Jambo/kitu gani hutakiwi kumhusisha Mungu?

Jambo/kitu gani hutakiwi kumhusisha Mungu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,941
Reaction score
51,061
Ukitaka timu yako ishinde unaweza kumhusisha Mungu. Jee ikishinda ni sawa kumshukuru Mungu na ikishindwa ni Mungu wa kulaumiwa?

Ukifanya biashara ni sawa kuhusisha Mungu, kama mizani yako haipo sawa ukipata faida unaweza kumshukuru Mungu.

Unapotongoza upate mke unaweza kumhusisha Mungu hata kama maneno utakayotumia kutongozea yatakuwa ya uongo?

Ni mambo gani mtu hatakiwi kumhusisha nayo Mungu?
 
Uovu na dhambi ni nini? Kucheza mpira wa miguu ni dhambi au ni uovu?
Waislamu wanasema uchi wa mwanaume unaanzia kwenye kitovu mpaka magoti lakini wamejazana kwenye mpira na wanaovaa hadi matangazo ya betting na pombe😁
 
Ahahah. Na kweli maana mpira wa miguu mi full kudanganyana. Unajifanya unaenda huku kumbe unapita kule mwenzako anaanguka chini. Unamdangajya kipa kupiga kulia kumbe unapeleka kushoto 😂.
Full uongo uongo yani
Mara unapiga mtu tobo, mara unamvisha kanzu. Na ni sawa tu hata ukifunga goli kwa kende 😂
 
Ukiwa unakufa usimshirikishe mana yeye ndo anaekuita. Ukimwita akutete maana yake hutaki kwenda
 
Inategemea na imani, ujue kila mtu ana mahusiano binafsi na Mungu...

Kwahiyo kila mtu ana tafsiri yake ya imani kufanya chochote.

Mfano kuna mtu ataiba huku akiomba Mungu amfanikishe, huyu anamchukulia Mungu kama msela wake.

Kuna mwingine akiiba anajihukumu sana, anajuta na kutubu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom