ya utafutaji ni kumwondoa kwenye nafasi yake kama mke. Elimu iliyolenga kutafuta mali tangu awali ilimlenga mtafutaji, mwanamume. Sasa badala ya dunia kuleta elimu inayolenga kuboresha nafasi ya mwanamke, ikaleta elimu inayolenga kumfanya mwanamke awe sawa na mwanamume. Mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanamume na ndio maana kinachotokea ni kuigiza kuwa kama mwanamume.

Wanawake wamekuwa wakiishi maisha ya uigizaji, na hii imewafanya kutokujitambua, kutokujua thamani yao na nafasi yao katika jamii. Jamii imemshusha hadhi mwanamke na kumfanya kama mwanamume, isipokuwa tu ameshindwa kabisa kuenenda kwa jinsia hiyo. Matokeo yake wanawake wamegeuzwa kuwa chombo cha starehe, matangazo ya biashara. Mwanamke ambaye zamani alikuwa akiishi na jamii iliyomzunguka huku akijiweka kumliwaza mume, sasa anaishi na jamii za mbali kwa sababu ni mfanya biashara ama mfanyakazi. Zamani alivaa kuteka hisia za mume leo anavaa kuteka hisia za watu wa nje kwa sababu ndiko anakotumia muda wake mwingi. Zamani alikuwa na marafiki waliomzunguka anapoishi leo ana marafiki wa mbali, ambao wana nafasi ya kumjengea mtazamo tofauti.

Mwanamke ameondolewa kwenye nafasi yake ambapoalikuwa chombo cha thamani kubwa na sasa amegeuka mshindani na wanaume. Jamii imemshusha hadhi mwanamke naye amefumbwa macho kuikubali hali hihyo, ndio maana anaishi maisha yasiyo na malengo na matokeo yake ni kuishia kwenye majuto makuu.

Najua mada kama hizi ni ngumu lakini lazima tuangalie ni wapi tulipojikwaa. Feminism ilipaswa kuboresha majukumu ya mwanamke, badala yake imefanya mwanamke awe kama mwanamume.
 
Kushushwa hadhi kutoka kumvutia mume kwenda kuvutia watu wengi.

Tatizo wanaume mnapenda kuwasemea wanawake.
Wana hadhi watu wanaolala wanaletewa chakula mezani, wana uhuru wa kusema, wana uhuru wa kuchagua wa kuishi naye wana uhuru wa kuchagua wafanye nini, wakae wapi. Unakuwaje na hadhi kama wewe ni wa kumridhisha mtu huyu halafu yeye akufanyie apendavyo na si upendavyo. Huu ni utumwa.

Hiyo hadhi unayosema wanawake hawana hata sasa. Na wakiwa kazini adha zao zinapungua kulinganishwa na wengine. Wanapata sauti. Na hiki ndicho kilichokutuma, sauti zao huko zinakutatiza maana umelelewa ukijua hawa hawana uhuru huo.

Makahaba wapo zama zote vivyo hivyo na wake.

Tukifanya kazi hatugeuki kuwa wanaume. Bado sisi ni wanawake. Bado adha za kike tunakutana nazo kama kawaida. Bado wengi hawana uhuru huo, wamelelewa kuwa wao hawatakiwi kuwazidi wanaume.

Wanaume mngependa tubaki nyumbani ingewezekana maana bado hiyo nguvu mnayo tatizo hamuitumii. Ingawaje wengine wameshajitengenezea tena ubwana kwenye mfumo huu mpya.
 
Hicho unachokisema ndio ukengeufu wenyewe. Jukumu la mwanamke ni kuzaa na kulea, hizo kazi mmepewa na wajanja na iko sababu ya kibiashara na kimapato ya serikali. Mwanamke anagawana majukumu na mune, mmoja nyumbani mwingine kazini. Ndio maana watoto wa siku hizi hawana malezi bora, kwa sababu mama anarudi saa nne usiku na baba pia. Wanawake mmejitwisha jukumu la wanaume, mkaacha jukumu lenu.

Kwamba wasio na kazi wana maisha mabaya si kweli, inategemea unatazasha vipi maisha. Wanawake wasio na waume nilioongea nao mimi hawana furaha wala amani hata kama wana kazi. Kazi sio kila kitu kwa mwwnamke ila dunia imejaribu kumwaminisha hivyo. Kwa mfumo sasa hakuna mwanamke tena, wote ni watafutaji tu. Mwanamke halisi atawazia malezi ya famikia bora kuliko kutafuta mali binafsi ndani ya ndoa.

Ukahaba kuwepo tangu kale ni kwa sababu wako wachache ambao hawakuzingatia maonyo. Na hiyo sio sababu ya kuendeleza ukahaba, misingi ya zama hizo haikushabikia ukahaba bali ilipinga kabisa, hivyo kauli yako ni mfu. Wanawake wengi wanaji expose kwenye system ya elimu, wanajikuta wameingia kwenye vitendo vya ukahaba kwani wanaanza kujitegemea wakiwa bdo hawako tayari.
 
Zama na zama wanawake wameshiriki kwenye shughuli za uchumi za familia kwa sura tofauti.
Zama zile bibi zetu walishiriki shughuli za kilimo za familia, hawakwenda vitani labda.
Na tatizo la wanaume wafanyapo kazi ambayo mwanamke hafanyi huwadunisha wanawake au kudunisha kazi wazifanyao wanawake.
Kama wangaliends kazini kitumike kwa ajili ya familia na si kwa maslahi binafsi na kutumia kama chambo cha kumnyanyasia hakuna ambaye angetaka hizi kazi za stress.
Kwa sababu wanawake ni viumbe watu wenye akili hii ni sehemu ya mapambano kulinda vinasaba na uwepo wetu duniani.

Na hiki kinachoendelea hapa ni stress za mfumo unaopingwa kama mfa maji kutapata.
Nashauri wanaume wajipange kuwaandaa vijana wa kiume maana sasa ulimwengu unampendelea mwanamke na kama ilivyo kwa wanaume sasa mambo yanaweza kubadilika.

Mwanamke hajawahi kudharaliwa, mabadiliko yamekuja kwa kufundishwa kuwa ananyanyaswa na kunyimwa haki. Nasikitika hicho unachokisema kuwa mfa maji haachi kutapatapa huko marekani na ulaya wameanza kubadilika. Huu mfumo mnaoushabikia unaelekea kushindwa vibaya.

Mwanamke kushiriki shughuli za kiuchumi ni sahihi, lakini tangu mwanzo alishiriki shughuli ambazo hazimfanyi awe mtembezi. Alifanya shughuli za kifamilia kama muda mfupi shambani, muda mwingi malezi ya watoto. Sio aishi mwanza biashara Dar na Mtwara. Matokeo yake ni kujaz machhokoraa na mateja mtaani.

By the way ni dhambi kubwa kutolea watoto katika maadili, jukumu la malezi ni la mwanamke, naye ameliacha na kukimbilia majukumu ya mwanamume. Ni kutokuwa na ufahamu mzuri kushabikia dhambi hii
 
Nimesikitishwa sana na hiki kipande cha bandiko lako inaonesha wazi kabisa haujui kabisa athari za huu mfumo unaompedelea mwanamke.

Ndugu huu mfumo unaofanya dunia ya sasa kumpendelea mwanamke sio wa kushabikia hata kidogo, maana athari zake ni kubwa mno na zinatulenga jinsia zote mbili.

Ulimwengu wa sasa unampendelea zaidi mwanamke kwa kumpa umuhimu mkubwa kuliko jinsia nyingine. Kuna taasisi nyingi sana duniani zimeanzishwa kwa ajili ya kushughulika na masuala ya wanawake, sheria zetu zenyewe zina mpendelea zaidi mwanamke na hata ukija kwenye jumuiya kubwa za kimataifa zinalinda sana maslahi ya wanawake kuliko wanaume mfano kama UN kuna departments zaidi ya 8 ambazo ni mahususi kwa kushughulika na women issues lakini hakuna hata moja inayoshughulika na wanaume.

Kutokana na hali hii ya mwanamke kupendelewa na kuaminishwa kuwa anaweza kuwa sawa na mwanaume imepelekea kutokea kwa gender isolation.

Siku hizi ni matukio ya wanaume kusingiziwa kesi za ubakaji na wanawake yamekuwa mengi sana, na sababu kuu hasa ni huu upendeleo wa kijinsia tulionao kwenye dunia ya leo.

Na hii imepelekea wanaume kutengeneza distance baina yao na wanawake kutokana na hofu pamoja na kutoona hawana umuhimu kwa wanawake. Yaani imefikia hatua mwanaume anaona yuko salama zaidi asipojihusisha na mwanamke kwa jambo lolote lile.

Ni kwa bahati mbaya sana waathirika wakuu wa hii gender isolation ni wanawake. Na tayari athari hii imeshaanza kuonekana huko ambako haya mambo yameanzia.

Nchini Sweden matukio ya uhalifu ikiwemo ubakaji yamekuwa mengi sana miaka hii ukilinganisha na miaka ya nyuma. Na waathirika wakuu wa matukio haya ni wanawake.

Mwaka juzi wanawake wa Sweden waliandamana wakiwalaumu wanaume wa nchi hiyo kwamba wamejitenga sana na ndio maana wanawake wengi wamekuwa wakibakwa na kufanyiwa matukio mengine ya kihalifu.

Kwa madai yao ni kwamba endapo kama wanaume wa kiswedish wangekuwa karibu na wanawake basi kusingekuwepo na matukio ya ubakaji kwa kiasi kikubwa hivi.

Cha kushangaza hao hao wanawake ndio chanzo cha wanaume kujitenga na wao mpaka wanakutwa na hayo maswahibu.

Kuna tukio lingine lilitokea huko Italy miaka ya nyuma kidogo linaloonesha jamii yetu imefikia pabaya sana kutokana na huu mfumo unaoufurahia na kuupigia debe. Ngoja nikuwekee kipande cha hiyo habari..

PASSENGERS of the Costa Concordia, the cruise ship that sunk off an Italian island on Friday [13th January 2012], told The Daily Mail that in the chaos after the ship was wrecked, men rushed for the lifeboats and gave no priority to women and children.

As she [one of the survivors ] waited for a flight home from Rome, grandmother Sandra Rogers, 62, told the Daily Mail: ‘There was no “WOMEN and CHILDREN FIRST” policy. There were big men, crew members, pushing their way past us to get into the lifeboats. It was DISGUSTING.’

Kwa kuangalia hiyo scenario hapo utaona wanaume wa leo sio wale wa zama zile za TITANIC, wanaume wa siku hizi hata wao wamejifunza kwenda na huu mfumo wenu mpya, yale masuala ya wanawake na wanawake kwamba ndio wanapewa kipaumbele kwenye kuokolewa pale yanapotokea majanga hayapo tena. Maana hata wanawake pia wanaweza kufanya chochote ambacho wanaume wanafanya ikiwemo kujiokoa wenyewe kwenye ajali.

Hivi umewahi kujiuliza siku Ikitokea vita ya tatu ya dunia hali itakuwaje?

Wewe unahisi kwa huu utengano na ubinafsi tuliojengewa na huu mfumo wenu wa haki sawa wanaume watakuwa tayari kujitoa kwa ajili ya wanawake kama walivyo fanya miaka ya nyuma??

Dunia ya sasa inajaribu kukuaminisha kwamba huko sawa na mwanaume kwa kila kitu, lakini hicho kitu hakipo na wala hakitakuja kutokea. Uking'ang'ania sana utajikuta wewe ndio unayepoteza pakubwa.

Tunaweza kuandika maelezo mengi hapa ukaona kama ni stress tu ndio zinazoandika lakini nikwambie kwa mawazo hayo uliyonayo unastahili kupewa pole sababu unashabikia na kufurahia kitu usichokijua madhara yake.
 
Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na mawazo ya huyu mwanamama.
 
Nakubaliana na wewe upendeleo huu hauna majibu mazuri kwa jamii. Athari zake ziko wazi na gharama kubwa.

Wanawake wamejiongezewa majukumu mengi na sasa jamii inakosa mwelekeo.
Kama hoja ya mtoa mada jamii imempora mwanamke lazima tukubali ulimwengu huu wanadamu, mwanamke na mwanamme wanategemea na wanashirikiana kwa usalama wa jamii ya viumbe wanadamu katika hii dunia na vile vile kama jamii ndogo ndogo.
Kukiwa kuna kuelemea sehemu fulani iwe kwa heri au kwa ubaya lazima majibu yake utayaona.

Haihitaji picha au maelezo kujua mwanamke anadharaulikaje katika jamii zetu. Tena hii mifumo pengine ina mbeba lakini yale yasiyoandikwa yanayotokea ndo uzoefu wa unyanyasaji wanaopitia wanawake. Nyuzi za jamii forums zinazomzungumzia mwanamke nyingi ziko wazi tu, kudunisha na kubeza wanawake.

Kama mwanamke niliyebahatika kusoma naona mifumo ya sasa ina fursa nzuri tu kwa ustawi wa jamii ya kike lakini bado hatufikii huko. Kwa nini hatuifikii huko ni majibu ya hoja dharili zilizopandikizwa kwa wote tangu tupo wadogo hizo fursa zinakuwa kaa la moto.

Jana tu kuna mtu amenijibu humu vile tunatoa damu kila mwezi hatuwezi kufanana na mwanaume. Hoja mezani ilikuwa umalaya, haihitaji degree kujua kuwa na mahusiano na watu wengi nje ya utaratibu wa jamii au dini ni umalaya. Ni wanaume tu wenye uwezo wa kutamka hilo kwa mwanamke hata anayemdhani tu.
Wanawake wanajua wanaume malaya na tunazungumza lakini utamkapo hilo kwa mwanaume ni unakaribisha balaa.

Juzi juzi baba yangu amenitamkia kuwa alinisomesha nisiwe mtumwa. Naamini wengi wanaonekana hivi wakiwa nyumbani wanalea. Hebu niambie ni nani anayependa utumwa.

Hii hali mahangaiko ya uchumi ni maumivu kwa wanawake ndo maana wengi wanatamani kupata wenzi walofanikiwa wapunguze stress za kuwazia uchumi huku akipata hadhi kwa jina la huyo mwenzi wake.
Wako wengi hutamka kama mume akiweza kutuhudumia vizuri mimi sina haja ya kazi. Wako wengi pia waliokubali haya na matokeo yake hawakujaliwa.

Tukubali mifumo ya upendeleo si salama kwa wote. Na kwa hili jamii zikubali kujipanga kuondoa athari za muda mrefu za pande zote na kuchagua mistakabali yenye mizania.

Ukiniambia leo tufanyeje sasa kufikia hayo. Sina majibu kwa kweli.
Na binafsi najitahidi nifanye sehemu yangu tu. Na nafahamu wote tumeathirika na wengine wana chuki za wazi kuona wafanyao tofauti, hili ni nje ya uwezo wangu.
 
Inapendeza kama hata wewe unafahamu fika kwamba huu mfumo tunaoambiwa kwamba umeletwa kwa ajili ya kuwasaidieni nyie wanawake kwa namna jinsi unavyo kuwa practiced unaleta athari nyingi kuliko faida kwa walengwa.

Athari zake zinaweza zisionekane kwa urahisi sasa hivi lakini tukaziona hapa baadae au hata kwenye matukio mbali mbali mfano kama kwenye ajali kama ulivyo ona kwenye comment yangu iliyopita.

Sasa nije kwenye hiyo kauli ya baba yako aliyokwambia juzi.

Kwa kuangalia tu hii kauli baba yako Nathubutu kusema yeye ni aina ya wazazi ambao wameshiriki kikamilifu kuharibu kizazi cha wanawake wa sasa.

Baba yako anaamini mwanamke asiyesoma ni lazima atakuwa ni tegemezi tu kwa mwanaume na huo utegemezi yeye anauona ni utumwa, sasa hili asiingie kwenye huo utumwa basi lazima asome sana...INASIKITISHA SANA KWA KWELI.

Naamini kabisa tangu udogoni kwako amekuwa akikujengea hii mindset kwamba kusoma=kuepuka manyanyaso ya mwanaume na mpaka sasa hivi umekuwa nayo na hujawahi kuona tatizo kwenye hilo.

Mbali na huu mfumo tulionao wazazi pia wamechangia sana kuwaharibu wanawake hasa nyie wasomi kwa namna jinsi walivyowalea.

Mzazi anampa binti yake elimu hili aje aitumie kama mbadala wa kuishi bila mwanaume. Yaani elimu inakuwa ni replacement ya mwanaume maishani mwake.. Very pathetic mindset.

Umewahi kujiuliza ni kwanini wanawake wengi wasomi ndoa zinawashinda? Sababu moja wapo kubwa ni kuwa na hii mindset waliojazwa na wazazi wa aina ya baba yako.

Wanawake wengi wasomi wawapo ndoani wakikutana na changamoto hawaitumii elimu yao kama nyenzo ya kutatua changamoto hizo na badala yake elimu hiyo wanaifanya plan B(mbadala wa mume baada ya kuachika) pale mambo yasivyoenda jinsi wanavyotaka wao.

wanawake hao wasomi ni rahisi sana kusema maneno kama "tuachane" "usinibabaishe" "ninaweza kuishi bila wewe" hata pale changamoto ndogo tu inapojitokeza. Yote hii ni kwa sababu tu wanaweza kujitegemea kupitia elimu zao na wameshaukimbia ule utegemezi(utumwa) na hii tafsiri ya neno utumwa kwao inaenda mpaka kwenye utii.

Elimu zao zinawaondolea ile haiba na nafasi ya mwanamke kwa mwanaume na kujikuta anakuwa mshindani badala ya msaidizi ndio maana ni ngumu sana kwao kuwa na ndoa thabiti, sululisho pekee la kukabiliana na changamoto za ndoa huwa wanaona ni kuvunja ndoa.

Nadhani umewahi kuona comments zangu humu nikisistiza kuwa mwanamke msomi hafai kuwa mke. Ninasema vile kwa kumaanisha wala sio maigizo.

Na ni kweli hamfai kuwa wake.

Angalia mfano kama wewe hapo tayari sasa hivi unaona eti mwanamke anayefanya kazi ya kulea tu watoto nyumbani huyo ni mtumwa!!! How?

Kwa maana nyingine unaniambia kwamba mwanamke anayechakalika sawa na mwanaume huyo ndio kajikomboa toka utumwani kitu ambacho si sahihi kabisa.

MWENYEZI MUNGU hakuwa mjinga kumfanya mwanamke kuwa tegemezi wa mwanaume na kumuepusha na shuruba zote za kazi kama ambavyo wazazi wa siku wanavyowaaminisha nyie mabinti.

Haya sasa hivi mmetoka kwenye huo utumwa mmeingia kwenye kushindana na wanaume Nadhani athari zake wewe mwenyewe unaziona.

Kushindana kwenu na wanaume kumepelekea wengi wenu kuishi bila wenza na mnajikuta mna majukumu mengi sana ya kuyakabili kuliko hata wale mnaowaona wako utumwani(tegemezi).

Na majukumu hayo mazito mliyojipachika yanawaleteeni athari za kiakili kwanzia nyie mpaka kwenye familia zenu.

Kuna observation moja ilifanyika nchini UK watoto waliolelewa na single parents na wale waliolelewa na wazazi wote wawili walikuwa wanaulizwa kama wanatamani kuishi maisha wanayoishi wazazi wao pale watakapokuwa watu wazima.

Karibia watoto wote wanaolelewa na single parents walisema hawatamani kabisa kuishi maisha ya wazazi wao, kwa sababu wazazi wao(single parents) wana struggle sana namna ya kubalance familia na careers zao, na hivyo watoto hao kujikuta muda mwingi wanauokosa ule ukaribu wa mzazi.

Na hii ni ukweli mtupu single mothers wengi(ambao hawako tena utumwani) hawana muda wa kukaa na familia sababu ya kukimbizana na majukumu.

Haya yote yameletwa na huu mfumo unaoshabikiwa na wengi ambao umefanya wengi kuwa na mentality kama hii aliyonayo baba yako ya kuamini utegemezi ni utumwa.
 
Kuhusu ndoa na utumwa.
Ni mambo ya wazi. Wazazi wanawaandaa watoto wa kike kwa mawili either kukubali utumwa au kuukataa.
Hapa ndo unakuta tofauti. Wangu alinilea niupunguze somehow. Na nimesikia hilo directly nina miaka kwenye ndoa tayari na yeye maneno yake na matendo yake yanashawishi ujipange.

Kuhusu ndoa na single mother,
Mwanzoni hata mimi niliamini kama uaminivyo. Nikiwa binti mdogo mara nyingine fursa ya elimu niliona kama kikwazo kufikia ndoto za mama na bibi zangu kuwa mke. Mara nyingi nilitamkiwa kuwa naweza nisiolewe na hata kuna classmate walisema hawawezi kuoa mwanamke kama mimi. Tuliambiwa watu wa profession yangu hawaolewi au hawadumu. Wakati huo nikihisi ndoa kwa wale walomaliza darasa la saba ipo tu na hakuna shida.

Uzoefu wangu sasa, kati ya wahadhiri wetu wa kike asilimia 80 wana ndoa.
Wanawake darasani kwetu chuo wamebaki asilimia 19 na wengine tayari wana pete tunasubiri harusi.
Huko uraiani kuna wanawake hawajasoma wengi tu na hawana ndoa.
Kuna wengine na kusoma kwao hata mimi nisingemshauri kaka angu aoe hao. Wamepungukiwa sana kwenye tabia.

Nakubali changamoto ya malezi itakuwepo tu lakini elimu kwa zama hizi (labda huko nyuma) si kigezo cha mwanamke kukosa ndoa maana wanaume sasa wanachagua wake wanaokaribiana nao kielimu.

Wanawake tufanye kazi tu jamani maana tusipofanya hakuna rangi tutaacha kuona. Kama mnavyojua wanaume wengi wamekuwa mafurushi hivyo za kuambiwa changanya na zako.

Lakini ktk kufanya kazi huko tusisahau tu kuwa watoto wetu wanatuhitaji sana.
Hakuna mfumo usio na faida ukakosa hasara.
 
MAJUKUMU ya asili usiyasahau hayo ndio namba moja kwako mengine ni ziada
 
Kuhusu ndoa na utumwa.
Ni mambo ya wazi. Wazazi wanawaandaa watoto wa kike kwa mawili either kukubali utumwa au kuukataa.
Hapa ndo unakuta tofauti. Wangu alinilea niupunguze somehow. Na nimesikia hilo directly nina miaka kwenye ndoa tayari na yeye maneno yake na matendo yake yanashawishi ujipange.

Kuhusu ndoa na single mother,
Mwanzoni hata mimi niliamini kama uaminivyo. Nikiwa binti mdogo mara nyingine fursa ya elimu niliona kama kikwazo kufikia ndoto za mama na bibi zangu kuwa mke. Mara nyingi nilitamkiwa kuwa naweza nisiolewe na hata kuna classmate walisema hawawezi kuoa mwanamke kama mimi. Tuliambiwa watu wa profession yangu hawaolewi au hawadumu. Wakati huo nikihisi ndoa kwa wale walomaliza darasa la saba ipo tu na hakuna shida.

Uzoefu wangu sasa, kati ya wahadhiri wetu wa kike asilimia 80 wana ndoa.
Wanawake darasani kwetu chuo wamebaki asilimia 19 na wengine tayari wana pete tunasubiri harusi.
Huko uraiani kuna wanawake hawajasoma wengi tu na hawana ndoa.
Kuna wengine na kusoma kwao hata mimi nisingemshauri kaka angu aoe hao. Wamepungukiwa sana kwenye tabia.

Nakubali changamoto ya malezi itakuwepo tu lakini elimu kwa zama hizi (labda huko nyuma) si kigezo cha mwanamke kukosa ndoa maana wanaume sasa wanachagua wake wanaokaribiana nao kielimu.
Wewe tayari inaonesha wazi mind yako iko crippled na misconception. Angalia jinsi unavyoutafsiri utumwa inashangaza kweli kweli.

Kwamba mwanamke yoyote asiyesoma basi huyo ni wa kuwa mtumwa tu na utumwa wenyewe ni ile hali ya kuwa tegemezi.. Very wonderful idea.

Kumbe mwanaume anayeoa mke atakaye mtegemea kama maandiko yanavyoelekeza basi mwanaume huyo aoi mke bali anaoa mtumwa.

Kwa maana hiyo kwa mwanamke kusoma ni kuukimbia utumwa na kutosoma ni kuukubali utumwa.

This is the most bizarre concept i have ever come across in my entire life and here is where I rest my case.

Nyenyere na hawa ndio wake zetu wasomi tulioandaliwa na wakwe zetu.

Hakika hawa wakwe zetu wanakwama sana kwenye malezi yao.
 
Back
Top Bottom