James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

James Rugemalila afungua kesi Mahakama Kuu

Status
Not open for further replies.
chikandi Kuleta taarifa kwa ID feki hapa JF ni kawaida hata EPA zililipuliwa hapa hivi hivi....ila kukanusha lazima ujenge mazingira ya kuaminika kimaelezo ikibidi hata identity ....
 
Last edited by a moderator:
I smell something fishy!

I guess mama Tibaijuka could be behind this move by Mr.Rugemarila.

However,this move is of great advantage to us.

Unadhani mama Tiba angenyamaza? Hapa ndipo ukweli utazidi kujulikana na hasa ukizingatia kabila yetu hatukubali kushindwa kirahisi.
 
chikandi Kuleta taarifa kwa ID feki hapa JF ni kawaida hata EPA zililipuliwa hapa hivi hivi....ila kukanusha lazima ujenge mazingira ya kuaminika kimaelezo ikibidi hata identity ....

Aliyeleta uzushi huu kaeleza kuwa ni tetesi. Mbaya zaidi, hajasema amezisikia wapi tetesi hizo. Sisi tunaojua ukweli tunasema huu "ni uongo". kama kuna ukweli arejee hapa. Mbona ameingia mitini? Acheni hizo bana. Rugemalira afungue kesi kwa misingi gani?
 
Zitto alilisema hilo wao akina Professor wakadai serikali ina kinga kutoka kwa mwekezaji mpya.Safi Ruge zunguka tena mbuyu ili uchote fedha nyingine za bure,zile ulizompa dada yake in good faith zilikuwa za udanganyifu,Tanzania haishi vituko,sasa mkulu alisema zile pesa sio za serikali na Ruge anaishitaki serikali.

Unafahamu anachoenda kushtaki? Ama unaongea tu?
 
Sijui kama nitaweza kujibu maswali yako yote ila kwa kifupi ni kuwa VIP engineering chini ya Ruge ilifunga mashauri ya ufilisi mahakamani kati yake na Mechamar juu ya ufilisi wa IPTL. Kabla shauri halijaisha akaibuka PAP ( wanajua wenyewe walichokubaliana) , Ruge akapeleka hapati ya kutoa hilo shauri ya ufilisi na akamuuzia PAP hisia zake 30%.
Hapo jaji utamwa akatoa hukumu kuwa all affairs of iptl should be handled to PAP.
Sasa kwasababu wezi walishadhamiria kutuibia wakapotosha hiyo hukumu wakasafisha akaunti ya escrow.... Hizo fedha zikagaiwa kwa wezi wote ikiwemo wale wa Ikulu yetu na wengineo na kumlipa Ruge dili lake la hisa 30% tena muhongo akiwa ndiyo dalali.
Sasa leo hii watanzania tunakomaa warudishe fedha zetu anaibuka mshirika wa wizi huu anamshitaki mwizi mwenzake. Huoni hapo kuna kamchezo wa kisanii.?

kwa hiyo PAP sio kampuni hewa, mahakama imeitambua! au sio?

 
Taariafa hii ya uzushi imeshakanushwa. Wewe mtoa mada umeitoa wapi?

Hata kama imekanushwa ila akiamua kudai ukianza na ile 56bn ya kuvunja mkataba na 36 bn ya gharama ya kesi aliyoshinda hizi akizitaka hata kesho mzee anazichukua kweupe
 
Mkuu kuuza hisa zake haimaanishi kwamba ile faida iliokuwepo wakati wa mgogoro imeondoka. Kumbuka fedha ziliaza kuhifadhiwa kitambo kwa hiyo katika zile zilizokuwa zinahifadhiwa, na zake zimo kama mmiliki wa kampuni wakati ule.

ukiuza hisa huuzi na madeni?
 
Njia ya mwongo huwa fupi huo ni mwendelezo wa walioshindwa hoja za msingi huko awali....wanatapatapa
Hapa hoja tuongelee Tapeli STD Charttered Hongkong wanaotaka kuliibia Taifa .
 
Hili suala LA ESCROW litaingiza Taifa shimoni........ MHONGO,RUGEMARILA,MASWI, TIBAIJUKA,WEREMA, CHENGE NA YULE SINGA SINGA.....Wameufunga mwaka 2014 kwa kishindo,siamini kama Hawa raia wanaitikisa Nchi halafu watu wanakenua tu meno.
 
JK naye ni wa kusikilizwa?
Ruge alipofanya dili na PAP halafu akakubaliana na hukumu ya jaji utamwa kuwa all iptl affairs should be handled to PAP ni kuwa Ruge alishapoteza kila kitu kuhusu iptl.
Kwa kifupi baada ya hapo iptl haitamuhusu tena.

Anachokomalia ni kwamba, Serikali ya JK na CCM ilifanya uzembe kwa kuruhusu/kuacha kampuni feki ya kigeni PAP kuingia nchini na kufanya ubia na mwekezaji mzawa ambaye ni yeye Rugemalira!
 
Hivi kwa nini Watanzania tunapenda kukimbia facts na kujadili porojo. Mmepewa facts zote kuhusu suala hili la Escrow lakini bado mnazungumzia habari za kufikirika! Nashangaa kwa nini moderators wanaacha thread ya kizushi kama hii ya Rugemalira kufungua kesi, iendelee kujadiliwa humu.
 
Yuko sawa kabisa....! Huyu mkwere bora tu anaondoka, sitashangaa kusikia ameshinda na serikali ya Kikwete imeamrishwa kulipa hayo mahela tena, mswahili!!!!! Haaaaa
 
Hii ni chai tu!
Huyu Ruge alikuwa na kesi ya ufilisi na Mechamar mahakamani , akaibuka PAP . Ruge akaongea na PAP wakakubaliana akapeleka hati ya kuondoa hiyo kesi. Jaji utamwa akatoa hukumu , Ruge akamuuzia hisia zake PAP.
Sasa hivi Ruge anatoa wapi ujasiri wa kufungua kesi?
Baada ya Ruge kuuzia hisia zake kwa PAP , maana yake hana chake tena IPTL na kwa hizo hizo hisia zake alizomuuzia PAP anakua mmiliki halali wa iptl.
Hamna kitu hapo , wametuibia hela zetu halafu wanatuletea michezo ya maigizo.
Tunataka pesa zetu mlizoiba escrow.
Hapa Ruge anataka kuthibitisha kwamba aliuza hiza zake kwa PAP isivyo halali kwa kuwa Serikali ilipaswa kumtahadharisha kuwa PAP haina usajili halali. He wants the government to be accountable for this lapse in the legal proceedings in companies' registration.
 
Yuko sawa kabisa....! Huyu mkwere bora tu anaondoka, sitashangaa kusikia ameshinda na serikali ya Kikwete imeamrishwa kulipa hayo mahela tena, mswahili!!!!! Haaaaa

Hapo bado PAP nayo haijafungua Kesi dhidi ya Serikali hii hii kwa kile kitakachokuwa kupewa baraka zote za ulipwaji na Serikali ya Kikwete na Kikwete mwenyewe kukiri fedha si ya umma ni ya PAP na kwamba ililipwa kihalali KISHA kugeukwa. Kikwete Kikwete my President wake up Umelala usingizi sana! Escrow inaidondosha Serikali yako ya CCM kama Serikali ya KANU Kenya!
 
Nahisi kama umetunga vile!

Hata kama jamaa katunga bado Rugemalira anaweza akafungua kesi hapo na akashinda! mwanya na ufa mkubwa huu mkuu. Rais Kikwete hakuwa na sababu ya kuchanganya mambo kwenye hotuba yake! Angempumzisha Muhongo, Maswi na Tibaijuka straight forward bila kupinda pinda
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom