James Ole Millya anakuwa Wakili leo

James Ole Millya anakuwa Wakili leo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kada wa CHADEMA na Mbunge Mtarajiwa wa Simanjiro,James Ole Millya leo anaapishwa rasmi na Jaji Mkuu wa Tanzania,Mohamed Chande Othman kuwa Wakili wa kujitegemea.

Kuapishwa huko kunafanyika kuanzia saa tatu asubuhi hii katika Ukumbi wa Ubungo Plaza.

Karibu Ole Millya na Mawakili wapya wengine katika Jumuiya ya Mawakili ili tutende haki na kuikomboa Tanzania yetu.

Hongera 'Wakili Msomi' James Ole Millya na yeyote awaye!
 
Nimemuona ameanza kwenda na kasi ya M4C.

Nilimuona na kumsikiliza mkutano wa mara ya mwisho pale Arusha....karibu kamanda.
 
Inapendeza sana kwa kiongozi wa chama makini kama CHADEMA kuwa na WELEDI kwenye fani aliyoisomea. Namtabiria Ole Millya kufuata nyayo za great lawyers kama Prof Safari, Marando na Lissu...

Kodos CHADEMA huyu kijana ni jembe mtumieni vizuri, sio kuwa na lundo la vijana waganga njaa pale makao makuu wanaoshindwa kutafuta hela kwenye fani walizosomea wanategemea kupiga majungu ndio wapate mlo wa siku. Pia msiige ule mfumo maarufu wa CCM wa JIKOMBE UKOMBOLEWE unawafanya vijana kama Nape kutofuata kile wanachokiamini kwa minajili ya kujikomba wabakie madarakani...

Congrats Ole Millya, its great day for you, great day for CDM
 
sio ubungo itakuwa viwanja vya school of law!
Asante Kamanda kwa taarifa hiyo. Nyaraka zangu za awali zilionesha ni Ubungo Plaza.Kumbe ni Law School of Tanzania? Safi sana.Ni pale nyuma ya Mawasiliano Towers kama unapita Sam Nujoma Road waungwana
 
Safi sana kamanda,hawa ndiyo watakotusaidia baadaye katika wizara ya sheria na katiba!!
 
Hongera Bro ukisha kuwa wakili njoo nyumbani makamanda wa Mererani wamekuandalia mkutano wa hadhara.,
 
Kuna jamaa anajita olemando wa simanjiro yumo humu jf akizipata hizi habari lazima apandishe mori anajitaidi kwa kila njia kumwombea mabaya millya.
 
Hongera Kamanda, umma hasa wa Simanjiro una matarajio makubwa kwako
 
Kuna jamaa anajita olemando wa simanjiro yumo humu jf akizipata hizi habari lazima apandishe mori anajitaidi kwa kila njia kumwombea mabaya millya.

huyu olemando yuko atown anashangaa magorofa!
 
DPP ( fereshi), general ulimwengu, nao wapewa mihuri........
 
Back
Top Bottom