Mwisho wa vita hauwi mzuri kwa mshindwaji! lakini unakuwa wa furaha kwa washindi hasa waliopigana usiku na mchana. Watu waliotayari kupika pilau na kunywa vileo kwa kushangilia ushindi hata kama bado mwanzo mbichi, lakini dalili ya mvua si mawingu?
Ukitaka kuua Jamii forum ni kazi ndogo, Pelekeni mafisadi jela, taifisha mali zao zote wagawie maskini!
Ukitaka kuua jamii forums na kuwakata kauli watu, wamiliki wote wa kagoda tuwajue na hatutaki usanii wowote ule, ama sivyo jamii forum haitakufa, watu wataongea hata kama kwa ishara, tutatuma ujumbe kuanzia kuzimu mpaka kwenye sayari ya pluto.
Nasema ukitaka kuua Jamii forums, wasizungumzie tena siasa fanya watakavyo wao, ongozeni kwa hekima na maarifa makubwa huku Haki ikitawala.
Pengine hivi karibuni jamii forum itakufa,pale ambapo TZ itakapokuwa kama peponi ya duniani, huku kila mmoja akitamani kuishi Tanzania.
Nasema ukitaka kuwanyamazisha hawa watu wasiongelee siasa ni rahisi sana muziki wa YONA NA MRAMBA uendelee, hata hivyo wataacha kuzungumzia siasa watazungumzia ushindi!!,Kipi bora kufurahia kwa ushindi kiduchu tunaouona au kuwa katika matumaini ya kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi kesho? haitawezekana kidogokidogo namna hii ina dalili zake ati!!, wenyewe watakosana watatajana tutakaa pembeni tukiwaona wanavyoumana,
Na hapo tutazidi kupashana kwa habari kwa furaha zaidi kuwa CCM wamemeguka hili halitakuwa la kupiga kelele watakuwa wametunyamazisha kuongea siasa na mafisadi! ila tutaongelea kuhusu ushindi huo pia!
Au wewe unafikiri nini kifanyike Kuinyamazisha JF??
nawasilisha
waberoya
Unamfahamu BRAZAMENI wewe?
His politiocs is greener than the environmentalists, his party card is the blue book, his religion is Latina chikas, the most apolitical brother you ever saw.
Mafisadi, kuna watu hawana habari bwana!
Kweli fasihi ngumu!!! JF is family take it man! hapo nashangilia jambo fulani
Hivi mmekuwa wageni Yerusalemu hii, hamjui lililotokea na litakalo tokea
lugha ya fasihi hiyo msiichukulie NEGATIVE THAT IS PURE POSITIVE
waberoya
jf haina haja ya kunyamazishwa , kwa namna inavyokwenda nadhani itafika sehemu itajinyamazisha yenyewe. ni vigumu sana kuamini kwamba ile jf niliyoijua kipindi cha nyuma imekuwa tofauti na hii ya leo. aaakh inakera kisha inaudhi kuona member wa jf leo hii wamemsahau adui yao na badili yake wanakuwa maadui wao kwa wao, kila siku ukija unaona mara huyu kaaga na mara huyu kamsema kwa ubaya huyu. mmmh its not too late acheni tubadilike kwa manufaa ya taifa letu. tuachaneni na mambo ya kitoto na mambo ya kitarabu tarabu.jf ni moja na lengo lake ni moja na member tuweni kitu kimoja. tanzania lazima igomboke!
mara nyingi huwa sieleweki, si unajua sikuenda shule tena , just niwieni radhi, lakini maelezo yako naona hayapingi nilichoeleza ila yanasupport nilichoeleza , siwezi kupinga tafauti ya mawazo baina ya members na najua kwamba jf ilikuwa imara na mpaka leo ipo imara lakini je itaendelea kuwa imara? kwa namna tunavyokwenda nayo?, waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na kwengine wanasema samaki mkunje angali mbichi, najua kijiumri changu kidogo na vijimawazo vyangu vya kitoto toto lakini mmmmh hisia zimekuwa kali kuliko mawazo katika kipindi cha siku mbili tatu zilizopita hapa jf .finger crossed nataka jf iwe kitu kimoja as a team hata kama tunatofautiana kimawazo .sorry kama nimekera.Ahhh...JF itajinyamazisha yenyewe!?Nilidhani wenye ndoto za aina hiyo ni mafisadi pekee kumbe hata baadhi ya wana-JF wenzetu!Hivi unaweza kutoa MIFANO HAI ya namna JF inavyotumia muda mwingi kujadili members badala ya mafisadi?Hii overgeneralization sio nzuri,hasa unapodai KILA SIKU huyu anaaga baada ya huyu kamsema huyu vibaya.This is an open forum,anayejiskia kujiunga anakaribishwa na anapojiskia kuondoa (hata bila kuaga ruksa).
JF kama forum inaweza kuwa moja lakini sio lazima members wake wawe wa aina moja kwa vile hii sio CCM ambayo kukemea ufisadi ni dhambi.Hapa kuna mkusanyiko wa watu wenye itikadi,taaluma,background,umri,imani,jinsia,etc tofauti.Katika mazingira kama hayo basi lazima tutatofautiana katika baadhi ya mambo.Na mfano hai ni huu wa wewe unayeamini kuwa JF itajinyamazisha yenyewe while mie (na well-wishers wa JF) tunaamini itadumu kwa muda mrefu.
Tanzania haiwezi kugomboka kwa mentality hizi za ku cherry-pick mabaya (eg uliyoyaita mambo ya kitoto au taarabu taarabu) na ku-ignore mijadala mizito inayopelekea haya yanayovuma leo hii huko nyumbani.Hivi umeshawahi kujiuliza mchango wa JF kwenye scandals za EPA na Richmond,kwa mfano?Hizi sio taarabu au utoto utoto.Na laiti ingekuwa hivyo basi vichwa kama FMES,Mwanakijiji,Pundit,GT,Jasusi,etc wasingeendelea kuwepo hapa na Invisible angeshaachana na shughuli hii ilopelekea akabughudhiwa na vyombo vya dola ( badala ya real criminals like the Kagodas).
By the way,ukiona mambo yako kinyume na matarajio yako unaweza kujichukulia likizo ya muda mrefu (au ya kudumu) kutembelea JF.I bet my last pence kwamba ukirudi utaikuta JF ikiwa as strong as ever.Nothing personal lkn hiyo overgeneralization haikustahili.
Kweli fasihi ngumu!!! JF is family take it man! hapo nashangilia jambo fulani
Hivi mmekuwa wageni Yerusalemu hii, hamjui lililotokea na litakalo tokea
lugha ya fasihi hiyo msiichukulie NEGATIVE THAT IS PURE POSITIVE
waberoya
JF sio forum ya kulani- mafisadi, mambo ya vita dhidi ya ufisadi ni kipengele kimoja tuu kati ya vingi ndani ya-JF, ni Jukwaa la Siasa. Vipenhele vingine vingi bado vipo. Hata vita vikiisha mambo mengine kibao muhimu yatapata nafasi nzuri mfano ni hoja ya kila Mtanzania ni tajiri, anatakiwa kumiliki gari, kuwa na nyumba nzuri na kuishi vizuri ikiwa ni pamoja na kula vizuri na kupata starehe. Tatizo hapa sio mafisadi, ni mfumo wa uchumi uliopelekea wachache wamiliki mali na wengi wahangaike.jF inatakiwa ikusaidie wewe usie na nyumba, gari na pesa za kutosha na ziada ya kununulia stock ili kubadili maisha yako, yangu na yake kwa kifupi maisha yetu. Sio suala la ufisadi ni zaidi ya hapo,. Hii ndio JF ijayo baada ya vita na 2010 kupita salama.