James Orengo vs Tundu Lissu

James Orengo vs Tundu Lissu

Unaleta uzi kwenye jukwaa la siasa alafu unasema wanasiasa mkae pembeni si ungepeleka kule kwenye jukwaa la katiba na sheria. Wewe ni chizi usiejitambua
wanasiasa wakae pembeni kwani hawana haki ya kuchangia/kutoa maoni?hahaha
 
Jaman nimeamin kwann watanzania itatuchukua miaka 100 kupiga hatua.

Imagine hapa watu wako bize kudiscuss tindu Lissu vs orengo

Hivi don't you have anything else to discuss?

Yaan anayesema Lissu sijui siyo vzr hebu tajeni basi ninyi mkijilinganisha naye mkoje? Ww umefanya nn?

Orengo mzur/wa kawaida/ anapofanyia kaz ndipo panapo mbaba dah!!...….hebu tuambie basi ww ukoje ukiwekwa kwenye hayo mazingira?

Ni akili za kujinga tuu zitakazo poteza muda kujadili watu.

Baadhi yenu ndio mliokuwa mnalalamika eti usaili wa tra mtihan ulikuwa mgumu. Kusoma na kujadili mambo ya msingi kwenu ni upumbavu ila kujadili watu ndio ya maana. Sijui nani kawaloga ninyi vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ni mihemko tu, wachache sana kama wapo wanabackground ya Orengo kama wanavyomhfahamu Lissu. Soma hii "His responses were calculated, respectful and sometimes remorseful. He was the exact opposite of the James Orengo in the campaign trail – where statements were made without caution"( Five ways James Orengo has proved to be brilliant lawyer). Toka amalize chuo kikuu cha Nairobi sheria amefanya shughuli mbili kubwa SIASA na SHERIA. Amekuwa kiongozi wa wanafunzi enzi hizo za Kenyatta-akipambana na serikali hiyo na chuo kufungwa mara nyingi tu. Labda kama kuna tofauti kati yake na TL ni experience ya Orengo ya sheria na siasa za upinzani ni ndefu zaidi (alimaliza chuo 1974) anaelekea 66+. Hii nafikiri ni petition yake ya 2 ya uchaguzi wa uraisi. Zaidi ya hapo sioni tofauti yao na TL bado ana muda wa kufanya mengi zaidi.
 
Nimeanza kumfuatilia James Orengo siku nyingi sana Mkuu na nadhani kumfananisha na Tundu Lissu utakuwa unamkosea mno Heshima ( James Orengo ) ila ninachoweza kusema ni kwamba Tundu Lissu ndiyo anamuiga na bado ana mengi sana ya kujifunza kutoka kwa ' Mwanamume ' James Orengo.

Zifuatazo ni Sifa zake James Orengo ambazo kwa ukizitafuta kwa Tundu Lissu unaweza usizipate leo wala kesho au hata zisiwepo kabisa:

  1. James Orengo ana akili za kuzaliwa siyo za kuzikuta shuleni au ukubwani.
  2. James Orengo alienda Shuleni kupata maarifa mengi na siyo Kuelimika tu.
  3. James Orengo si Mtu wa Kukurupuka bali ni Mtu makini na mwenye kupima jambo Kwanza.
  4. James Orengo ana nidhamu hasa ya Kisheria na huwa si Mkaidi mbele ya Sheria za nchi na Mamlaka.
  5. James Orengo tokea akiwa anasoma Chekechea hadi University alikuwa wa Kwanza / anaongoza tofauti wa wengine ambao wamekuja kuwa wa Kwanza kwa Kubahatisha tu wakiwa Mlimani / School of Law.
  6. James Orengo hana rekodi yoyote ile ya uwendawazimu kama ambavyo Wanasheria wengine sehemu mbalimbali duniani inasemekana waliwahi kuwa na uwendawazimu uliotukuka.
  7. James Orengo huwa hafanyi Uanaharakati bali anafanya Siasa safi na zenye mashiko.
Kumfananisha James Orengo na Tundu Lissu ni sawa na leo hii utake kumfananisha Kocha Jose Mourinho ( James Orengo ) wa Chelsea ya Uingereza na Kocha Jamhuri Kihwelo ( Tundu Lissu ) wa Dodoma Kombaini ya Dodoma Tanzania. Wapi na wapi?

Bado sijaona kama James Orengo hapa East Africa.

Ni wazi huwajui wote, Lissu au James Orengo.

Eti East Africa hujaona kama James Orengo we we unawajua lawyers wote?

Hujui hata aina ya siasa anazofanya Orengo. Wapo senior councils wengine moto hapo hapo Kenya kuliko Orengo.

Watu wengi wanahisi Orengo ni Counsel ambaye amewakilisha tu NASA wasichojua ni kwamba hapo anatetea chama chake kama Senator kama ambavyo Lissu hufanya kwa kesi za Chadema.
 
Huyu bwana kajizolea sifa lukuki kwa wakenya na wapenda sheria wote duniani. Imefikia mpaka Watanzania wanamfananisha na Mwanasheria machachari Tundu Lissu..

Sijawahi kumshuhudia Lissu akiwa mahakamani, ila nimemwona Orengo, jamaa is very calm and calculated. Anaongea kwa tone ambayo kila mmoja atashawishika kumsikiliza, sijui Lissu akiwa mahakamani anakuaje, lakini kama anaongea kwa ile tone ya bungeni na kwenye mikutano ya kisiasa naona wazi Lissu atakuwa na weakness fulani.

Ningependa mpitie hili andiko ambalo limempa Orengo sifa lukuki na ni kwanini ameshinda hii kesi akiwagalagaza SC wengine wanne..

Five ways James Orengo has proved to be brilliant lawyer

JE NI HAKI KUMFANANISHA ORENGO NA LISSU? Naomba vijana wa siasa mkae pembeni ningependa kujibiwa na wanasheria na watu wenye uzoefu na mahakama..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka naona unafananisha kichuguu(Lissu) na Orengo(Mlima tena Mlima Kilimanjaro),Lissu anaweza kesi za akina Sepetu ,Orengo kakubuhu kwenye kesi za kikatiba hajaanza leo wala jana ,alianza tangu enzi za Moi na kufungwa mara nyingi(sio kuwekwa jela kwa akina Lissu)siku moja .Orengo ni kati ya mawakili waandamizi Kenya ilihali Lissu ni wakili mihemuko
 
Kuna mwanasheria mmoja wa Kenya, nafikiri jaji yule,nilimsikia BBC, anasema"the national erection", nikataka kucheka sana.

Wakenya wanavyotucheka Watanzania hatujui Kiingereza halafu Jaji wao mkubwa sana anasema "national erection".
 
Tundu Antipas Lissu is "Eloquent"...he has legal language anapokuwa mahakamani,na anapokuwa bungeni,he has a "political Language".

Ubaya wa Lissu ni kuwa,maisha yake yote amechagua kuwa upande wa "kupinga" na si "kukubali"...Toka shule ya Msingi,Shule ya upili,chuo,JKT mpaka katika maisha yake ya kila siku,amechagua kuwa "upande wa wachache wasio na sauti"

Upande wa wachache huwa hauna sifa,ni upande wa kufitiniwa na kuhujumiwa...Zaidi ya lugha ya kimahakama,nje ya siasa na sheria,Tundu Lissu ni mtu muungwana sana,ana lugha nzuri na si mtu wa kisasi wala hasira za haraka!!

Kuna wakati ukikaa na Lissu kuongelea maisha na familia,unaweza kujiuliza,hivi huyu ndio Lissu wa Bungeni?
Sasa kwa nini alivalishwa kilemba na Bi Kijo?
 
Ingekuwa vyema wale walio shuhudia TL akiwa mahakamani watujuze, sio wengine wanaleta chuki za kisiasa kwenye hoja muhimu kama hii.
 
Inabidi tuwaweke pamoja kisha tuwapambanishe
 
Sijawahi kumshuhudia Lissu akiwa mahakamani, ila nimemwona Orengo, jamaa is very calm and calculated. Anaongea kwa tone ambayo kila mmoja atashawishika kumsikiliza, sijui Lissu akiwa mahakamani anakuaje, lakini kama anaongea kwa ile tone ya bungeni na kwenye mikutano ya kisiasa naona wazi Lissu atakuwa na weakness fulani.
Acha dharau mkuu,huwezi kumfananisha Orengo na mpayukaji tundu lissu.
Tundu anashindwa kutengeneza tu hati za viapo kuwanasua wabunge 8 wa cuf mpaka wamefukuzwa kila siku wanarudishwa wakasahihishe hati za kiapo.
James Orengo ametengeneza hati ya kiapo ya kurasa 2400 na hakuna hata siku moja tumesikia ameambiwa akarekebishe
Tundu Lissu ni wakili wa kesi za bange na uchochoezi tu,ndio maana aligalagazwa na Dr Tulia Ackson kwenye kesi ya mita 200.
Lissu anakua overated,hakuna mtu makini anaweza kumpa kesi yake huyozaidi hao matanapa wenzake
 
Binafsi namuona T. Lissu kijana shujaa,mwanasiasa machachari sana, msomi anae ijua vzr sheria, mwenye msimamo wa kusimamia anachokiamini.

Tatizo lina kuja pale anapo kutana na Speaker&/Naibu speaker aliye hongwa Ubunge!! Hata ufanye nn hawezi kutenda haki!! Ana timiza matakwa ya mteuzi wake.

Speaker ana mpa Mbunge adhabu ambazo hazipo hata ktk kanuni za Bunge! Je huu ni mhimili au kivuli? Speaker anatangaza ubabe majuzi tukutane Sept 5. Huu ni upuuzi wa hali ya juu.

Mahakamani T. Lissu anakutana na Majaji/Mahakimu walio ahidiwa ukimfunga flani...tutakupandisha cheo. Kesi za kusingiziwa ndio usiseme!!

Generally, mazingira anayo pitia (kesi kila kukicha), ishi, kuwindwa, operate T. Lissu ni magumu kuliko Orengo.

Nimpongeze tu T. Lissu, wala asikatishwe tamaa. Tiyar kaisha jenga ari kubwa sn kwa vijana kuhoji vitu.

JPM KAMATA WEZI
 
Nadhani tofauti iko wazi. Ukisoma maelezo hayo, Orengo aliweza kutofautisha jukwaa la siasa na chumba cha mahakama. Jambo ambalo mwenzetu huyu anayeitwa machachari, hana kabisa! NImeona anavyoshindwa kutofautisha Bunge na mikutano ya mitaani. Nadhani Orengo ni mtu mwenye sifa za pekee. Ni mtu anayeweza kujua uso wa mwenzake unasema nini. Tatizo la Lissu anataka kila mtu amsikilize yeye anasema nini bila kujali msikilizaji ni nani.

naomba audio au vidio lissu akiwa mahakamani. otherwise acha unafki.
 
..lakini waandishi wanasema James Orengo wa kwenye majukwaa ya siasa ni tofauti na yule aliyeonekana mahakamani.

..mazingira ya mjadala, kuanzia na hoja iliyoko mezani, weledi wa wanaoshiriki mjadala husika, pamoja na busara na maadili ya muongoza mjadala, yana athari kubwa ktk jinsi ambavyo washiriki wa mjadala huo wata-behave.

..JAMES ORENGO ukimpeleka kwenye bunge la Tz linaloongozwa na SPIKA asiyetenda haki kama NDUGAI anaweza ku-behave tofauti kabisa na yule uliyemuona mahakamu kuu ya Kenya.

..Hata TL ukimuweka ktk mazingira ambayo HAKI inatendeka nina hakika atajenga hoja zake kwa utulivu.
Jamaa amesema hataki kujibiwa kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kumdharilisha Orengo kumfananisha na Lisu.Lisu hana utulivu na hana uwezo mzuri wa kuzungumza na kujenga hoja km mwanasheria. Ana jaziba na akikutana na wanasheria wazuri atapigana hata ngumi. Anapata sifa kutokana na system corrupt ya uendeshaji mashitaka hapa nchini

Hata hapa Tanzania, bado Lisu hauwezi kumweka level ya akina Nyaucho au Lamwai au Dk Nshala au Ringo Tenga na wengine wengi kwa ustadi wa kuzungumza na kujenga hoja km mwanasheria.Ni mtu wa kupayuka na hayupo organized.

Lisu ni mwanasheria kwa sababu alifaulu mitihani lakini hana traits anazopaswa kuwa nazo mwanasheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu bwana kajizolea sifa lukuki kwa wakenya na wapenda sheria wote duniani. Imefikia mpaka Watanzania wanamfananisha na Mwanasheria machachari Tundu Lissu..

Sijawahi kumshuhudia Lissu akiwa mahakamani, ila nimemwona Orengo, jamaa is very calm and calculated. Anaongea kwa tone ambayo kila mmoja atashawishika kumsikiliza, sijui Lissu akiwa mahakamani anakuaje, lakini kama anaongea kwa ile tone ya bungeni na kwenye mikutano ya kisiasa naona wazi Lissu atakuwa na weakness fulani.

Ningependa mpitie hili andiko ambalo limempa Orengo sifa lukuki na ni kwanini ameshinda hii kesi akiwagalagaza SC wengine wanne..

Five ways James Orengo has proved to be brilliant lawyer

JE NI HAKI KUMFANANISHA ORENGO NA LISSU? Naomba vijana wa siasa mkae pembeni ningependa kujibiwa na wanasheria na watu wenye uzoefu na mahakama..

Sent using Jamii Forums mobile app


Mh.Lissu huwa anaongea point Ila binafsi uwathirishaji wake wa hoja namchukulia kama mropokaji.
 
Back
Top Bottom