Jamhuri ya Shirikisho la Brazil | República Federativa do Brasil

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
4,125
6,250
| Jamhuri ya Shirikisho la Brazil, República Federativa do Brasil au Federative Republic of Brazil

Ni taifa linalopatikana bara la Amerika ya Kusini, lenye ukubwa wa eneo zipatazo millioni 8,511,965 Km[SUP]2 [/SUP]sawa na millioni 3,286,488 Square Mile's.

Brazil iliyopakana na Argentina, Bolivia, Colombia, Ufaransa (Ufaransa ya Guyana), Guyana, Paraguay, Suriname na Venezuela ni nyumbani kwa takribani watu millioni 212,559,420 kufikia Machi 25, 2020.

Brazil-Bandera.png

Bendera ya Jamhuri ya Shirikisho la Brazil

Lugha rasmi ya taifa hili ni Kireno, pesa rasmi ikiwa Riali (Real) Riali 1 ni sawa na Centavos 100. Mji mkuu wa taifa ni Brasilia, wenye kuhodhi shughuli za kiserikali.

Brasilia-21.jpg

Mji wa kiserikali Brasilia joao Phes

Kauli kuu ya taifa hili (Motto) ni "Ordem o Progresso" | "Utaratibu na Maendeleo"

itamaraty-2832206_1920.jpg

Ofisi ya Rais - Itamaraty © Central Brasil

Taifa hili lenye historia ya aina yake, rasilimali kama zote, uchumi wote, nyumbani kwa wote, teknolojia na vumbuzi zenye kustaajibisha sisi sote ni nyumbani kwa msitu wa Amazon, mto Amazon, bwawa la kufua umeme Itaipu Dam (lenye ushirika na mataifa matatu).

Brasilia JK.jpg

Daraja Brasilia JK 1 © Gonçalves Menior


| Uchumi, Biashara, Kilimo, Maendeleo na Utalii

Koloni hili la zamani kwa Ureno, limejengwa kwa ubora na ustadi. Likiwa kama taifa huru linayo miji iliyokuwa bora na yenye maendeleo ya kuvunja na mundu. Taifa hili linavyo viwanja vya ndege 2,500 huku viwanja 202 vikiwa na uwezo wa kupokea ndege ya aina yoyote ile.

Sao-Paulo.jpg

Jijini São Paulo ©Neison Moreno

Miji iliyokuwa kwa kiasi chake ni São Paulo, Rio de Jeneiro, Brasilia, Belo Horizonte, Fortaleza, Manaus, Salvador/Bahía, Recife, Nova Iguaca, Sao Luis, Joao Pessoa, Maceibo, Vitoria, Goiana, Cuiba, Belem, Porto Alegre, Campinas, Curitiba na Campos Grande.

Rio de Jeneiro Statue.jpg

Sanamu la Kristo - Rio de Jeneiro

Brazil ni nambari tisa kwa uchumi imara, huku ikiwa kinara kwa kilimo cha kahawa, sukari, maharage ya soya, kokoa, mihogo, katani, papai na machungwa.

Biashara ya dhahabu na uchimbaji wa mafuta ni tegemeo na sekta muhimu katika ukuaji wa kiuchumi.

Bridge Brasilia JKLights.jpg

Daraja la Brasilia JK ©Vienno Çasu

Viwanda ndani ya Brazil vinaifanya kuwa nchi ya 6 kwa mapinduzi ya viwanda. Uwapo Brazil utashuhudia viwanda vya magari, tarakilishi, ndege, roketi, mavazi, vyakula, vinywaji, madawa, saruji na nyama.

Viwanda vya magari chapa Volkswagen, Ford, General Motors, Iveco, Renault, Peugeot, Citroën, Toyota, Honda, Mercedes-Benz, BMW na Hyundai vinapatikana Brasil kwa ukanda wa Amerika ya Latin.

VEIS Beach Raphael-Nogueira.jpg

Fukwe ya VEIS © Raphael Nogueira

Milima, mabonde, mito, sehemu za kale na fukwe za kisasa zinalifanya taifa kuwa sehemu ya utalii. Fukwe 10 bora kati ya 50 za dunia zinapatikana Brazil, huku fukwe inayosemekana kuwa namba moja Boa Viagam inapatikana jijini Fortaleza.

| Sayansi na Teknolojia

Dunia imeshuhudia sayansi na teknolojia ya kustaajibisha kutoka ndani ya Brazil baada ya uvumbuzi wa uchimbaji mafuta na gesi katika maji ulioasisiwa vilivyo na kampuni ya uchimbaji, uchakataji na uuzaji wa mafuta na gesi Petrobas.

Divulgaçao Petrobas Oil Platform_P-51_(Brazil).jpg

Uchimbaji wa mafuta Katika maji © Petrobas/Hereilo Bau/Wiki

Ujenzi wa kituo cha anga cha kimataifa (ISS) umechagizwa na mchango wa asilimia 30 katika ujenzi na Brazil.

César Caltes, Mario Schönberg, José Leite Lopes na Fritz Müller ni wanasayansi waliozichakata protokali na kuzinyambulisha ipasavyo.

Brazil ni taifa la kwanza katika utumiaji wa mitandao kwa shughuli za kiserikali na mahakama, kuanzia miaka ya 2009 imekuwa ikitumia mitandao ya YouTube na Twitter kutekeleza masuala ya kiserikali.

| Elimu na Afya

Tunapozungumzia mataifa yenye wasomi basi huwezi kuacha kuitaja Brazil. Taifa lenye wasomi katika nyanja mbalimbali zikiwemo kilimo, teknolojia ya habari na mawasiliano, uchimbaji na uchakataji mafuta na gesi, sayansi ya anga za mbali, kemikali kwa uchache, inayopelekea wasomi wengi kutumwa katika mataifa yanayoendelea.

Ministro Participa da inauguração do Acelerador de Partículas Sirius.jpg

Wizara ya Elimu, Sayansi, Vumbuzi na Teknolojia - Brasilia © Sirius x Wiki

Vyuo ndani ya Brazil ni vyenye hadhi yake kama Chuo cha São Paulo, Oswaldo Cruz Institute, Butantan Institute, Aerospace Technical Center na Brazilian Agricultural Research Corporation.

Wasomi wenye miaka 18 - 70 ni lazima kupiga kura, wenye kiwango kidogo cha elimu kuanzia miaka 16 na zaidi ya 70 si lazima kupiga kura.

Huduma za afya ni bure kwa kila raia | Huduma hii inachagizwa na asilimia 9 ya mapato yote kuelekezwa katika afya.

| Michezo, Burudani, Sanaa na Filamu

Mpira wa miguu ni mchezo wa taifa hili, bingwa wa kihistoria wa kombe la dunia mara 5. Makao makuu ya vilabu mwiba kimataifa Corinthians, Botafogo, Santos, Atlético Mineiro na Grêmio.

Maracana.jpg

Uwanja wa taifa - Maracana

Brazil ni chimbuko la mpira wa ufukweni (Beach Soccer) na mpira wa ndani (Fútsal), nyumbani kwa Cicinho, Robinho, Paulinho, Juninho, Fabinho, Ronaldinho, Jairzinho, Coutinho, Fernandinho, Sylvinho, Kaká, Dani Alves, Neymar, Roberto Carlos, Firmino na mwamba wa kuanguka Richalson.

IMG_20200520_020357.jpg

Dani Alves ©Fred Ciiedo Macli

Waandishi Joaquim Manuel der Macedo na José de Alencar. Wachoraji Victor Meirelles, Ismael Nery, Vicente do Rego Monteiro.

Graffiti Brasil.jpg

Graffiti Ezasue © Ismael Nery

Anitta+MTV+MIAW.jpg

Anitta ©MTV Miaw

Brazil inawakilishwa vyema na mwimbaji pia muigizaji Larissa de Macedo Machado maarufu kama Anitta aliyetamba na nyimbo kama Medicina na Downtown.

nego-do-borel.jpg

Nego do Borel © Visit Lisbon

Kijana Leno Maycon Viana Gomes maarufu Nego do Borel anayetambulishwa kwa vibao Bonde dos Brados, Diamante e Lama, Minha Cama na Corazón. Wanamuziki wengine ni Deejay Télio mwenye uwezo wa kuchanganya nyimbo kwa kutumia (Disc Jockey) sahani 8 Kevinho, Pocah, IZA, Pablo Vittar, Clau, Luisa Sonza, Lexa, Damni Russo na Michel Teló wameionyesha dunia vipawa kutoka Brazil.

Upande wa filamu. Brazil inawakilishwa vyema na muongozaji Fernando Meirelles mtayarishaji wa filamu ya "City of God" na waongozaji wengine ni Pablo Cesar Saraceni, Nelson Pereira dos Santos na Gonçalo Carvoeiras anayetegemewa kwenda kituo cha anga cha kimataifa kuongoza filamu.

Hii ndio Jamhuri ya Shirikisho la Brazil 🇧🇷
 
Dah!.. nchi kubwa sana hii ni sawa na nchi yetu ya Tanzania ziwe tisa (9) kisha uziunganishe pamoja.

Wataalamu wa Samba hawa (mabingwa wa kihistoria wa kombe la Fifa la dunia) na soka ⚽⚽⚽ huko ndiyo nyumbani kwake bila kusahau warembo wa huko usipime wamesimama mbaya...😂😂😂

Huu msitu wao (Amazon) unachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa hewa Safi duniani kwa kunyonya kiasi kikubwa Cha Carbondioxide inayozalishwa toka viwanda vikubwa duniani.

Vipi mkuu ile hadithi ya kuwepo kwa Anaconda na wahindi wekundu huko msitu wa Amazon ina ukweli wowote?

God bless Brazil 🇧🇷🇧🇷🇧🇷
 
Dah!.. nchi kubwa sana hii ni sawa na nchi yetu ya Tanzania ziwe tisa (9) kisha uziunganishe pamoja.

Wataalamu wa Samba hawa (mabingwa wa kihistoria wa kombe la Fifa la dunia) na soka ⚽⚽⚽ huko ndiyo nyumbani kwake bila kusahau warembo wa huko usipime wamesimama mbaya...😂😂😂

Huu msitu wao (Amazon) unachangia kwa kiasi kikubwa uwepo wa hewa Safi duniani kwa kunyonya kiasi kikubwa Cha Carbondioxide inayozalishwa toka viwanda vikubwa duniani.

Vipi mkuu ile hadithi ya kuwepo kwa Anaconda na wahindi wekundu huko msitu wa Amazon ina ukweli wowote?

God bless Brazil 🇧🇷🇧🇷🇧🇷
Proved umemaliza points zangu ambazo nilipanga kuzitumia 😄

Anaconda na red Indies wote wanapatikana Brasil ni ukweli kabisa kwa mujibu wa Brazilian-Tanzanian aliyepo Brasil.
 
Terra adorada, Entre outras mil,
És tu, Brasil, Ó Pátria amada!

Mkuu hili ndio ungeliweka lá mwisho ktk nchi za amerika latina,hii nchi ndio baba yao😂😂😂
Yaani mreno asingekuwa bahiri basi angekuwa na eneo kubwa sana kwa kuwa mspanhol alitaka kumuuzia Bolívia,peru n.k
Kuna documentar ya equatorial Guiné inadai ya kuwa mreno na mhispanyol walibadilishana makoloni,kwa kuwa mreno hakuwa na koloni América basi akapewa Brasil na kwa kuwa mspanhol Hana koloni Afrika basi akapewa equatorial Guiné!

Nalog off
 
Back
Top Bottom