Jambo TBC: Time is NOT Money!

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
6,032
3,944
Kila mara ninapoangalia kipindi cha Jambo kinachorushwa hewani na Televisheni ya Taifa TBC napata wasiwasi kwamba ama viongozi wa kitaifa wa Tanzania hawafahamu kuwa Time is Money, hata dakika moja tu, ama hawajali.

Utaratibu wa kipindi hiki ni kumuita mheshimiwa kiongozi yoyote na kuanza kuhojiana naye lakini katikati ya mahojiano hayo kipindi kinapelekwa kwa mtangazaji mwingine ambaye husoma taarifa za michezo ama za magazeti kwanza ndipo hurejeshwa kwa mtangazaji anayehojiana na mgeni wa kipindi ambaye atakuwa amekaa tu akisubiri!

Nimekuwa nikijiuliza kwa nini hawaendelei kumhoji tu mgeni aliye studio wakamalizana naye kabisa akajiondokea kuendelea na shughuli zake nyingine ndipo waendelee na habari za nagazeti na michezo.

Ninajiuliza sana kuhusu aina ya viongozi, wakiwemo hata mawaziri, wanaokubali kuwekwa kando kwanza kwa dakika kumi ili kupisha habari za magazeti na za Michezo!
Dakika kumi ni nyingi sana kwa kiongozi kukaa tu Studio akisubiri kuhojiwa!

TBC, mhojini kiongozi,malizaneni naye kabisa ajiondokee akaendelee na shughuli zake za kujenga nchi na nyinyi muendelee na habari za michezo na magazeti! Kwani kuna tabu gani kufanya hivyo? Time is Money, jamani! Unless Viongozi wa Kitanzania wanaoitwa studio za TBC hawalioni hili!
 
Nilidhani ni mimi peke yangu mwenye shida na ule utaratibu!...Lakini inaonyesha wanakuwa comfortable tu, hivi nyie hamjui raha ya 'kuuza sura na kuosha VINYWA?...
 
Hii inasikitisha sana nami pia huwa sipendelei,utakuta mtangazaji kamuuliza swali mgeni,ile mgeni kaanza kujibu ohhh tusome massage,oohhh kuna simu,oohh tusilikilize habari za magazeti:Baadae wakirudi kwa mgeni kesha sahau hata point aliyopanga kujibu aibi kubwa sana TBC badilikeni.
 
Hata kwenye world cup utakuta Chacha kamuuliza swali Edo ile inaanza kuelezea mafundi wanachomeka tangazo hivyo Chacha kwa haraka bila hata kumuomba Edo hutamka moja kwa moja kuwa tusikilize tangozo.Haaaaaaaa,inasikitisha
 
Utaratibu wao unaharibu kabisa flow ya taarifa inayotolewa, na mvuto wa kipindi unapotea kabisa.
 
Mie pia huwa sielewi kwanini wanakatisha kipindi na kuendelea na matangazo mengine kisha wanaendelea na maongezi na mgeni wao wa siku hiyo..Sababu za msingi ni zipi kwanini wasimalize kimoja baada ya kingine?
 
Back
Top Bottom